Baada ya Chaguzi za Baraza la Wazee ndani ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ngazi ya Taifa hapo jana, utafuata Uchaguzi wa Baraza la Vijana (BAVICHA) na kisha Baraza la Wanawake (BAWACHA) na kuhitimishwa na Uchaguzi wa Mwenyekiti Taifa mwezi huu wa Septemba.

Ephata Nayaro (pichani juu) ni mmoja wa wagombea wa Nafasi ya kuwa Mwenyekiti wa BAVICHA Taifa. Ana nia na Dhamira ya Kushinda Nafasi hiyo ili kulifanya Baraza la Vijana kuwa la manufaa zaidi. Anasababu nami nazikubali.. Anauwezo na amethibitisha hilo kwa vitendo.
Akiwa Mwenyekiti wa Chadema Wilaya ya Arusha Mjini na Mwenyekiti wa Bavicha Mkoa wa Arusha ameweza kuongoza chama kuimarika na kuwa eneo la kuogopwa na CCM. Bila kusahau kuwa ni Uongozi wa Nanyaro Jijini Arusha ndio ulifanikiwa kutetea Kata nne zote za waliokuwa madiwani wakafukuzwa uanachama na pia kuchukua Kata mbili zikizokuwa za CCM! Kwa ufupi ni mafanikio makubwa sana chini ya Uongozi wake. Namkubali. anafaa, anaweza na anastahili kuongoza BAVICHA mpya kwa mafanikio zaidi!
Nikushirikishe hapa mengine usiyoyajua kuhusu Ephata Nanyaro.
********************

SIFA BINAFSI
-Ephata Nanyaro amezaliwa tarehe 27.11.1984
-Ana mke mmoja na watoto wawili.
-Elimu yake ni ya Shahada ya kwanza.
-Ni mcha Mungu
- Ana Certificate ya Campaign for Change
UZOEFU WA KIUONGOZI NDANI YA CHAMA
-Mwenyekiti wa BAVICHA Mkoa wa Arusha (2009-2014)
-Mwenyekiti wa CHADEMA Wilaya ya Arusha Mjini(2011-2014)
-Diwani wa Kata ya Levolosi Arusha Mjini (2010 hadi sasa kuelekea 2015)
-Mbunifu wa Siasa ya Uchumi kwa Viajana wa Chadema Jijini Arusha kwa kuasisi VIPATU (Vijana Kwa Pamoja Tunaweza)
- Taasisi ya vijana ambayo imeinua vijana wengi kiuchumi mkoa wa Arusha.
KWA NINI ANAFAA KUWA MWENYEKITI BAVICHA TAIFA

1.Uwezo wa Kiuongozi
Amekiongoza Chama Wilaya ya Arusha Mjini kwa mafanikio makubwa sana. Katika kipindi cha uongozi wake Chadema ilifanikiwa kushinda chaguzi zote ndogo, na kuongeza Kata za Sombetini na Daraja mbili ambazo awali zilikuwa zinaongozwa na CCM, pia kuzitetea Kata nne za Kimandolu, Kalolei, Themi, na Elerai ambazo madiwani wake walifukuzwa kwa kukosa ndiahmu kwenye chma.
Aimewatumikia wanawanchi wake wa Kata ya Levolosi kwa uaminifu na uwezo mkubwa,ambapo ameweza kutekeleza ahadi kwa wastani wa 80% hadi sasa.
2.Ubunifu
Amebuni miradi mbalimbali ya BAVICHA Mkoa wa Arusha, yenye malengo ya
(a)Kuboresha na kuinua maisha ya vijana kiuchumi
(b)Kukifanya chama kuwa relevant kwa wananchi wengi. Chini ya mpango huu alianzisha VIPATU(Vijana Pamoja Tunaweza)
3.Oganizesheni imara ya BAVICHA
Kwa kuwa malengo makuu ya chama ni kuchukua DOLA,na BAVICHA ina jukumu kubwa la Kuhakikisha malengo makuu ya chama yanafikiwa.
Hivyo tunahitaji kujenga oganaizesheni imara ya BAVICHA kutoka chini hadi juu.BAVICHA itakayokuwa mhimili mkuu wa CHAMA katika kufikia malengo,hili tutalijenga katika misingi ya Uadilifu,Uwajibikaji,Uwazi,Utu na Ujasi ri mkubwa sana
Kwa heshima sana anaomba KURA kwa vijana wenzake, wajumbe wote wa Mkutano Mkuu wa BAVICHA, na wasio wajumbe annawaomba sana mumuunge mkono katika kuwatumikia vijana.
Hakika ukimchagua Nanyaro hutoijutia kura yako.
View attachment 183457
CHAGUA NANYARO BAVICHA 2014-2019
Malengo na dira yake katika kuliongoza baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA) yanampambanua yeye kama mgombea pakee mwenye mikakati thabiti ambayo ikimpata msimamizi, BAVICHA itaonekana katika sura mpya hasa wakati huu ambao CHADEMA ni chama kinachosubiri kuongoza DOLA.
Dhamira ya Nanyaro ni kuhakikisha mipango kazi yote inayoandaliwa na baraza la vijana Taifa inaanzia kwanza kwenye ngazi ya MATAWI na MISINGI kwakuwa huko ndiko wanachama waliko.
-Kuhakikisha vijana wanajitegemea kiuchumi, kwa kuanzisha fursa za uchumi kama kuwekeza katika kilimo, viwanda vidogo na ufundi, na kupunguza vijana kutumiwa na wazee kwa malengo yao ya kisiasa.
-Kuhakikisha Bavicha inakuwa taaisis inajiyotegemea kiuchumi na kifikra bila kutegemea ufadhili toka chama, hii itawezesha baraza kujitegemea kimajukumu na kufanikisha malengo yake yote na kufanya kazi zake kwa uhuru.
-Ni BAVICHA ya vijana walio jitambua, BAVICHA inayo fanya kazi kwakusimamia Misingi, Falsafa na Itiadi ya CHADEMA.
-Demokrasi, Uadilifu, Uwajibikaji, Uwazi, Uzalendo na Ujasiri uliotukuka kwa maslahi mapana ya chama na Taifa letu ni TUNU zinazo muongoza Ephata Nanyaro mtakapompa ridhaa ya kuliongoza baraza la vijana wa CHADEMA (BAVICHA)
-Kuhakikisha dira kuu ya BAVICHA inafikiwa yaani vijana kuwa nguvu ya mabadiliko ya kidemokrasia kwa maendeleo yao na ya Taifa kwa ujumla-Kuwezesha sera sahihi, uongozi bora na kujenga oganizesheni dhabiti yavijana kwa maendeleo endelevu
-Mafunzo ya maswala ya kijamii (afya,uchumi,demokrasia,na uongozi)
-Chemichemi ya uongozi
Ni Ephata Nanyaro Mwenyekiti BAVICHA Taifa 2014 – 2019 kwa Baraza la Vijana imara na lenye uthubutu katika kupigania maslahi mapana ya vijana ndani ya Taifa letu kupitia CHADEMA.
*****************

"And there comes a time when one must take a position that is neither safe, nor politic, nor popular but he/she must do it because CONSCIENCE tells him it is RIGHT" - Ephata Nanyaro BAVICHA 2014-2019
View attachment 183459