Enyi wanaume msiwe na tabia kama za mume wangu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Enyi wanaume msiwe na tabia kama za mume wangu

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by SUNGURA MPOLE, Dec 24, 2011.

 1. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #1
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nimeolewa na nina mtoto 1 wa 5yrs, mwanzo wa ndoa yetu tulikuwa na maisha ya chini ndugu wa mume waliniheshimu nami niliwaheshimu, MUNGU akatujalia rizki tukajenga na tukafungua biashara, mawifi (Wamachame)wote wameolewa na wanamaisha mazuri wakaanza tabia ya kuja kwangu ghafla kwa wakati tofauti bila taarifa na wananiambia naomba laki 5,6 nitarudisha, inabidi nijipigepige niwape nikatoa km mara 3 hawarudishi.

  Mwisho akaja mmoja kutaka nimpe kaki 8 atarudisha nikamuuliza mbona hajarejesha ile hela nyingine aliyonikopa? hapo ndo wakaanza kunipiga vita na kumwambia mdogo wao "mume wangu" kuwa mimi simfai eti kwanini nawanyima hela.

  Wakati ni za ndugu yao, na mume wangu akaanza kunichukia, nikimwelewesha haelewi amenimbia hataishi na mimi kama mke wake na hatajishughulisha na mtoto aliye tumboni mwangu kwa sababu sitaki kuwafanyia dada zako chochote wanachotaka.

  HUU NI MWEZI WA 2 UNAISHA HAJAWAH KUNIULIZA CHCHT JUU YA MAENDELEO YANGU WL MWANAE TUMBONI ila mara 3 sasa anaamka usiku analia na kumuomba MUNGU AMSAMEHE, NIFANYAJE MIMI?
   
 2. Bishanga

  Bishanga JF-Expert Member

  #2
  Dec 24, 2011
  Joined: Jun 29, 2008
  Messages: 15,347
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 0
  anaamka usiku na kulia na kumwomba Mungu amsamehe kwa kosa lipi sasa,la kukuoa wewe au la kukuchukia wewe? Anajutia nini,embu vavadua hapo kwanza.
   
 3. Eiyer

  Eiyer JF-Expert Member

  #3
  Dec 24, 2011
  Joined: Apr 17, 2011
  Messages: 28,238
  Likes Received: 3,675
  Trophy Points: 280
  Huwa napata hasira sana ninaposikia wanaume mabwege kama hawa(samahani kwa kutumia lugha kali,nina hasira mno)hawa wanatuaibisha WANAUME ambao tumepewa mamlaka ya kusimamia nyumba na kuiongoza,dada,pole ishi nae kwa uangalif sana,kama kero za namna hii zitazidi itabidi ujiulize kama unaihitaji hiyo ndoa,hebu soma threadi yenye kichwa kilichoandikwa;WANAWAKE NA KABURI LA MAPEMA(sijui kama nimekipatia,lakini kitakua kinafanana hivyo)
   
 4. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #4
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  kuna ndumba nini hapo? Maana siku hizi hata hao watu nao wako mbele kwenda kwa mzee Pinda kununua Wanga!!!
  Kwani wewe ni kabila gani?
   
 5. Judgement

  Judgement JF-Expert Member

  #5
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 13, 2011
  Messages: 10,361
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 145
  Hiyo familia inahitaji sana kikao cha ushauri nasaha kuliko maombi ! Na agenda ya kikao iwe JITAMBUE (wajitambue)
   
 6. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #6
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  SIJATHUBUTU KUMUULIZA ila wiki iliyopita nilikua kazini ghafla nikaanza kuishiwa nguvu nikamuomba anisaidie anipeleke hosp. Akakataa nikamwomba shemeji yng akaja akanipeleka kumbe presha na skari vilikua vimeshuka ikabidi nilazwe hajaja kuniangalia wl kunipigia simu hadi nilipotoka hosp. KWA UCHUNGU NILIOKUA NAO NILIPOMWONA MACHOZI YALIANZA KUTEREMKA KM MAJI SIKUWEZA KUMSEMESHA HATA NENO 1 ZAID YA SALAM.
   
 7. Kongosho

  Kongosho JF-Expert Member

  #7
  Dec 24, 2011
  Joined: Mar 21, 2011
  Messages: 36,126
  Likes Received: 303
  Trophy Points: 160
  hivi hujawahi kuja na mada hapa tena ya kuhusu mmeo?
  Nadhani hii ni mara ya pili?

  Afu ntakujibu kitu
   
 8. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #8
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hapana!
   
 9. ndyoko

  ndyoko JF-Expert Member

  #9
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 4,974
  Likes Received: 279
  Trophy Points: 180
  dada we kabila gani? ukijibu swali hili ntajaribu kukupa ushauri unaoweza kukusaidia!
   
 10. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #10
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Hata mimi nimemuuliza swali hilo hali hajatoa jibu!!
   
 11. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #11
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mwanzo niliumia sn nilitaka kuondoka lkn nikamwangalia mwanangu nikaangalia na haliyng nikajua nitakapojaribu kuondoka nitapoteza haki zt za wanangu ambapo nilipata shida sn kuzitafuta
   
 12. o

  omholo Member

  #12
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mimi nijuavyo mume atamwacha baba yake na mama yake na kuambatana na mkewe nao watakuwa mwili mmoja si wawili tena,siyo suala la sakaramenti ya ndoa tu bali kuwa wamoja katika maamuzi ya maisha yenu yote,labda kama mliazima pesa kwa ndugu wa mme zikawasaidia kuinuka kimaisha ndo wanatumia mwanya huo.Haingii akilini wewe upiganie dada zake walipe madeni yeye anakasirika,niwajuavyo wachaga kwa pesa mmmmmmmh hawezi achia pesa kirahisi may be kuna jambo zaidi tujuze.pia punguza mawazo magonjwa uliyoyataja ni hatari kama utaendele na hali hiyo,vyinginevyo kaonane na psycologist kwa ushauri au daktari kwa ustawi wa afya yako.
   
 13. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #13
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  MIMI NI MPARE, ila nilizaliwa na kulelewa mjini huku kwa wachaga na kwa bahati mbaya makuzi mengi nililelewa na mama baada ya baba kufariki, nimesoma hadi form 6.
   
 14. Dena Amsi

  Dena Amsi R I P

  #14
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 17, 2010
  Messages: 13,137
  Likes Received: 255
  Trophy Points: 160
  Acha ujinga wewe wanawake wanaweza siku hz namna gani bana alah hao mawifi zako wanakupa uhai? Wanaweza kulala na kaka yao bila nguo? Wewe una nafasi yakumshawishi kitandani mkiwa hamna nguo jaribu halafu unambie kama hajaingia line hujui trick zahawa viumbe?
   
 15. Sumba-Wanga

  Sumba-Wanga JF-Expert Member

  #15
  Dec 24, 2011
  Joined: Feb 2, 2011
  Messages: 5,387
  Likes Received: 15
  Trophy Points: 135
  Sasa dada kuna mambo mawili unaweza kufanya. Inawezekana hujalogwa, ila stress za ndoa ndio zinazokusumbua hadi ukalazwa. I have been there myself, najua hali illivyo. Hali aliyofikia mume wako, unaweza hata ukafa, na yeye akaoa mwanamke mwingine; Katika hali hiyo kuna mambo mawili unaweza kufanya:

  1) Kubali kuwa hiyo ndio ndoa yako na kama unavyosema mwenyewe, ulishindwa kuondoka. Wewe ni mpare na kwenu umeshafanyiwa send off. Hapo ndio kwako na umefika. Cheza mpira jinsi unavyochezwa uwanjani. Usibishane na mume wako au wifi zako, wewe kuwa kawaida, kama wanataka pesa na wewe unazo, basi wape kama kaka yao anaona ni sawa. Na wakati huo huo na wewe uwe na akili yako, invest kwenye kujenga nyumba au kitu kingine kwa mama yako, ili hata siku mamabo yakiwa mabaya, uwe na pa kusimamia. Kwa manenp mengine; Play it cool

  2) Unendelee na msimamo wako huo ambao huna hakika mwisho wake utakuwaje? either wewe ufe kwa stress umwachwe mwanao kama unavyoogopa, au labda hata mumeo afe. Uzuri wachaga hawatakufukuza kwenye kiamba cha mume wako kwa kuwa tayari umewazalia. This is one of the very positive side of the Chagga


  Kubwa zaidi, muombe na kumtanguliza mungu kwenye kila unalofanya.

  Kila la kheri.
   
 16. S

  SUNGURA MPOLE Member

  #16
  Dec 24, 2011
  Joined: Dec 5, 2011
  Messages: 19
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  HATUJAWAH KUWAJOPA KWANI WKT TUNAOANA MIMI NA YEYE TULIKUA WAAJIRIWA NA TULIPANGA JINS YA KUTUMIA HELA NA AKIBA TULIIDUDULIZA MPAKA TUKAWEZA KUFUNGUA BIASHARA NA KUJENGA, ninavyoelewa jambo jingine lililowaudhi mawifi ni WALIKUA WANANILAZIMISHA NIACHE KAZI NA NIMUACHE MUME WANGU MJINI NIKAKAKAE MACHAME NA MAMA MKWE jambo ambalo nililikataa pia
   
 17. Baba Erick

  Baba Erick JF-Expert Member

  #17
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wee ropoka ropoka tuu! Alafu nahisi haujaolewa! Ameandika machache sana yaani hatujui ni mangapi ameficha na ni madhaifu gani wanayo. NAKUSHAURI DADA WAITE WAZAZI WAKO NA WAKE KAENI MUELEZEE MADHAIFU YENU NA MPATE SULUHU NA SIYO HAPA HATUWEZI KU-RESOLVE PROBLEM BY USING SINGLE CANDIDATE.
   
 18. Baba Erick

  Baba Erick JF-Expert Member

  #18
  Dec 24, 2011
  Joined: Aug 24, 2011
  Messages: 483
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Wee ropoka ropoka tuu! Alafu nahisi haujaoa! Ameandika machache sana yaani hatujui ni mangapi ameficha na ni madhaifu gani wanayo. NAKUSHAURI DADA WAITE WAZAZI WAKO NA WAKE KAENI MUELEZEE MADHAIFU YENU NA MPATE SULUHU NA SIYO HAPA HATUWEZI KU-RESOLVE PROBLEM BY USING SINGLE SIDE.
   
 19. MwanajamiiOne

  MwanajamiiOne Platinum Member

  #19
  Dec 24, 2011
  Joined: Jul 24, 2008
  Messages: 10,478
  Likes Received: 82
  Trophy Points: 145
  Mh! Pole dada! Mwanaume mwenye uwezo wa kumjibu mkewe mwenye kiumbe chake tumboni maneno kama hayo mie huwa ninamwazia mengi sana. Hivi hajui depression na maudhi ya mara kwa mara yanawezamdhuru mtoto?!

  Hii thread ningeomba wanaume wamsaidie mwanaume mwenzao kama ni kweli yametokea
   
 20. o

  omholo Member

  #20
  Dec 24, 2011
  Joined: Nov 24, 2011
  Messages: 24
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  sawa dada naona unachofanya kusimamia mali zenu ni sawa kama mlichimba wenyewe endelea kumuomba Mungu atakusaidia ipo siku mmeo atakuelewa tu,lakini usijaribu kuacha kazi eti kwenda kukaa na mama mkwe,usionyeshe chuki kwa mmeo mtimizie yote ulokuwa unamfanyia hapo kabla hajakengeuka,ila mawifi acha noma iwe noma kwao,kwani mkiishiwa hawataonekana hata mmoja.
   
Loading...