PAYE
JF-Expert Member
- Jun 19, 2025
- 415
- 545
Arsenal, ambao ni vinara wa Ligi Kuu England (EPL), wamepoteza mchezo huo kwa mabao 2-1 dhidi ya Bournemouth katika dimba la Emirates. Matokeo hayo yanaifanya Arsenal kubaki na alama 70 baada ya kucheza michezo 32, huku wapinzani wao wa karibu, Manchester City, wakiwa na alama 61 na michezo 30.
Kupoteza huko kumeongeza presha katika mbio za ubingwa, hasa wakati tofauti ya alama ikiendelea kupungua kadri ligi inavyoelekea ukingoni.
Mchezo ujao wa Arsenal utakuwa mgumu zaidi kwani watakuwa ugenini katika dimba la Etihad, wakikabiliana na Manchester City katika mwendelezo wa ligi hiyo. Huo utakuwa mchezo muhimu sana katika kuamua hatima ya mbio za ubingwa