Escrow ilipoa,TAKUKURU wanaipasha

Escrow ilipoa,TAKUKURU wanaipasha

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2010
Posts
6,140
Reaction score
18,004
Rais alishaeleza kwa kirefu na kina sakata lote la Escrow. Pointi kubwa toka kwa Rais ni kuwa pesa za Escrow hazikuwa za umma. Zilikuwa za watu binafsi ambao ni IPTL. Tukasikia na kuelewa. Wapo waliobaki na maswali na majibu. Wapo waliobaki wakishangaa dhahiri au kwa kuhadaa.

Mambo yakapoa kama kiporo cha Profesa Muhongo. Hali ikatulia. Sasa,TAKUKURU wameanza kuwaburuza Mahakamani maafisa mbalimbali wa Serikali. Wanawahusisha moja kwa moja na kashfa ya Escrow. Kwamba,walipokea mlungula toka kwa wanufaika wa Escrow.

Maswali yanamea;majibu yanapotea. Mfano,iweje hongo iwe kwenye fedha halali na binafsi? TAKUKURU mnapasha moto kiporo cha Escrow. Hatutaacha kukila katika njaa ya ufahamu na kusaka ukweli tuliyonayo.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 
walio pelekwa mahakamani ni kondoo wa kafara, tunataka maafisa waandamizi wote washitakiwe bila kujali nafasi walizo nazo akiwemo HABINDER SINGH SETH
 
Kama hao wametoa rushwa je Mbona salio pokea ziiiiiii!! au wametoa rushwa na kupikia wenyewe....!!!!. Napita naomba nisitafutwe
 
TAKUKURU wanazidi kuihujumu 'Tawala', wananchi wanazidi kupandwa na hasira....! Na safari hii hakuna kupinga matokeo....! Kinaeleweka kabla ya uapishaji.
 
Back
Top Bottom