Escrow kumuumbua Rais Kikwete

Ni aibu! aibu! aibu!.....ikulu kuwa pango la wanyanganyi! Hati jk anasema pesa siyo ya umma....Mwigulu anawatumia ankara za kodi waliochukua pesa za escrow.....jk anashindwa kutekeleza maamuzi ya bunge la jamuhuri ya muhungano wa Tanzania.

Nashangaaa wanaojitoa ufahamu kutetea upuuzi huu. Na ni mshukuru Muhongo kugoma kujiuzuru wakati akijua anayemwsjibisha naye mwizi kama yeye. Mguse muone 'kama ardhi ya Tazania haita tetemeka!
 
Unaweza kunieleza kuwa werema aliiba kiasi gani kwenye hiyo ac?

Nenda pale STANBIC utapata jibu,si mmekalia report ya waliochota kule,subiri iletwe hapa JF utapata kizunguzungu
 

Kosa kubwa alilofanya Mkulu ni kukaribisha wahaya ikulu na kujiweka karibu nao. Serikali zilizopita ilikuwa kinyume chake!
 
Yote kwa yote kama be mkubwa anaonewa aseme ukweli coz anaujua then wananch 2tamkingia kifua, hatutak ambwele vjiwen
 
Uongo mtupu.

Mtamtafuta sana mwana wa mwenzenu hamumpati ng'oo. Mahasidi wakubwa.

Mmemtafuta miaka 9 hamjampata mtampata leo imebaki miezi 9? Mnanchekesha.
 

Hukuielewa ripoti ya PAC kama uliisoma.Kuna pesa ilikuwa inalipwa IPTL moja kwa moja. Hivyo hizo bil 306 toa izo bil 202 ujue hicho kiasi kilichokuwa kimelipwa IPTL moja kwa moja.
 
Nenda pale STANBIC utapata jibu,si mmekalia report ya waliochota kule,subiri iletwe hapa JF utapata kizunguzungu

Hao ni malaika wa ccm majina yao yakiwekwa wazi nchi itatisika
 
Kwani kwenye ripoti ya CAG na TAKUKURU kuna mahala amehusishwa Rais KIKWETE?

...tumia akili wewe, kwa nini Filikunjombe aliwakataza wabunge kumuhusisha rais na akasema haitakuwa rahisi kumshughulikia rais bila nchi kuyumba?
Kulikuwa na haja gani kwa yeye katoa tahadhali hiyo?
 
Wametolewa sadaka waliopitishiwa mpunga mkombozi, wale wa stanbic wamewekwa kiporo. Kule waliko dereva wa tax asombe kwa trip kwa ijira wa mil 15, zilifungwa kwny viroba maalum
 

Well, hapa unachanganya mambo. Hapa ni kama vile unamtetea Tibaijuka. Ukweli ni kwamba Tibaijuka amekula mlungula na anapaswa kuchukuliwa hatua. Vivyo hivyo, Chenge amekula mlungula na anapaswa kuchukuliwa hatua. Kutokujadiliwa kwa "Chenge huko CC aondoke kwenye CCM"[sic] hakufuti makosa ya Tibaijuka. Unachopaswa kufanya ni kushinikiza kusiwe na double standards na wote waliovunja sheria za nchi wachukuliwe hatua badala ya kutumia kutochukuliwa hatua kwa mkosaji mmoja kufuta au kuhalalisha makosa ya mwingine.

According to Oxford Dictionary, scapegoat means a person who is blamed for something bad that somebody else has done or for some failure. Sasa kwenye hili, Tibaijuka hawezi kuwa scapegoat. Ni kweli alihongwa shillingi 1.6 billion na lazima achukuliwe hatua za kisheria. Matumizi yako ya neno scapegoat hapa yanaonesha kuwa unashangaa kwa nini hawamlindi Tibaijuka kama wanavyomlinda Chenge? Kwa maneno mengine, unataka waendeleze utaratibu wao mchafu wa kulindana. Tusingependa walindane bali kila mtu abebe mzigo wake.
 
Na akiondoka aiache list ya wauza unga ofisini ama sivyo atakamatwa kabla hajavuka Makumbusho on the way to Msoga.

Ndiyo maana ningependa Rais ajaye awe ni mtu mwenye sifa na utashi wa kurejea madudu yote haya na kuwashughulikia ipasavyo (ikiwa ni pamoja na kutaifisha mali zao) wote waliohusika. Hata kama mtu alikuwa Rais, sheria inayomlinda itenguliwe na aadhibiwe ili iwe fundisho kwa wengine.
 
Siku Kikwete akimaliza muda wake pale magogoni cha moto atakiona, hawa watu hawatakubali kupelekeshwa puta ilihali mwizi mkuu wanamjua
 
Siku Kikwete akimaliza muda wake pale magogoni cha moto atakiona, hawa watu hawatakubali kupelekeshwa puta ilihali mwizi mkuu wanamjua

Kwanza handover process itabidi Ambulance iwe inawaka muda wote.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…