Epuka kuachana vibaya na x-boy/girl friend wako

Kakole

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
2,094
1,745
Natumai wote mu wazima wa afya njema,

Namshukuru sana Mungu kwa hekima ilikuwa mwaka 2008 mwanzoni nilipoachana na g'friend
wangu ambae kwakweli nilimpenda sana kiasi kwamba najiulizaga ingekuwaje kama tungefanikiwa
kuoana maana nanzani angeweza hata kunifanya mume bwege kama endapo tungeoana.

Nakumbuka tuliachana baada ya yeye kwenda chuo halafu mimi sikufanikiwa kwenda chuo mwaka huo baada ya kutoqulify kupata mkopo hivyo nikawa nabangaiza maisha kwenye kampuni moja binafsi ya kimataifa mjini Dar, kiujumla alijua kuwa nampenda sana na kitendo cha mimi na yeye kushindwana kilinifanya nikose usingizi siku mbili mfululizo mpaka ilinibidi niombe annual leave ili kunusuru uwezekano wa mimi kuharibu kazi, kuna siku nilifanikiwa kuonana na x-g'friend wangu huyu na katika kubadilishana mawazo na ndipo nikagundua anaweza kuwa msaada sana kwangu kulingana na shughuli anazofanya kwa sasa ila uwezekano wa kurudiana haupo we remained as just a normal friends.

Sasa najiuliza endapo kama ningemtukanatukana kipindi hicho au kuachana kwa shari kubwa ingekuwaje? ukiona umeshindwana na mtu kubali matokeo maana kuna kitu kizuri Mungu amepanga juu yako, usilazimishe maji kupanda mlima.

Nawasilisha!
 
Kuna mwingine hakutukani matusi ila matendo yake kwako ni Matusi tena kuvuana nguo
Mwingine siri zako zote anaenda kuzibwaga kwa marafiki na hawara zake au watu wa karibu zikikufikia si Bora unitukane yatapepea kuliko kunichoresha aisee ... Mie nikikutana nae namwagia uji wa moto ababuke kima huyo
 
Huko ndio kuachana vibaya sasa ambako inapaswa kuepukwe sana onyesha njia mkuu usimpe mtu credit ni bora umpe nafasi aende salama ili huko mbeleni umpe deni la kukukumbuka kwa mazuri ni sii mabaya.
 
Huko ndio kuachana vibaya sasa ambako inapaswa kuepukwe sana onyesha njia mkuu usimpe mtu credit ni bora umpe nafasi aende salama ili huko mbeleni umpe deni la kukukumbuka kwa mazuri ni sii mabaya.
Mkuu we wasema tu ... Kuna mwingine hata shetani hamtambui kwa matendo yake Ana bahati mie sio mtoa roho!
 
Jana nimeachana na mchepuko wangu lakini, kwahiyo nisijibishane naye vibaya nitunze akiba ya kesho??
Basi sawa, ila inategemeana na mlivyoachana pia.
 
Hata kama hatokuja kunisaidia huko mbeleni, still sioni sababu ya kuwekeana chuki, visasi sijui vinyongo. Ukinikwaza yani ile yenyewe ntakachofanya ni "kukuignore" kikubwa tu, Maisha yanaendelea fresh tu. Hiyo energy ntakayotumia kukuchukia si bora niitumie kutengeneza mahusiano mazuri zaidi na watu wengine. "Thanks, it was good having you... best of luck",
 
You made a good point mkuu, nakubaliana na ww 100%
 
Mi sina Ex, Tukiachana SIKUJI, HUNIJUI OLE WAKO UJICHANGANYE KWENYE 18 ZANGU, nitakunyaliiiii mpaka kiranga chako chote komoooo.
Duuuuuh!!!!!!!!!!! kwa hiyo mkishaachana ni kama mmetangaza vita???
 
Kwahiyo huwezi kuwa na kumbukumbu yeyote kabisa kuwa uliwahi kuwa naye? lazima utakumbuka tu those good things you shared together wit him/her, kwanini ujenge uadui? @ Lara 1
 
Back
Top Bottom