Eric James Shigongo, pls 2015 gombea ubunge Buchosa kwa tiketi ya CDM

kekuwetu

JF-Expert Member
Oct 24, 2010
327
98
Kaka Eric James Shigongo(Mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali) nimeamua kutumia njia hii kufikisha ujumbe kwako, ninaamini ujumbe wangu utaufanyia kazi na hautaudharau (nakufahamu wewe si mtu wa dharau).

Kwanza naomba nikueleze kwa ufupi jinsi nilivyokufahamu.Kaka Eric, nataka ufahamu wewe ni mmoja wa watu ninaowaheshimu sana(ingawa sijawai kukutana na wewe) mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa hadithi zako, nakumbuka nilianza kuzifuatilia hadithi zako nikiwa primary school wakati huu ilikuwa ni kwenye gazeti la KIU kabla hujaamua rasmi kulitosa na kuimarisha kampuni yako ya global publisher.

Kuna kipindi (samahani, sikumbuki vizuri, uligusia histori ya maisha yako yalivyokuwa, mapito uliyopitia ukiwa mtoto na mahali ulipo, kaka Eric hapo nilianza kukufahamu vizuri.

Kwanza una hofu ya Mungu ( wewe ni mcha Mungu mzuri), pili wewe ni mtu wa malengo, na una nia na dhamira kuhakikisha malengo unayoweka yanatimia, si mtu wa kukata tamaa haraka, (kwa hilo naomba nikupongeze) naamini hari yako hiyo imechochea kwa kiasi kikubwa mafanikio uliyonayo na ninaamini utafika mbali kimafanikio zaidi ya ulipo sasa kama utaenda kwa kasi hiyo hiyo.Sasa naomba nije kwenye mada iliyosababisha nikuandikie waraka huu. Kaka Eric James Shigongo ulitoka wapi na CCM mpaka kuamua kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM Buchosa 2010?:angry: Niliposikia umejitosa kugombea ubunge kwa tiketi ya CCM niliudhunika sana, nilijua una nafasi kubwa ya kuwa Mbunge Buchosa, Nilijua wana Buchosa wangependa uwe mbunge wao, nilikuwa nafuatilia habari za kampeni zinavyoendelea Buchosa, (soma baadhi ya vicha vya habari kwenye magazeti) "Shigongo arudisha fomu ya ubunge kwa matumaini""Shigongo kama Obama Buchosa""SHIGONGO AIPASUA CUF BUCHOSA"Nilifahamu mapema kushinda utashinda ila haki hutapewa, kuchakachuliwa CCM ni moja ya fani yao, CCM haipendi haki, haukuwa chaguo lao, walikuwa wamesha muandaa mtu wao.

Ndio maana Rais alitamka wazi kwenye kampeni kuwa wewe ulisogeza mpaka wake wa shamba bagamoyo. (sasa hapo sifahamu kati yako na Rais nani alimuibia mwenzake) jibu unalo wewe.Sitaki kuongea sana sababu mimi sio mwandishi wa habari, ushauri wangu ni kuwa bado una nafasi kaka, please please badilisha mawazo yako, nakushauri jiunge na Chadema kuanzia sasa.

CDM inahitaji wapambanaji kama wewe, usiwaangushe watu wa Buchosa tena, weka nia ya kugombea Buchosa kwa tiketi ya CDM, nakuakikishia kaka unapendwa sana huko, hawatakuangusha kaka, fanya hima bado una nafasi, wana Buchosa wanataka kukuona ukiwapigania bungeni, huyo waliyowekewa yupo usingizini hana nia wala dhamira ya kuwatetea wana Buchosa.

Naamini utaufikiria ushauri wangu na ninategemea kukuona UKIVUA GAMBA NA KUVAA GWANDA. Karibu CDM mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali Eric James Shigongo.:clap2:
 
Kaka Eric James Shigongo(Mwalimu wa kimataifa wa ujasiriamali) nimeamua kutumia njia hii kufikisha ujumbe kwako, ninaamini ujumbe wangu utaufanyia kazi na hautaudharau (nakufahamu wewe si mtu wa dharau). Kwanza naomba nikueleze kwa ufupi jinsi nilivyokufahamu...

Utakuwa Eric Shigongo wewe; unataka kujua mawazo ya wana JF!
 
Nafikiri ni jukumu la wana Buchosha kuamua kama wana muhitaji uamuzi uko mikononi mwao.
 
Nafikiri ni jukumu la wana Buchosha kuamua kama wana muhitaji uamuzi uko mikononi mwao.

mkuu BUCHOSA tunamtu wetu mh KASWAHILI sema magamba walimchakachua! hili nijembe! huyo mtu wa magazeti hatumtaki kwanza alitoa rushwa sana japo kuwa baadaye nayeye walimpiga chini magamba wenzie kwahila! kama wasingeiba kura kule visiwani kwakukosa ulinzi! TIZEBA asingekuwa mbunge BUCHOSA!
 
Mie pia nakubaliana na wewe kwamba anaonekana ni mtu makini pamoja na kwamba ana mambo mengi chini ya kapeti ambayo si vema kuyaweka hapa ila ni mchapa kazi hilo halina ubishi na kwa kuwa una ushahidi huo basi nafikiri ushauri wako ataupata.
 
eti nini? Shigongo kama Obama....ha ha ha ha

Kwa sentesi fupi kabisa, Eric Shigongo HAFAI kuwa kiongozi wa jamii iwe kupitia CCM au chama kingine chochote. Ninadikiriki kumuita MNAFIKI, akijinasibu kama mlokole na wakati huo huo magazeti yake yakiongoza kwa kuandika kinyume na maadili na utamaduni wa Mtanzania. Kuna tofauti ndogo sana kama ipo kati ya Shigongo na muuza dawa za kulevya
 
Mkuu umemaliza. Muanzisha thread anatumia forum Kama kipima joto.
 
huyo hafai saa zote yupo dar hata hana asili ya kusaidia wananchi....niliwahi kusikia magamba wenzake wakimkandia ana tabia mbaya
 
eti nini? Shigongo kama Obama....ha ha ha ha

Kwa sentesi fupi kabisa, Eric Shigongo HAFAI kuwa kiongozi wa jamii iwe kupitia CCM au chama kingine chochote. Ninadikiriki kumuita MNAFIKI, akijinasibu kama mlokole na wakati huo huo magazeti yake yakiongoza kwa kuandika kinyume na maadili na utamaduni wa Mtanzania. Kuna tofauti ndogo sana kama ipo kati ya Shigongo na muuza dawa za kulevya
Niliwahi kuandika hapa kuwa binafsi simpendi huyu Bwana kwani anajifanya mtoa ushauri nasaha lakini si mkweli na hajiweki katika hali yake halisia.Kuwa mtu wa Mungu wakati kipato chako kinatokana na ujasusi katika maisha ya watu.
Kuharibu hata pale ambapo suluhu ingeweza kufanya kazi kwa ku pubilicise mambo ambayo hata hayana faida.
Kuna aliyesema hana tofauti na muuza madawa ya kulevya lakini mimi nasema hana tofauti na wamiliki wa ze utamu.
 
Dah... Kweli wa TZ tupo desperate sasa, hivi Shigongo ana political and leadership acumen kweli?
 
Dah... Kweli wa TZ tupo desperate sasa, hivi Shigongo ana political and leadership acumen kweli?

Mkuu aligombea 2010 kupitia CCM kwenye kura za maoni alipigwa chini na nilivutika kuhudhuria kampeni zake cha ajabu hana anachokifahamu kwenye medani hii ya kisiasa.
hajui yuko kwenye jamii ipi na inahitaji nini na kwa wakati upi, binafsi hana jipya.
 
Sio kila MTU maarufu anaweza kuwa mwanasiasa.....huyu mzee WA udaku anachojua ni umbea tu na kuchunguza mambo ya watu. Abaki tu kwenye maudaku yake....kwanza ni mmoja kati ya waTz walio'play ROLE KUBWA katika kuharibu MAADILI SAFI ya WATANZANIA, maadili yaliyoasisiwa na Mwalimu Nyerere. 2mi he's an Opportunist who doesn't give a sh**t......He can do whatever in order 2get what he want that's it.
(this my personal thought)
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom