kekuwetu
JF-Expert Member
- Oct 24, 2010
- 327
- 98
Kaka Eric James Shigongo(Mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali) nimeamua kutumia njia hii kufikisha ujumbe kwako, ninaamini ujumbe wangu utaufanyia kazi na hautaudharau (nakufahamu wewe si mtu wa dharau).
Kwanza naomba nikueleze kwa ufupi jinsi nilivyokufahamu.Kaka Eric, nataka ufahamu wewe ni mmoja wa watu ninaowaheshimu sana(ingawa sijawai kukutana na wewe) mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa hadithi zako, nakumbuka nilianza kuzifuatilia hadithi zako nikiwa primary school wakati huu ilikuwa ni kwenye gazeti la KIU kabla hujaamua rasmi kulitosa na kuimarisha kampuni yako ya global publisher.
Kuna kipindi (samahani, sikumbuki vizuri, uligusia histori ya maisha yako yalivyokuwa, mapito uliyopitia ukiwa mtoto na mahali ulipo, kaka Eric hapo nilianza kukufahamu vizuri.
Kwanza una hofu ya Mungu ( wewe ni mcha Mungu mzuri), pili wewe ni mtu wa malengo, na una nia na dhamira kuhakikisha malengo unayoweka yanatimia, si mtu wa kukata tamaa haraka, (kwa hilo naomba nikupongeze) naamini hari yako hiyo imechochea kwa kiasi kikubwa mafanikio uliyonayo na ninaamini utafika mbali kimafanikio zaidi ya ulipo sasa kama utaenda kwa kasi hiyo hiyo.Sasa naomba nije kwenye mada iliyosababisha nikuandikie waraka huu. Kaka Eric James Shigongo ulitoka wapi na CCM mpaka kuamua kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM Buchosa 2010?:angry: Niliposikia umejitosa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM niliudhunika sana, nilijua una nafasi kubwa ya kuwa Mbunge Buchosa, Nilijua wana Buchosa wangependa uwe mbunge wao, nilikuwa nafuatilia habari za kampeni zinavyoendelea Buchosa, (soma baadhi ya vicha vya habari kwenye magazeti) "Shigongo arudisha fomu ya ubunge kwa matumaini""Shigongo kama Obama Buchosa""SHIGONGO AIPASUA CUF BUCHOSA"Nilifahamu mapema kushinda utashinda ila haki hutapewa, kuchakachuliwa CCM ni moja ya fani yao, CCM haipendi haki, haukuwa chaguo lao, walikuwa wamesha muandaa mtu wao.
Ndio maana Rais alitamka wazi kwenye kampeni kuwa wewe ulisogeza mpaka wake wa shamba bagamoyo. (sasa hapo sifahamu kati yako na Rais nani alimuibia mwenzake) jibu unalo wewe.Sitaki kuongea sana sababu mimi sio mwandishi wa habari, ushauri wangu ni kuwa bado una nafasi kaka, please please badilisha mawazo yako, nakushauri jiunge na Chadema kuanzia sasa.
CDM inahitaji wapambanaji kama wewe, usiwaangushe watu wa Buchosa tena, weka nia ya kugombea Buchosa kwa tiketi ya CDM, nakuakikishia kaka unapendwa sana huko, hawatakuangusha kaka, fanya hima bado una nafasi, wana Buchosa wanataka kukuona ukiwapigania bungeni, huyo waliyowekewa yupo usingizini hana nia wala dhamira ya kuwatetea wana Buchosa.
Naamini utaufikiria ushauri wangu na ninategemea kukuona UKIVUA GAMBA NA KUVAA GWANDA. Karibu CDM mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali Eric James Shigongo.:clap2: