Engineer aliyejenga uwanja wa ndege Mwanza

Engineer aliyejenga uwanja wa ndege Mwanza

Hivi navyopost kuna mvua ya maana inaendelea kupiga tangu kama d,k 15 zilizopita.Ngoja tuone nayo kama itawa"Pinda" abiria wa asubuhi hii.Mlioko Airport kuja mwz endeleeni kupata srengeti za asubuhi,halikadhalika mnaoelekea aiport ya JKNIA kwa safari ya mwz jiandaeni kuahirishiwa safari.maana mvua ya mwanza mwaijua.
 
Kweli Tanzania zaidi ya uijuavyo,kiongozi akivurunda ofisi hii anapewa nyengine mara nyingi yenye maslahi makubwa kuliko awali.
 
Samahani kwanza hiyo Kampuni ya chambo ilipewa tenda wakati yupo kwenye hiyo wizara au kabla hajakuwa Katibu Mkuu?,na kama alipewa hiyo tenda akiwa tayari Katibu Mkuu hamuoni hapo kuna mgongano wa maslahi,
Kusema ukweli uwanja wa ndege mwanza mvua ikinyesha inakuwa balaa ni kama swimming pool,nakumbuka ulikuwa mwezi February au March(wakati mabomu ya G/Mboto yalipolipuka) nilienda Mwanza kwa ndege ,siku hiyo mvua zilikuwa zinanyesha pale Mwanza,tulipotua ndege ilikuwa kwenye dimbwi la maji ikabidi tuvue viatu kwani hiyo sehemu ilijaa maji
 
Mvua bado inaendelea kunyesha ila sio kubwa sana kama asubuhi.Tayari jamaa yangu mmoja kishachelewa ofisi baada ya kutumbukia sehemu barabara ilipokatwa na maji.Bado sijapatataarifa za eneo la "pinda"
 
Tatizo la tenda za nchi mtu anapewa kwa kufaamiana
kwa hiyo mtu anafanya kama atakavyo kwa sababu uliyempa ana % yake
 
Nawashangaa sana watu wa mwanza, 2006 Nikiwa jijini mwanza ndipo ile documentary ya mapanki ilikuwa imezinduliwa sikumbuki uzinduzi ulifanyikia wapi, Ndugu Dr, Ruteni kanari, Engineer kikwete alipokuja na kusema ile documentary ya ndugu saupa (Darwin nightmare)si ya ukweli na masela wa mwanza wakaandamana kumpinga Saupa ingawa ile documentary walikuwa hawajaiona, mimi binafsi sikwenda kwani sikujua nani ni mkweli kati ya Dr, Eng Kikwete na Saupa, Nikiwa chuo jamaa wa CASS by then FASS wakatuletea na tukashuhudia nani mkweli na nani mwongo. Yote yalizungumzwa juu ya uwanja wa ndege wa mwanza including uchafu maofisini.
 
Ndio mjue wabongo sio, wakati mwanza wanaataabika KIA lipo iddle muda mrefu na jamaa wanaporomosha intl. Airport songwe-mbeya wakiamini huko kuna abiria lukuki.
Mnamnyoshea kidule mtu wakati system ndio noma.
 
Hii nchi iuzwe tu kila mtu apewe chake atambae manake naona wanafaidi wachache tu wakati huku uswahilini hata sukari hatuwezi kununua, baba riz tangaza tenda ya kuuza nchi mtugawie chetu hata kama ni buku kila mtu asepe kivyake, tumechoka
 
Back
Top Bottom