EPL: Arsenal yashinda 6-0 dhidi ya West Ham

Mchochezi

JF-Expert Member
Feb 29, 2012
10,416
6,578
Klabu ya Arsenal imeibugiza West Ham kwa mabao 6-0 katika mchezo wa ligi kuu england maarufu kama EPL.

Mpaka mapumziko Arsenal ilikuwa mbele kwa mabao manne kwa nunge, huku mabao hayo yakifungwa na Saliba dakika 32, Saka dakika ya41 kwq penati, Gabriel 43 na Trossard dakika 45+2.

Kipindi cha pili Arsenal aliongeza kupitia Saka dakika 63 huku Rice akiwafunga waajiri wake wa zamani dakika ya 65.

Kwa matokeo hayo Arsenal amefikisha alama 52 baada ya michezo 24 huku wakiwa nafasi ya 3 ya msimamo wa ligi hiyo.

Vipi unawapa Arsenal nafasi ya kutwaa ubingwa?
 
Hamna kitu kama hicho labda mechi zote zilizosalia ashinde kwa kiwango hicho kitu ambacho ni ngumu
 
Back
Top Bottom