TANZIA eng. Felix Mlima Ngoako, Meneja wa Tanroads Ruvuma afariki dunia akishiriki mbio za hisani

Mrao keryo

JF-Expert Member
Aug 29, 2022
1,610
2,168
Meneja wa Tanroad mkoa wa Ruvuma, mhandisi Mlima Ngaile amefariki asubuhi ya leo baada ya kuanguka ghafla wakati akifanya mazoezi ya kukimbia maarufu kama marathon Songea mjini!

Baada ya kuanguka alikimbizwa hospitali ya mkoa wa Ruvuma na kufariki muda mchache baada ya kufikishwa hospitalini!

Taarifa kamili zitawekwa hapa na wahusika. Chanzo mdau aliekuwa kwenye mazoezi pamoja na marehemu!

R.I.P
1705486181509.png
 
Meneja wa TanRoads Mkoa wa Ruvuma mhandisi Ngaile amefariki ghafla baada ya kudondoka ghafla wakati akiwa kwenye mazoezi ya mbio za hisani zilizoandaliwa Mkoani humo.
---


Songea. Meneja wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mkoa wa Ruvuma, Mhandisi Mlima Ngaile amefariki dunia leo asubuhi baada ya kudondoka wakati akishiriki mbio zilizoandaliwa na Wiloles Foundation Marathon.

Mhandisi Ngaile baada ya kudondoka inaelezwa akiishiwa pumzi akiwa eneo la Matalawe Manispaa ya Songea na kupelekwa Hospitali ya Rufaa ya Songea (Homso) kwa matibabu, lakini alifariki dunia.

Mkuu wa Wilaya ya Songea, Wilman Ndile amesema leo Ijumaa Januari 12, 2024 kuwa daktari amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na mwili wa meneja huyo umehifadhiwa hospitalini hapo kusubiri taratibu za mazishi kuendelea kwa kushirikiana na Tanroads makao makuu.

Akisimulia jinsi walivyoshiriki mbio hizo, mkuu huyo wa wilaya (DC), amesema leo asubuhi kulikuwa na mbio za hisani za kuchangia fedha kwa ajili ya kununua vifaa vya kuokoa maisha ya watoto wachanga katika Hospitali ya Rufaa ya Songea.

Amesema meneja huyo alikimbia mbio za kilomita tano na katika kundi lake alikuwepo yeye (DC), Katibu Tawala Mkoa na Mganga Mkuu wa mkoa huo.

“Tulikuwa tunakimbia kwa mwendo wa kawaida, ila tulipofika kilima cha Bombambili tulishangaa akipanda kwa kasi sana na sio kawaida, kwani huwa tunakimbia kila mwisho wa mwezi na tukifika hapo huwa tunatembea.

"Kabda alipata shida kwenye moyo na alipofika Matarawe aliishiwa pumzi na mtu mmoja aliyetambulika kwa jina la Msigwa alipiga simu kuita gari la wagonjwa na walifanikiwa kumkimbuza hospitalini, lakini kwa bahati mbaya alifariki dunia akiwa katika jengo la dharura katika Hospitali ya Homso na mwili wake umehifadhiwa hapo," amesema DC Ndile.

Amesema tayari uongozi wa mkoa umewasiliana na Tanroads Makao Makuu na taratibu zinaendelea na mazishi zinaendelea.

Mkuu huyo wa mkoa ametoa pole kwa ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu wakiwemo watumishi wenzake na amewataka waendele kuwa watulivu na kumuombea marehemu.

Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa Songea, Dk Majura Magafu amesema taarifa zaidi ya tukio hilo atatoa baada ya kuwasiliana na daktari aliyekuwa akimuhudumia, kwani wakati tukio linatokea alikuwa Uwanja wa Majimaji kwenye mbio hizo.

My Take
Prof.Janabi aliwahi Kuonya Watu kushiriki jogging bila kupima Afya kwani ni hatari kwa Afya.
 
Meneja wa TanRoads Mkoa wa Ruvuma mhandisi Ngaile amefariki ghafla baada ya kudondoka ghafla wakati akiwa kwenye mazoezi ya mbio za hisani zilizoandaliwa Mkoani humo.

View: https://www.instagram.com/p/C2AF9ASt_d9/?igsh=eW15d3VmbGJnY3Vq

My Take
Prof.Janabi aliwahi Kuonya Watu kushiriki jogging bila kupima Afya kwani ni hatari kwa Afya.

Nakumbuka aliwahi zungumzia na kuonya kuhusu hizi jogging kabla ya kupima afya japo watu huwa wanambeza ila tahadhari ni muhimu kabla ya hatari japo kifo kikifika hakuna wa kupinga
 
Back
Top Bottom