Eric Shigongo....Hapa umepitiliza ! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Eric Shigongo....Hapa umepitiliza !

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Kizimkazimkuu, Mar 12, 2012.

 1. Kizimkazimkuu

  Kizimkazimkuu JF-Expert Member

  #1
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 8, 2007
  Messages: 336
  Likes Received: 51
  Trophy Points: 45
  Nimesikitishwa sana na habari iliyochapishwa na gazeti la Ijumaa wikienda (Global publishers) inayohusu watotot walioenda mahakamani kumlilia mtoto wao ambaye ni mtuhumiwa wa biashara ya ukahaba. Kitendo cha kuwapiga picha, kuwataja majina na wanapoishi na kusoma si dhani kama ni sahihi. Watoto hawa leo wataanza kuitwa watoto wa changudoa mitaani na shule. I can imagine mateso ya kisaikolojia watakayoyapata na naweza kufikiria madhara ya muda mrefu yatakayoombatana na kadhia hii. Habari hii ingeweza kukamilika na kueleweka pasipo kuweka majina na picha za watoto hawa. Tumeshuhudia mara kadhaa mkiandika habari za maneno kama "kigogo fulani", jina kapuni nk...kwa nini haikuwa hivi kwa watoto hawa. Kwa nature ya kazi yangu nimekutana na watu wengi ambao leo wanaishi maisha ya tabu kwa kuwa waliacha shule.....na moja ya savavu kubwa ni kunyanyaswa kwa namna moja au nyingine. halii hii hupeleka mtu kukua huku amekosa "kujiamini" (self esteem). hali hii ina madhara makubwa sana katika maisha yetu ya kila siku...tabia zetu, uwezo wa kufanya maamuzi, uongozi nk hujengwa katika kipindi mtoto anakua. Nawasikitikia sana hawa watoto.....habari hii iko hapa
   
 2. J

  JATELO1 JF-Expert Member

  #2
  Mar 12, 2012
  Joined: Oct 31, 2011
  Messages: 1,235
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 145
  Ndugu yangu;
  Hata mimi napata shida sana kwa maandishi kama haya ambayo ni hakika yanakuwa na longterm effects kwenye maisha ya watoto hao. Nashindwa kuelewa nini makusudi ya mwandishi kama huyu. Je hata Mhariri wa gazeti hili hakuweza kuona hili? Hivi Global Publishers wanafanya hivi kwasababu hawa WATOTO hawana uwezo wa kuwafungulia kesi ya madai Mahakamani?

  Nafikiri waandishi wa habari wa aina hii wanapaswa kurudi Shule ili kuweza kujua msingi wa kuandika habari. Hii hali imeniumiza sana na kama ningekuwa LAWYER by profession, hakika ningejitolea kusimamia kesi kwa niaba ya hawa Watoto hawa dhidi ya GLOBAL PUBLISHERS.
   
 3. Memo

  Memo JF-Expert Member

  #3
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 2,147
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Shigongo ni aina ya vijana wakati n wenye tamaa ya hela na madaraka.
  Shigongo hajui ethics za kazi yake.
  Shigongo hafai kwa Hanoi ya utandawzi lei
  Mujini huyu wa ccm ambae ni good for nothing!
   
 4. S

  Sojochris Member

  #4
  Mar 12, 2012
  Joined: Jan 28, 2012
  Messages: 27
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  "watoto walioenda mahakamani kumlilia mtoto wao" anyway but it confuse.
   
 5. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #5
  Mar 12, 2012
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  yote hii itakwisha kama tutakuwa na specific Privacy Law au data protection law.
  sheria hii tatizo hata kama itapitishwa na bunge lazima ipelekwe
  Umoja wa Ulaya ambako kuna kitu wanakiita working party chini ya
  kifungu 29 cha Data Protection Directive ambao ndio wanaahakiki kama
  sheria tutakayopitisha itaendana na matakwa yao of kozi ni biashara
  zaidi kwa kuwa kuna restrictions za data flow kutoka europe kwenda
  3rd world countries.Ikumbukwe hata China,japan,austarlia na USA sheria
  zao za data protection zimehakikiwa na hawa jamaa wa ulaya kwa
  hivo utaona kuna mwingiliano wa kiutawala
  kwa ufupi sheria hizi zinatoa mipaka hata kwa wanahabari kutumia
  picha au habari za mtu bila idhini yake sembuse watoto.
  Ni mda sasa wa kuwalilia wabunge wafanye hiyo kazi,
  Hata hivo mhanga wa hili jambo bado anaweza kutumia
  sheria zingine kama penal code au katiba kupinga suala hili
  la wanahabari kuuza magazeri kwa kuharibu au kuingilia uhuru wa mtu binafsi.
   
 6. THK DJAYZZ

  THK DJAYZZ JF-Expert Member

  #6
  Mar 13, 2012
  Joined: Sep 14, 2011
  Messages: 2,144
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 145
  Searching...100%
  Loading...100%
  Network Connected !

  Kwa hili Shigongo amechemsha.
   
 7. MissyNana

  MissyNana Member

  #7
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 29, 2011
  Messages: 40
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Halafu anasema "IN GOD WE TRUST" kweli????Huyu angesema "in money we trust" ni lazima pesa aipate kwa njia yoyote ile. Hafuati maadili ya uandishi kabisa. Ni kuharibia wau maisha yao tu.
   
 8. arabianfalcon

  arabianfalcon JF-Expert Member

  #8
  Mar 13, 2012
  Joined: Oct 19, 2010
  Messages: 2,292
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Asowake ana Mungu.....
   
 9. Bosi Michembe

  Bosi Michembe JF-Expert Member

  #9
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 24, 2011
  Messages: 273
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Mambo ya mpuuzi anaejiita Shakespeare wa bongo.. Shule na exposure muhimu sana ndugu zangu kutokea kuuza magazeti Pamba road Mwanza na kuja mjini imekuwa balaa. Kama hawezi au anaona aibu kurudi shule angesoma hata kale kakitabu ka Ethics za uandishi kalikotolewa na media council kangemsaidia..
   
 10. O

  OMEGA JF-Expert Member

  #10
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 12, 2011
  Messages: 671
  Likes Received: 106
  Trophy Points: 60
  Msamehe bure kwani tatizo ni elimu yake
   
 11. CAMARADERIE

  CAMARADERIE JF-Expert Member

  #11
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 3, 2011
  Messages: 4,427
  Likes Received: 158
  Trophy Points: 160
  Ni uchungu wa kiuzazi tu naamini alimaanisha "watoto walioenda mahakamani kumlilia mama yao"
   
 12. elmagnifico

  elmagnifico JF-Expert Member

  #12
  Mar 13, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 7,913
  Likes Received: 7,458
  Trophy Points: 280
  hata mimi niliposoma hiyo habari nilistaajabu kuona picha za hao watoto bila hata kufichwa sura zao. Halafu shogongo naye ni after money hana cha ulokole wala nini. Kuna mambo mengi yanaandikwa na magazeti yake yanakuwa na uongo mwingi nishaona vitu kibao anavitoa kwenye mtandao vimetokea nchi za jirani huko anadai ni hapa bongo.
  He is real after money na madaraka but sometimes anakosea may be because naye ni binadamu but he got to watch his steps
   
 13. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #13
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,874
  Likes Received: 6,228
  Trophy Points: 280
  shigongo ni janga la taifa, na magazeti yake yaliyojaa ngono.....anaharibu watoto wa kizazi hiki
   
 14. Josephine03

  Josephine03 JF-Expert Member

  #14
  Mar 13, 2012
  Joined: Feb 7, 2012
  Messages: 752
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Mnatabia ya kulalamika kuna kabila linapenda pesa je na yeye ni mmoja wapo?
   
 15. BPM

  BPM JF-Expert Member

  #15
  Mar 13, 2012
  Joined: Mar 10, 2011
  Messages: 2,766
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  nadhani kwa sasa anatumia picha za matukio mengi kuvutia biashara yake .. imefikia hatu hadi kuchukua picha kwenye Facebook na kuweka kwenye magazeti kuonyesha mahusiano mbali mbali
   
 16. Gwankaja Gwakilingo

  Gwankaja Gwakilingo JF-Expert Member

  #16
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 26, 2012
  Messages: 1,963
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 145
  Ndio madhara ya kukumbatiwa na Magamba.Awaombe radhi watoto pamoja na mama yao tena kupitia Kurasa za mbele za magaazeti yake na gaazeti la serikali.mpuuzi sana huyu kijana,yale magaazet huwa hayahaririwi yele
   
 17. H

  Huihui2 JF-Expert Member

  #17
  Mar 13, 2012
  Joined: Jan 5, 2012
  Messages: 395
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Hapa ndiyo TAMWA ya Ananilea Nkya na LHRC ya Helen Kijo Bisimba walipaswa kuonyesha ubavu wao
   
 18. M

  MIGNON JF-Expert Member

  #18
  Mar 13, 2012
  Joined: Nov 23, 2009
  Messages: 2,587
  Likes Received: 1,563
  Trophy Points: 280
  Umeandika vizuri mno.Kwenye vigogo hawatajwi ila kwa maskini,majina na mtaa unatajwa.
  Mungu anisamehe lakini simpendi Shigongo kwani hujipatia pesa kwa ujanja tu.
  Magazeti yake mengi vichwa na habari na habari iliyomo ndani ni tofauti au haina uzito unaolingana.
   
 19. j

  joe peters Member

  #19
  Mar 13, 2012
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 85
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 13
  Mkuu huwa wanasema "In GOD we trust all others pay CASH"
   
 20. trachomatis

  trachomatis JF-Expert Member

  #20
  Mar 13, 2012
  Joined: Jun 7, 2011
  Messages: 3,653
  Likes Received: 93
  Trophy Points: 145
  Hata mimi sijaelewa... Au mama yao si mtoto wao...
   
Loading...