Sammy Nyoni
Member
- Aug 25, 2010
- 9
- 0
tunawaita "maji yamekatikaa" kisha wanatoa matusi ya hatarKitu kingine nimekumbuka....mnakumbuka zamani kulikuwaga na malori yanapita mitaani yakiuza magunia ya mkaa? Basi wale wauza mkaa walikuwaga wanakaa nyuma kwenye magunia kule...basi hawa jamaa walikuwa kila wakipita mtaani lazima tuwazomee na kuwatania sana. Basi walikuwa hawapendi.....siku moja lori la mkaa likapita mtaani bana...basi mimi kujifanya mjanja si nikaanza kuwatania. Heheheheee siku hiyo wakaamua kunitolea uvivu bana...jamaa mmoja akanishukia akaanza kunikimbiza. Ebana nilitoka mkuku kaa nini unaambiwa huku nikipiga mayowe...baaaaba...baaaaba.....dah...yaaani nikikumbuka nacheka sana. Lakini uzuri hakunipata wala nini...nilimtimulia vumbi tu jamaa
Yeah, I can Imagine! Ukizingatia siku hizo underwear chache, ukibahatika unavaa zile VIP.....kazi kweli kweli!
Napita tu,hizo enzi za chachacha,solo na utanikoma saa sita!
Kumbe wote ni vijana? Nilifikiri tumecheza wote "Embakasi" ya Les Mangelepa?
Hahahaa!Mh, umenikumbusha vijarida vya dr love pimbi, enzi hizo tunavisoma darasani! Kumbe vilikuwa vya ukweli eeh!
Aaah mimi nilikuwa mtu wa ndaba zile za kuchumpa. Mnazikumbuka Avia, Hi-Tech, LA Gear? Ila kuna ndaba zilikuwa zinaitwa Troop....hizi zilikuwa bab kubwa enzi hizo. Mimi nilikuwa nazo pair mbili...nilitesa nazo sana aisee. Nakumbuka nilipata mademu kwa kutumia hizi ndaba. Halafu wakati wa likizo nilikuwaga lazima ninyoe panki...si unajua shuleni mapanki yalikuwa yanakatazwa....basi mimi nilikuwaga nasubiri mwezi wa sita na wa kumi na mbili....
Cheki Troop hiyo...