proxy
JF-Expert Member
- Jul 3, 2016
- 1,479
- 1,348
Ni saa sita za usiku sasa bado Jaji Hyera yuko sebuleni akiendelea kupitia kitabu chake cha sharia. Katika meza ndogo kulikuwa na vitabu vingine zaidi ya saba vya sheria.Aliendelea
kufungua ukurasa baada ya ukurasa.Alionekana
kuwa na mawazo mengi mno.Wakati akiendelea
kupitia kurasa za kitabu kile mke wake akaingia
pale sebuleni akiwa na kikombe cha kahawa,
akakiweka mezani halafu akainama na kumbusu
mumewe.
“ You need to take a rest now.Tommorow is your
big day” akasema Flaviana mwanamke mwenye
uzuri wa kipekee. Hyera akakifunika kitabu chake
na kumtazama mkewe ,akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo na kusema
“ Natamani sana nipumzike lakini sina hakika
kama nitapata usingizi.”
Mke wake akamuangalia kwa makini halafu
akasema
“ Kuna jambo nataka nikuulize mume wangu”
“ Uliza usihofu ”
“ Najua kesi hii ni moja kati ya kesi kubwa na
ngumu kwako.Hukumu unayotarajia kuitoa kesho
inasubiriwa kwa hamu kubwa sana na umma wa
watanzania.Wewe ni jaji na nina imani maamuzi
yako utakayoyachukua ni sahihi kabisa,lakini swali
langu ni je Yule msichana ana hatia?
Swali lile lilionekana gumu sana kwa Jaji Hyera Akainama akafikiri kidogo halafu
akachukua kikombe cha kahawa akanywa kidogo
na kumtazama mkewe.
“ My love kesi hii ni ngumu sana na imejaa utata
mwingi na ndiyo maana unaniona mpaka hivi sasa
bado niko hapa.” Akasema Hyera
Flaviana akamtazama mume wake na akagundua
kwamba hakuwa tayari kumjibu swali
alilouliza.Akasimama na kusema
“ Sina wasi wasi na maamuzi utakayoyatoa kesho
lakini nakuomba utoe haki kwa upande wenye
haki.”
Hyera hakumjibu kitu akabaki akimuangalia
“ Come to bed when you are done,but don’t stay
till very late.You have a big day tomorrow.”
Akasema Flaviana na kuelekea chumbani .Elibariki
akavuta pumzi ndefu na kuchukua kitabu chake
cha sheria akaendelea kukisoma.
“ Katika maisha yangu ndani ya sheria sijawahi
kukutana na kesi ngumu yenye mitihani kama
hii.Hata hivyo niliapa kusimamia sheria na
kutenda haki kwa kila mwenye haki.Katika
maamuzi yangu ya kesho lazima nifanye kwa haki
japokuwa nina hakika nitakuwa katika matatizo
makubwa baada ya hukumu ya kesho lakini siwezi
kupindisha sheria eti tu kwa sababu ya shinikizo
toka kwa mtu au kikundi cha watu.Mungu
ataniongoza na kunisimamia ili nitoe hukumu ya
haki” akawaza Hyera na kufunga vitabu vyake
akaelekea chumbani kulala, tayari Flaviana mke
wake amekwisha lala.Akamtazama kwa makini na
kujisemea moyoni
“ Nina hakika hata wewe hautanitazama vizuri
baada ya hukumu ya kesho,lakini sina namna
nyingine zaidi ya kutenda haki.Utanisamehe mke
wangu” akawaza Hyera na kupanda kitandani
kulala.
****************************
“ Hyera my love,amka kumekucha !! ..Ilikuwa ni sauti tamu na laini ya Flaviana akimuamsha
mumewe.Jaji Hyera ambaye asubuhi hii
alionekana kuzama katika usingizi mzito
akafumbua macho huku akiguna na kutazama saa
ya ukutani.Ni saa kumi na mbili na dakika ishirini
za asubuhi.
“ jana sikupata usingizi kabisa.Usiku wangu
ulikuwa mrefu sana” akasema kwa sauti ya
uchovu.
“ Please wake up honey.Today its going to be a very long day” akasema Flaviana. Hyera akainuka na kuelekea katika chumba chake cha mazoezi akafanya mazoezi kidogo halafu akaelekea bafuni. Bado kichwa chake kiliendelea kuwa na mawazo mengi sana. Alivyooga akarejea chumbani na kukutana na suti nzuri aliyoandaliwa
na mke wake akavaa na kujitazama katika kioo
kikubwa kilichokuwamo chumbani mwao.Aliganda
pale katika kioo hadi mke wake alipoingia naye
akaanza kujiandaa.
“ Leo unakwenda kazini? Akauliza Jaji Hyera. Flaviana akacheka kidogo na kusema
“ Usinichekeshe mume wangu,yaani niende kazini
leo? Siwezi kufanya hivyo hata kidogo.Leo ni siku
yako kubwa.Ni siku yetu kubwa.Ni siku ambayo
jina lako litaingia katika vitabu vya historia kwa
hukumu unayokwenda kuitoa.Vyombo vyote vya
habari vitakuwepo mahakamani ,lazima na mimi niwepo nikuunge mkono pamoja na mdogo wangu Oliver.” Akasema Flaviana. Hyera hakujibu kitu
akaendelea kujitazama katika kioo.
“Are you nervous my love? Akauliza Flaviana
“ No I’m not” akajibu Hyera halafu wakaongozana kuelekea katika chumba cha
chakula kwa ajili yakupata kifungua kinywa.Wakati
wakiendelea na kupata kifungua kinywa simu ya
Jaji Hyera ikaita.Akaitazama ikiita akasita kuipokea.
“ Mbona hupokei hiyo simu? Akauliza Flaviana
“ Its your father.Mr President” akajibu Elibariki
“ Usiogope.Ongea naye .Si kawaida yake kupiga
simu mida kama hii, inawezekana ana jambo la
maana la kukwambia” Akasema Flaviana. Hyera
akaichukua simu na kubonyeza kitufe cha
kupokelea huku akiinuka na kuelekea sebuleni.
“ Hallo Mr President” akasema Jaji Hyera
“ Hallo Jaji.Mnaendeleaje vijana wangu?
“ Tunaendelea vizuri mzee.Ninyi mnaendeleaje?
“ Tunaendelea vizuri sana”
“ Nashukuru kusikia hivyo” akasema Hyera na
kimya kifupi kikapita
“ Hyera,today its your big day” akasema
Mheshimiwa rais.
“ Najua unakwenda kutoa hukumu katika kesi
ngumu inayovuta hisia za watu wengi na hasa
kwa kuwa binti wa rais naye kesi hii inamuhusu
kwani mchumba wake ndiye aliyeuawa.Sikufundishi kuifanya kazi yako lakini fanya maamuzi ya
haki kwa namna uonavyo wewe.Pamoja na hayo
kuna jambo ambalo nataka kukuomba kijana
wangu” Akasema Profesa Daka Masumbuko rais wa jamhuri ya Muungano wa
Tanzania.
“ Nakusikiliza mzee” akasema Jaji hyera kwa
wasi wasi .
“ Nilikuteua kuwa jaji kwa sababu wewe ni msomi
mzuri na unazifahamu sheria za nchi kwa hiyo
sitaki kuingilia maamuzi yako lakini nakuomba
kijana wangu japokuwa nimechelewa kukuomba
lakini try in anyway you can to make my daughter
Happy.Ni hilo tu ninalotaka kukuomba kijana
wangu.Nakutakia siku njema” akasema
mheshimiwa rais na kukata simu.Jaji Hyera alibaki ameduwaa asijue afanye nini. Maneno yale
ya rais ambaye ni baba mkwe wake yalimfanya
ahisi kuchanganyikiwa.
“ Huu ni mtihani mgumu sana lakini Mungu
atanitangulia nitatenda haki” akawaza Hyera na
kurejea mezani
“ Amekwambia nini baba? Mbona sura yako
imebadilika namna hiyo? Akauliza Flaviana
“ Nothing.Just greetings” akajibu Hyera na
kuendelea kupata kifungua kinywa.Baada ya
kumaliza akarejea chumbani na kujitazama tena
katika kioo na kuvuta pumzi ndefu.
“ Please help me Lord.I’m in a very difficult situation” akasema Hyera kwa sauti ndogo na
mara mke wake akaingia mle chumbani
“ Its time my love.Are you ready?
“ Let’s go” akasema Hyera,wakatoka wakaingia
garini na kuondoka.
**************************
Hakukuwa na nafasi tena ya kukaa ndani ya
chumba cha mahakama kutokana na watu
kujaa.Ni siku ya hukumu ya kesi ya mauaji
inayomkabili mmiliki wa maduka makubwa ya
mavazi ya Ritha Fashion, Ritha Wambinga. Kesi hii
iliyovuta hisia za watu wengi na kuwafanya
wafurike ili kuja kusikia hukumu ilikuwa
inaonyeshwa moja kwa moja katika runinga. ILikuwa ni kesi ya kwanza kubwa
kurushwa moja kwa moja katika runinga nchini, Katika kila kona ya nchi watu walikuwa wakifuatilia matangazo ya moja kwa moja ya kesi
hii ambayo hukumu yake ilikuwa inasubiriwa na
watu wengi.
Ndani ya chumba cha mahakama ilikuwepo familia
ya rais ikiongozwa na mke wa rais, Dr Flora
Daka ambaye alikuwa ameambatana na binti
zake wawili Flaviana na Oliver.
Familia ya Edson
Kobe kijana anayedaiwa kuuliwa na Ritha nayo
ilikuwepo mahakamani hapo ili kuhakikisha
kwamba haki inatendeka.Familia ya Edson na ile ya rais zilikuwa ni familia rafiki kwa muda mrefu sana.Kwa upande wa Ritha hakukuwa na ndugu
yake yeyote aliyefika mahakamani pale zaidi ya
rafiki zake wachache.
Tayari mtuhumiwa amekwisha ingizwa
mahakamani na aliyekuwa akisubiriwa ni jaji
anayeisikiliza kesi ile aweze kuingia na kuisoma
hukumu.Wakati wakimsubiri Jaji aingie, John Wabukoba mwanasheria anayemtetea Ritha alikuwa
akibadilishana mawili matatu na mteja wake .
“ John,kabla hukumu haijaanza ninaomba
nikwambie kitu.” Ritha akanyamaza kidogo na
kuendelea.
“ Nakushukuru sana kwa kila kitu ulichonifanyia.
Umenisimamia katika kesi hii kwa kila namna
ulivyoweza.Najua chochote kinaweza kikatokea
siku ya leo hivyo nakuomba endapo ikitokea
nikakutwa na hatia na kufungwa kifungo cha
maisha au kifo uhakikishe yale yote
niliyokuandikia katika karatasi unayatimiza.Wewe
ni zaidi ya rafiki.Wewe ni ndugu yangu pekee
ninayekutambua. Ninakukabidhi kila kilicho changu endapo mambo yataenda kinyume na matarajio yetu." Akasema Ritha huku machozi yakimtoka
“ Ritha naomba usikate tamaa hata kidogo. Nimepambana vya kutosha kuhakikisha
kwamba tunashinda kesi hii lakini kama mambo
yataenda tofauti na matarajio yetu hautakuwa ni
mwisho.Nitafungua ukurasa mpya wa mapambano
na nitapambana hadi nihakikishe haki
imepatikana.” Akasema John na mara Jaji Hyera
akaingia.Wakati Jaji akiingia Ritha akamnong’oneza John sikioni
“ I didn’t do it.I didn’t kill him”
“ I know Ritha and I believe you” akasema John
na mara mahakama ikaanza.”
JAJI TAYARI AMEINGIA NA MAHAKAMA IMEANZA
,JAJI HYERA ATAAMUA KITU GANI? RITHA NI
NANI NA AMEFIKAJE HAPA ALIPOFIKA... Tuonane katika toleo lijalo
NB: Majina ni ya kutunga tusitafsiriane
Itaendelea kesho....