EPL ndiyo ligi bora duniani

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
Kesho nitamsimulia mwanangu umahiri wa Andres Iniesta wa kupiga pasi adhimu, Pasi tamu na ilikuwa ni faradhi kufurahi muda wowote ukimwona Iniesta na mpira. Utafurahi zaidi akiwa na Xavi pembeni wakimpelekea mpira yule Njiti wa Rosario Argentina Aufanye mpira Anavyotaka , awanyanyapae Mabeki na kuzichezesha Singeli Nyavu.

Screenshot_20210521-061959.png
Nitamsimulia mwanangu pia umahiri Wa CR7, Sjui itamchukua muda gani kuamini, kuwa mreno huyu Angekufunga popote anapopapenda Yeye. Makipa wote waliofungwa na CR7 sjawahi kuwalaumu. bali niliendeleza miiko yangu ya kumsifia mfungaji.

Na kwanini nisimsimulie mwanangu umahiri wa nliowashuhudia ilhali Babu yake, alinivuta mkono na kunipeleka kushuhudia michuano tele huku ngonjera za kuwasifu , wakina Beckham , Ronaldo de lima ,Zidane ,Ronaldinho, Steven Gerrad na wengine hazikumkauka katika mdomo wake popote awapo nami aongeleapo Kandanda, Kwa bahati mbaya Moyo wangu haukuchagua Timu aliyoipenda.

Alinifundisha kuupenda Mpira Naam, mchezo sahihi sana.

Maajabu ya Ligi Kuu ya Uingereza yalishtua ulimwengu wakati timu hizo zilipoamua kutawala mashindano ya Ulaya msimu wa 2018-19. hapo hapo Liverpool na Tottenham zilikabiliana katika Fainali ya Ligi ya Mabingwa (UEFA Champions League) kule mjini Madrid.

Nani angepinga sasa kama ligi hii haikuwa bora duniani kuliko nyingine?

Hata wale wayahudi wa kule Jerusalem na Nazareth waliokaidi mafundisho ya Bwana Yesu wasingethubutu kukukatalia miujiza na ubora wa ligi Hii .
Hata wakati mashabiki waliposhuhudia disco la Vijana wa London katika Fainali ya Europa League kati ya The Gunners na The Blues.

Fainali zile zilitawaliwa na watoto wa Uingereza.

Na ndiyo ilikuwa mara ya kwanza kabisa katika dunia hii ya mpira, kwa vilabu kutoka ligi hiyo hiyo kufika fainali zote mbili za Ulaya.

Hiyo pekee isingetosha kuliua na kulizika swali lisumbalo bongo za wengi katika kariba ya mpira.

Screenshot_20210521-062313.png


"Je, EPL ni bora zaidi ulimwenguni?

Ubora wa ligi hii umejibiwa tena, na watabe hawa wa Uingereza kukutana katika fainali nyingine tena 2021 hapa tunawazungumzia Vijana wa Mhispaniola Pep Guardiola na Vijana wa Darajani Chini ya Mjerumani Tuchel.

Naam,!
walistahili , walistahili kupita kwenda fainali na hapa ndipo wanapothibitisha kuwa ligi yao ni bora na Ngumu kuliko nyinginezo,.
Nusu fainali ya ligi ya Europa ilipokea waingereza wawili , lakini mwishowe fainali ikapata mwingireza mmoja , huku wengi wao kati ya wote wanaoufahamu mpira wakiwapigia upatu Mashetani wekundu kunyakua kindoo hicho vivyo hivyo nusu fainali ya UEFA, ilitoa waingereza wawili na mwishowe waingereza hao wanakutana Fainali.

Angefanya nini tena zidane pale anapomuona mjerumani Tuchel akimnyanyasa na kumwadhibu kwa kumtumia kijana wa Taifa kama la kwake , Kijana mfupi na Mweusi Mfaransa alietumwa kazi Ng'olo kante.

Kwa bahati mbaya Tuchel alikosa Roho ,ya Ukatili ile Roho ya Baba zake Wajerumani wakina Adolph Hitler , ile roho nyeusi isiyo na Doa jeupe la Usafi wa roho na Huruma ya nafsi, Laiti angemiliki roho hiyo hata kwenye chemba moja tu ya moyo wake ukiacha zile Nne , Basi Angempiga Zidane hata Goli sita.

Na ndiyo muda huu nikajiwazia na nafsi yangu Huenda sala na Dua za Zidane alizielekeza kwenye imani ya kwamba lolote litokee , Zile come back za Ronaldo , na maajabu ya kubeba Kombe la Mabingwa mara tatu mfululizo , kwa bahati mbaya hayo yote hayakutokea na yule Ronaldo hayupo tena Madrid. Na ile ndiyo tafsiri ya Mpira wenyewe sasa.

Kimavi hiki kimewapata pia vijana wa Ufaransa PSG , na Yule bishoo wao wa brazil na wachora tattoo wenzake wakina Mauro Icardi wanabaki wakiutazama tu Mnara eiffel pale Paris na pengine wanaomba ndiyo lingekuwa taji lenyewe lakini hilo nalo ni ndoto. wanabaki kukabana koo na Lille kwenye taji la ligi yao.

Na hatma ya mwanamwali huyu anakwenda kuolewa na wanaume kutoka ardhi ya malikia. Ungereza.

Ile ndiyo uingereza Ligi kuu na , ligi bora kuliko nyingine.

--Hapa kidogo nitajaribu kujibu , kwa maoni yangu sababu nyinginezo za kuifanya ligi hii kuwa Bora.

Screenshot_20210521-062223.png

1-WACHEZAJI WA KIMATAIFA
Hii ndiyo hoja yenye nguvu zaidi Kwangu EPL inazizidi kila ligi kuu ulimwenguni inapofikia idadi ya wachezaji walioitwa kwenye timu za kimataifa.

Klabu kubwa sita za EPL huwa na zaidi ya wachezaji 11 nwenye majukumu kimataifa. Hiyo inamaanisha kwamba wakati unatazama timu hizo kubwa sita zikicheza, unatazama wachezaji bora katika nchi zao na bahati mbaya Sunna hiyo haipo katika ligi nyingine yoyote.
Lakini kubwa zaidi Katika timu hizo za kimataifa ni zile zifanyavyo vyema katika Rank za Fifa

Aghalabu hii huwa inatokea katika ligi zingine, vile vile, lakini sio kwa kiwango sawa na kwenye EPL

Screenshot_20210521-062034.png

2-USHINDANI MKALI
Hakuna ataekataa , yakuwa ushindani ni mkali katika Ligi Kuu ya England kuliko ligi nyingine. Haiwezekani kutabiri matokeo ya Ligi Kuu kabla, kwani kila timu kubwa haswa zile sita ina nafasi nzuri ya kushinda. Juzi tu tumeshuhudia The blues akifa chini ya Gunners goli kutoka kwa kijana mdogo S.Rowe.

Pia kipigo alichopokea kutoka kwa Leicester city kwenye FA cup, haikutegemewa, mara nyingi ni nadra kutabiri na kupatia nani atachukua Taji.

Ligi zingine huko Ulaya mara nyingi ni mbio za farasi wawili, au kuna desturi na mila ya kilabu kimoja endelevu. Mfano Bayern Munich huko Bundesliga ni mfano mzuri. kwenye hekaya hii ya soka la wajerumani.

Liverpool, ambayo leo ni moja ya vilabu vyenye vipaji zaidi ulimwenguni na kocha mwenye weledi wa soka ilitumia miaka 30 kutafuta kombe la EPL.

Huwezi kufikiria kabisa kwa akili ya kawaida timu nyingine yenye kiwango cha ulimwengu. Katika ligi za Ulaya kama kingetumia miaka tajwa hapo juu bila mataji ya ligi ya ndani. Hiyo ni kawaida kabisa katika EPL, kwani kila mtu anaelewa jinsi ilivyo ngumu kushinda.
kongole kwao MAN city Msimu huu.

3 -VIWANGO VYA UEFA
EPL ina timu bora kwa ujumla kuliko ligi za kiwango cha juu huko Ulaya tumekiri baada ya fainali hii kukutanisha miamba ya Ligi yao , UEFA Club Coefficient Rankings imeweka ligi hii Katika rank ya kwanza.

Uingereza inaongoza kwa alama 100.140 ikifwatiwa na Uhispania ikiwa na alama 97. 712
Hoja hizo zinaonyesha jinsi vilabu vya jumla kutoka EPL vimekuwa vikifanya vyema kwa miaka kadhaa iliyopita hata sasa.

Mbali na kufanya vizuri katika ligi zao za ndani, vilabu hivi vinahitaji na bado vina kiu ya kutawala katika mashindano ya Ulaya, na kubeba mataji.

Nani ashangae?

Haiitaji miujiza ya nabii Musa ya kugeuza , fimbo kuwa nyoka ama bahari kuwa mchanga kukufanya ukubali EPL ni ligi bora kuliko nyingine, Ukikaidi pengine utakuwa unajichumia dhambi , dhambi nyekundu ambayo pengine unaweza usisamehewe kamwe.

daVinci XV​

 
huuyo baba yako alikua kilaza, alikua anamsifia Gerrard? Yani aliwaacha akina akina Kaka, Riquelme, Totti, Figo, Del Piero, huyo pumbav kabisa
 
Tuvumilie Kidogo ndugu yangu...... Pale Kwa Mkapa tunayo Shughuli Ya Kitaifa....Tukimaliza tu Tunakuja Kwenye Uzi huu.
 
huuyo baba yako alikua kilaza, alikua anamsifia Gerrard? Yani aliwaacha akina akina Kaka, Riquelme, Totti, Figo, Del Piero, huyo pumbav kabisa
kilaza ni wew ambaye hujaliona neno na wengine baada ya hayo majina
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom