kinacho nishangaza mkuu hapa ni kwamba kuwa walisema swala la migomo liko mahakama na wao ccm ndo wamelianzsha why?
sasa yeye ana ushahidi gan kusema waliomtesa ulimboka walikuwa wamevaa
magwanda!? Kama sio uvumi
na kama uvumi Mnyika kasema vyombo vya habar vimendika pamoja na wamemrekod Ulimboka mwenyewe kuwa waliomtesa ni police! Why?
Ikabdi wamkalishe kwa ubabe wao!
Stella Manyanya amenistua mno na kauli yake bungeni.
1. Police wameuwa Nyamongo na kutupa maiti barabarani - hakuna hata mtu mmoja amekamatwa.
2. Police wameuwa raia Arusha wakati wa maandamano - hakuna mtu amekamatwa
3. Mauji yametokea Igunga, Arumeru, hakuna yoyote aliyekamatwa
4. Wabunge wa CCM wamevamiwa na kujeruhiwa vibaya - hakuna yoyote aliyekamatwa
5. Doctor Ulimboka amekamatwa, amepigwa usiku mzima, ameng'elewa meno, kucha, kavunjwa taya and left for the dead, mungu kamuepusha na kifo na sasa yuko nje ya nchi kwa matibabu. Lakini siku 5 zimepita sasa hakuna mtu hata mmoja aliyekamatwa na kuhojiwa licha ya Dr Ulimboka kutaja majina!
Sasa, leo Mbunge wa CCM na mkuu wa mkoa ambaye amepata ubunge kwa njia na sababu anazojua yeye mwenyewe anasimama mbele ya bunge na kumuita huyu mhanga wa mateso ya kupindukia Hitler! Wazazi wa Dr Ulimboka na wananchi wa Mbeya wakianza kupaza sauti kweli watakuwa wamekosea?
Inakuwaje serikali iwe na uwezo wa kukamata majambazi yaliyomuua mzungu in just 2 days lakini washindwe kusaka watu waliomfanyia Unyama Dr Ulimboka? Tena huku akiwa ametaja majina?
Wananchi bado tuendelee kuiamini serikali ya chama anachotoka Stella Manyanya kwamba watatupa ulinzi? Nani atakeyamini kuwa sasa polisi hawana 'plaizi' za kung'oa watu meno na kucha? Nani atakayeamini police watu hawana riffle za kutupiga? Usalama wa watanzania uko wapi? Stella Manyanya anaweza kutupa majibu? Na tukayaamini?
Nimefedheheshwa mno na ukatili aliouonesha huyu mama!