Nilikuwa naishi mitaa ya kingalu morogoro karibu kabisa na hosteli za morogoro sec girls,basi mida ya jioni jioni,mabinti wa morogoro sec ilikuwa ndo tabia yao kuoga nje.Mkipita nje ya fensi hata kama hamjawaona,watapiga kelele mpaka mjue kwamba wapo nje na wanaoga nje.Me nakumbuka tulipokuwa form 3,shule yetu ya gals tupu,bweni letu la form 3 lilikuwa mbali kidogo na mengine afu limejitenga flani na mabweni mengine,tulikuwa tunapenda sana kuoga nje(kuna kisehemu kilikuwa kama kibaraza),basi kuna mwalimu mmoja alikuwa hapendi sana hiyo tabia akatuchimba mkwara NIKIWAKUTA MNAOGA TENA HAPO NJE NTAWAFUNGA NYUCHI ZENU NA MINYONYORO NA KUWAVUTA HIVYO HIVYO HADI ASSEMBLY.
Mkwawa high school kwa sisi tuliosoma o level seminari tulipata shida sana nyakati za mwanzo kusoma na mabinti hasa nyakati za prepo. Kombolela hasa siku za jumatatu katika mabweni ya wavulana...
pale KIBITI SEC SCHOOL Kulikuwa na ticha wa kike ambaye ilipokuwa zamu yake hupita kila dom kuwaamusha madent, basi bwana ipo cku tukakubaliana kwamba tulalapo hamna kujifunika shuka, hamna kushusha net wala kulala na nguo yoyote ile ikiwemo CHUPI, Alipokuja maadam karudi mbio akipiga makelele na toka ck hyo alikata mguu kuamsha watu
Mi nakumbuka mwaka 1994 tukiwa sengerema secondary a.k.a Singapore, ile tunaingia form 5 kuna mwalimu mmoja tulimkuta anaitwa mwalimu BUGA.kumbe bwana lilikuwa jina la utani...siku moja akanikamata sijaenda parade, basi akawa ananiuliza namjua yeye ni nani? me kwa kujiamini nikamwambia wewe si mwalimu BUGA.. aiseeeeeee nilichezea kichapo cha hatari..kumbe bwana BUGA lilikuwa jina la utani,,kwa vile alikuwa anavaa suruali zile BUGA..yaani ile juu imebana afu chini umemwagika..ahahaha sitasahau kabisa..
Nyie mlikuwa kiboko......ahahahaaah!!Nakumbuka mashindano ya kujamba niko f. 3.tulikuwa tunakulamaharage changanya na sukari na ugali mwingi mkitoka prepo tunakula kiporo tena cha beans ,kwenye saa 4.tunatulia kwenye cube mtu akitoa ushuzi muhimu ni ile sauti na lazima mwingine ajibu.kulikuwa na milio kama ya trekta,ndege ,filimbi ...
Mkwawa Complex and Casino, I just love it...Nilikwenda kufanya 'hijja' pale but was sad coz sasa imekuwa university. The government needs to preserve some sites for historic interests.