Ahahahaaah!!! Mkuu Mazwi ya wapi? Ya Headmaster Yamsebo!!Daa wanajamvi mie nakumbuka tulipo fika 2 form one pale Mazwi secondary, tulikumbana na kwataa kwa wiki sita nakumbuka jamaa walitupigasana mabuti na mitama
Umenichekesha sana!!
Nakumbuka pale Mzumbe SEC ukiumwa Malaria unapewa SOFT DIET(Wali topetope na kabichi). Basi watu tulikuwa tunaumwa kila siku. Tatizo sasa mpaka Daktari wa shule(hata sio daktari), akuandikie(21days SD). Hapo ndugu chereko tu hahaha
Nakumbuka siku moja nikiwa o-level form 1 kibaha sec,si unajua ule utaratibu wa misosi,watu kadhaa mnaunda kikosi,maybe watu 13 mnakuwa na dishi lenu moja la ugali/wali na moja la mboga.Ugumu ulikuwa unatokea ikifika zamu yako,unafuata msosi jikoni,unagawa kwa wenzio na kuosha madishi na kuyarudisha jikoni.siku moja jamaa alipojua ni zamu yake akaamua kutokuja kabisa.Tulikuwa form one 5,form two 4 na form four 2.Form four mmoja akashauri form one(nyoya,salamanda,nyoka) mmoja ajitolee lakini tuligoma wote.Wale form iv walijitolea ku-save msosi,ila walichofanya sitasahau.Waligawana msosi wao wawili wakatosheka,baada ya hapo walimwaga wali wote uliobaki chini na mchuzi wakaugeuza maji ya kunawa,kiufupi tulipigwa dash.Dah!vp wewe ulipokuwa form one,tupe kisanga kilichokukuta!
KIBAHA SEC.kuna mwalimu alikua akiitwa MPALAZA alikua wa kilimo na ufugaji.Tulipokua form 1 alikua akisema ni heri form one kumi kufa kuliko nguruwe mmoja wa shule ee bwana nilikua nachukia balaaa.kwa waliosoma mawenzi sec ilikuwa tunapata luch shule ila wavulana waliokuwa bweni walikuwa wanamind hivyo walikuwa wanaenda kunachukua madishi hata ya madarasa matano wanaenda kuyaficha wanakula badae ila walikuwa wakikamatwa wanaletwa assembly cha kushangaza kila dishi walikuwa wanakula watu wawili .
Halafu kulikuwa na wengine wanaenda jikoni wanachota krimu wa juu kwenye sufuria ya maharage
Kwa kweli thoz dayz a nice 2 remember
Duh, basi mi nakumbuka tukiwa Old Moshi sec...
kwanza ni bifu tulilokkua nalo na Moshi tech...yani kuna siku tulitembea mpaka huko Moshi tech..kuanzisha vita tu!
Ila nakumbuka zaidi nilipoingia form one nikaitwa na majamaa (na walikuwa wakurya.. kutokana na lafudhi zao-afu nikakumbuka stori nlizokua nasikia kuhusu wakurya ati wakija kusoma sekondari ni wababa kabisa na wao vita ni jambo la kawaida kwao)
basi wakaniita nje ya bweni pale Hanang...wakanipa kiatu kinachonuka uvundo..wakasema nipige simu nyumbani nimwambie baba pesa zimeisha...kwa hiyo nikajifanya ninaongea na baba yangu. Basi nikatunga stori nilipokata simu nikawaambia amesema, atanitumia baada ya muda. Hivyo wakajifanya wana huruma sana...wakanipa shilingi mia, wakasema dogo kajinunulie maandazi na soda ila kabla hujanunua uje na maziwa na mkate mkubwa...duh! nilitoka jasho....
ilibidi niingie bwenini nichukue pesa zangu nikawanunulie...!!!!
tangu siku hiyo...mimi na njia ya hanang siendi...
sanasana nilikua natembea na wale majamaa vipofu, ukiwa nao hawakusumbui...hicho ndo kilichonisave....GUD OL' DAYZ....Auld Lang Syne...
Na wale masai waliosema sisi haiwesi kula ugali bila nyama na masiwa!Nakumbuka kibaha mwaka huo tupo kidato cha kwanza, intake kubwa ilitoka usukumani, na kibaha ilikua punga(wali) daily, siku moja msukuma mmoja alibidi aende kulalamika kwa mkuu, 'Wajameni sisi tunataka mabondo(ugali) mawali atushibagi' ikaongelewa hiyo baraza, jamaa alipata kibano toka form 2 mbaya.
Ahahahahaaaah!! Mkuu kumbe unakipata eeeh!!Mazwi=maneno,au vp mkuu katavi.
Lazima ukipate kumbe jirani!Si unajua mi mtu wa border(TUNDUMA)!
Ahahaha hapo kwenye blue nona lazima mtoke mkuku, Mama wengine wamechanganyikiwaKwanjeka noma,kuna mother mmoja tulimkamata mwanae kwa wizi wa viatu,alipotonywa kuhusu mwanae kukamatwa na wanafunzi,alikuja mkuku na kuanza kuvua nguo moja baada ya nyingine,wote tulitoka nduki tukamwacha yeye na mwanae.
we mama mbavu za...nguu--Nakumbuka mashindano ya kujamba niko f. 3.tulikuwa tunakulamaharage changanya na sukari na ugali mwingi mkitoka prepo tunakula kiporo tena cha beans ,kwenye saa 4.tunatulia kwenye cube mtu akitoa ushuzi muhimu ni ile sauti na lazima mwingine ajibu.kulikuwa na milio kama ya trekta,ndege ,filimbi ...