Ester Bulaya: Prof Magembe ni mwepesi kama 'tishu'!

mpk

JF-Expert Member
Sep 26, 2012
3,115
3,863
Mbunge wa Bunda mjini Ester Bulaya jana alivuruga bunge baada ya kusema Prof Maghembe ni mzigo mwepesi kama tishu. "Huyu waziri aliwahi kuitwa mzigo na Kinana na kweli ni mzigo tena mwepesi kama tishu" alisema Bulaya.

Kauli hiyo ilimuinua Muhagama aliyetaka Bulaya afute kauli hiyo kwani ni ya kuudhi lakini Bulaya alikataa kufuta kauli hiyo kwa kusema mbunge hachaguliwi cha kusema.
 
Daaah! Tishu ya napkin au t.p?? Regardless, nadhani kulikuwa hakuna haja ya kutumia hilo neno. Ni mtazamo wangu tu!!
 
Safi tu ni katika kuhakikisha kuwa viongozi wazembe wanachapa kazi kwahiyo lazima kuwa na lugha za kutiana jazba kidogo,we utanuna huku kitaa wenzio wakimaliza session wanakaa pamoja wanapiga story wakati nyie huku mnataka kushikana mashati
 
Upinzani Bungeni, naomba muache kuwaiga wenye vijembe na kejeli, mjuwe huku nje tunawategemea kwa busara zenu msikate tamaa.
 
Upinzani Bungeni, naomba muache kuwaiga wenye vijembe na kejeli, mjuwe huku nje tunawategemea kwa busara zenu msikate tamaa.
Sie tunawapa vijembe vya kuwaongezea hamasa ndo anatakiwa apambane aoneshe kuwa sio mwepesi kama ile ya TP
 
Hiv mbona ccm hawaeleweki? Yule mlinga wa ulanga mbona alitoa lugha ya kuudhi wakapiga makofi? Arrrgh inakera sn kujifanya wao ni malaika.ebooo
 
Iv I aliesema wabunge wa viti maalumu upinzani ni kipoozeo alichukuliwa hatua gani?hayo hayakuwa maneno yakuuzii?

mbona muhagama hakumwambia mtoa kauli afute kwa kua matamshi aliyotoa yalikuwa yakuuzi
 
Back
Top Bottom