Engine ya d-4 ya gari

Engine ya d-4 ya gari

chingunduli

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2012
Posts
268
Reaction score
51
Wana jamvi naomba kujua uzuri na ubaya wa engine ya D-4, nina mpango wa kununua gari aina ya toyota premio ila engine yake ni hiyo d4. Hasnteni sana.
 
Hata mimi hizo gari nazipenda sana lakini nilishauriwa nisinunue hizo gari kwakuwa zina engine za D-4 ambazo wanadai zinasumbua sana,hivi ni kweli so far hakuna mafundi hapa bongo wanaoziweza au ni tatizo la manufacturers ambalo halina tiba?
 
Wana jamvi naomba kujua uzuri na ubaya wa engine ya D-4, nina mpango wa kununua gari aina ya toyota premio ila engine yake ni hiyo d4. Hasnteni sana.

D-4 ni injini za petroli za Toyota zenye kutumia mfumo wa direct injection. Mitsubishi nao wana injini za aina hii ambazo wao huziita GDI (gasoline direct injection). Kwa kifupi injini hizi ni nzuri kwani zina nguvu zaidi na matumizi yake ya mafuta ni mazuri ukilinganisha na injini za aina nyingine zenye ukubwa (capacity) sawa. Tatizo la injini za D-4 ni kwamba zinataka mtumiaji awe makini sana na mafuta anayotumia kwenye gari lake, siyo kuweka petroli ili mradi ameweka petroli. Cha kuzingatia zaidi ni kutumia petroli yenye kiwango cha octane (samahani sijui Kiswahili chake) kinachoshauriwa na mtengenezaji. Petroli yenye kiwango cha octane chini ya kile kinachoshauriwa na mtengenezaji huweza kuleta matatizo ya kujaa kaboni (carbon) kwenye valvu na hii mara nyingi huleta matatizo mengi tu kutokana na umuhimu wa valvu katika injini. Kwa bahati mbaya sana, petroli inayopatikana sehemu nyingi za Tanzania haina ubora (kiwango cha juu cha octane na cha chini cha salfa) unaohitajika kwa injini za D-4.
 
Mkuu Bingwaman naona unazifahamu sana hizi engine za D-4. Namimi nilikua nataka kununua Toyota Brevis 2.5L engine ni D-4 vvti. Naomba kujua wapi naweza kupata hiyo petrol ya uhakika ambayo haijachakachuliwa vilevile incase ikitokea gari ina tatizo kwenye engine wapi kwa kupeleka maana mafundi wetu wengi zinawashinda.

Natanguliza shukrani mkuu.

D-4 ni injini za petroli za Toyota zenye kutumia mfumo wa direct injection. Mitsubishi nao wana injini za aina hii ambazo wao huziita GDI (gasoline direct injection). Kwa kifupi injini hizi ni nzuri kwani zina nguvu zaidi na matumizi yake ya mafuta ni mazuri ukilinganisha na injini za aina nyingine zenye ukubwa (capacity) sawa. Tatizo la injini za D-4 ni kwamba zinataka mtumiaji awe makini sana na mafuta anayotumia kwenye gari lake, siyo kuweka petroli ili mradi ameweka petroli. Cha kuzingatia zaidi ni kutumia petroli yenye kiwango cha octane (samahani sijui Kiswahili chake) kinachoshauriwa na mtengenezaji. Petroli yenye kiwango cha octane chini ya kile kinachoshauriwa na mtengenezaji huweza kuleta matatizo ya kujaa kaboni (carbon) kwenye valvu na hii mara nyingi huleta matatizo mengi tu kutokana na umuhimu wa valvu katika injini. Kwa bahati mbaya sana, petroli inayopatikana sehemu nyingi za Tanzania haina ubora (kiwango cha juu cha octane na cha chini cha salfa) unaohitajika kwa injini za D-4.
 
Last edited by a moderator:
Back
Top Bottom