Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Uongo mtupu.

Mtamtafuta sana mwana wa mwenzenu hamumpati ng'oo. Mahasidi wakubwa.

Mmemtafuta miaka 9 hamjampata mtampata leo imebaki miezi 9? Mnanchekesha.

Nakuambia kikwete atakamatwa kabla hajavuka viwanja vya Jimukana.
 
Zungu Pule Nadhani Umeisoma hiyo taarifa vizuri... Na Unajua ya kuwa Prof. Tibaijuka hakuwa kwenye hiyo campaign ya kuidhuru serikali ya nchi yetu kwa hiyo mikataba dhaifu; Ila alipewa pesa kama watu zaidi ya 40 kwenye Account zao, wako wa kila aina... lakini ni kwanini yeye kuchaguliwa kati ya hao 40 ndani ya serikali --- that's when SCAPEGOAT comes...

Yeah... sijasema hana Makosa kupokea hizo pesa kama kiongozi wa serikali bila kujua undani wake ni kuwa UNETHICAL --- na kuwa kiongozi wa serikali tukufu unatakiwa kuwa ETHICAL... kuondolewa Uwaziri ungetosha kabisa na kama watatumia njia za kutaka pesa zirudishwe ni kumuandama the main known culprit or culprits...

As you know...
There may be times when we are powerless to prevent injustice, but there must never be a time when we fail to protest.
 
uzombi huu utaisha lini??
 
Agenda kuu ktk uchaguzi 2015 nikuwa RAISI JK kutoka CCM kaiba pesa za wananchi, hili lazima liingie vizuri kwenye vichwa vya wananchi na lazima lihubiriwe kila kona na kila pembe ya nchi
 
Tibaijuaka kupelekwa mahakamani siyo tija tayari jk alisema siyo pesa ya umma sasa anapeleka watu mahakamani kwa lipi totally hii ni contradiction ya hali ya juu.
 
Ninavyojua mimi ni kwamba Anna Tibaijuka hakuiba hizo pesa bali alipewa zilizoibiwa. Sina uhakika kama alijua kuwa anapewa pesa zilizoibiwa au la. Swali langu ni hili: Kwa kuwa Tibaijuka alikuwa muwazi na akatwambia huyo aliyempa pesa (zilizoibiwa), kwa nini huyo aliyetoa hizo pesa za wizi asibebeshwe mzigo wa huo wizi? Kujaribu kumfanya Anna aonekane kuwa ndo mwizi ni kumfunya kuwa mbuzi wa kafara tu.
 
Tibaijuaka kupelekwa mahakamani siyo tija tayari jk alisema siyo pesa ya umma sasa anapeleka watu mahakamani kwa lipi totally hii ni contradiction ya hali ya juu.

Wewe umekuwa Jaji mkuu? Mtu amekula rushwa na hilo ni kosa kisheria. Unazungumzia tija gani? Na haki inapatikana mahakamani. Kwanini mnaogopa huyu Mama kufikishwa mahakamani? Kama kweli yeye ni safi kama anavyodai, kwanini anaogopa mahakama?
 
Unachanganya. Tibaijuka amekula rushwa. Haijalishi kama pesa zimeibiwa au la. That is source ya hela za mtoa rushwa si hoja hapa. Jiulize, mbona hukupewa wewe hizo billion 1.6? Au wewe ulikuwa huhitaji?
 
tunataka wahumiwa Wote kuanzia werema mpaka muhongo
 
Tibaijuka alipokea rushwa, bila kujali "undani" wa fedha alizopokea. Watu wanachanganya kitendo cha kupokea rushwa na chanzo cha fedha zilizotumika. Hivi ni vitu viwili tofauti. Je unamaana kuwa kama fedha alizopokea Tibaijuka zisingekuwa zimetoka kwenye akaunti ya escrow, basi ingekuwa ethical kwake kupokea fedha hizo? Au TAKUKURU wasingenyanyua bendera kuashiria kuwa kiongozi kapokea mlungula kinyume cha sheria?
 
Unachanganya. Tibaijuka amekula rushwa. Haijalishi kama pesa zimeibiwa au la. That is source ya hela za mtoa rushwa si hoja hapa. Jiulize, mbona hukupewa wewe hizo billion 1.6? Au wewe ulikuwa huhitaji?

​Kama hiyo ni rushwa, kwa nini mtoa rushwa haguswi badala yake kosa lote anabebeshwa mpokeaji tu?
 
ot Lady;11724321]Kubenea anahangaika sana. Fedha za Reginald Mengi alizolamba kushinikiza Muhongo afukuzwe anaona kuwa zinataka kumtokea puani[/QUOTE]tupe facts
 
​Kama hiyo ni rushwa, kwa nini mtoa rushwa haguswi badala yake kosa lote anabebeshwa mpokeaji tu?

Hayo ndiyo maswali unayopaswa kuuliza. Na si kusema huyu mama hastahili kuchukuliwa hatua za kisheria. Kutokuchukuliwa hatua kwa mtoaji hakufuti makosa ya mpokeaji (They will not be tried jointly.). Makosa ya mtoa rushwa hawezi kubebeshwa mpokeaji. Haliko hivyo. Huyu mama, kama atashtakiwa, atashtakiwa kwa kosa la kupokea rushwa na si kutoa rushwa. Si umefuatilia mashtaka ya wale wengine yanavyosomeka? Kwamba, mnamo tarehe 2 February 2014 majira ya saa nne asubuhi kwenye maeneo ya Benki ya Mkombozi, Mshitakiwa Anna Tibaijuka alipokea rushwa ya Shillingi 1.6 billioni kutoka kwa James Rugemalira kinyume na Sheria ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…