kalooo 25594
JF-Expert Member
- Jun 14, 2016
- 300
- 194
Ndg wanajamvi,Habari za majukumu,Wapo poleni na wapo hongereni,mimi mwenzenu bado ni mzima wa Afya.
Kama ilivyo kawaida kwa watu wa asili moja,nchi moja bara moja lazima na ni bora tuwe na mtazamo wa dunia moja katika ulimwengu tuishio,Hapa Nina mtazamo wa kalooism kuhusu namna fulani inayoweza kuchangia ama kutoa challenge fulani juu ya baadhi ya mifumo yetu ya kuinua watu ndani ya sauti yetu.Naomba kwanza kukiri kuwa tumetoka mbali licha ya mazingira magumu tuliyowekewa na mataifa ya nje,mfano kwa Taifa letu limeweza kupambana na kufika uchumi wa kati katika kipindi kigumu cha ugonjwa wa Corona.Hivyo hizi ni baadhi ya mitazamo mingine kuweka ujumuishi na mingine sawia katika angle fulani iwezayo kurekebishwa na kukoselewa na hata kufanyiwa kazi baadhi yake katika kuboresha panapo husika.
Pia soma Katika dunia inayobadilika kila kukicha vijana wa kiafrika wanahitaji zaidi uhuru wa ardhi-wanahitaji ukombozi wa nafsi
Yapo madhaifu ya ESS system katika kuwapeleka watu kwenye mbingu saba zilizopangana kwa madaraja/safu.

- Mfumo huu hutegemea taarifa za mtu binafsi na msimamizi kujazia maandishi yanayoweza fanana na alichokisomea mtu japo yanahusishwa maeneo yasiyo na ushahidi, hivo hakuna uhalisia wa kazi na matokeo ndani ya muda kulileta Taifa huru.
- Hakuna ushahidi wa wazi wa ufanisi wa mtu kazini kuwa bora kwa Taifa kwanza(wazuri wa kujieleza ndo wanaonekana wanastahili si matokeo).
- Upendeleo wa msimamizi unaweza kuwa kigezo cha kupendezesha taarifa sababu hakuna taarifa sahihi zilizofanyika sambamba ndani ya muda wa kazi zake mpaka sasa.
- Taarifa za mwaka mzima si kigezo cha mtu kuonekana anastahili au hastahili kupanda.
- Unaweza kuzaa matokeo magumu kwa wengine watakao upima kwanza kuwa hakika ni Agizo tu la sawa na kutumia barabara huku unalifokea japo si kipimo sahihi kwa dunia mpya ya fikra mpya na daraja jipya moja tulitakalo tufike wote,Kama uko mbinguni je utataka tena kwenda mbinguni?Jamani msiba hujibu kila kitu hapo hapo.
Hakuna ubunifu dhahiri labda ule wa kujipendekeza kujaza taarifa hizo kwa hofu ya kufukuzwa kazi au kusimamishiwa mishahara(maadui na dogma watauona ni dogma,ni mfumo usio na ushahidi wa kimazingira hata rejea mbalimbali alafu umeletwa kisa kufukuzwa).
NAMNA BORA YA KESHO YETU.
| No1. | Kipengele | Sasa | Badae nini kifanyike. |
| 1 | Aina ya kipengele | Fomu yenye maelezo binafsi ya mtu mwenyewe unaohalarishwa na kalamu iliyoko ofsini kwa mwaka | Taarifa binafsi ya kila robo ya mwaka inayoenda sambamba na miradi iliyokuwepo kwenye kituo cha mtumishi. |
| 2 | Mtoaji taarifa | Mtumishi mwenyewe tu na msimamizi bila kuzingatia wakati wa kazi katika uhalisia. | Mchanganyiko wa wadau:meneja yeye mwenyewe na wateja wawe sehemu ya kutoa maoni yao kwa kila mradi kama uridhisha. |
| 3 | Uhusiano wa wateja wetu | Fomu jazwa/mfumo haielezi Kazi na matokeo. | Viwepo kazi na matokeo moja kwa moja remodeling kutoka eneo la mradi. |
| 4 | Kipimo cha mafanikio | Maandishi tu ndo ushindi,asiyejaza si mtumishi tena mwaka huo | Matokeo halisi,data za utendaji pamoja na gharama zilizotumika kukamilisha kutoka kwa wasimamizi wake. |
| 5 | ufanisi wa mfumo | Wanaojua kujieleza kwa maandishi,90-100% huyu anafaa na mwingine chini ya hapo kwa msimamizi hatufai | Ufanisi wa kazi,kazi zenyewe zinajielezea. |
| 6. | Uangalizi wa ubunifu | Hauoneshwi na mfumo wa ESS | Ubunifu ndo kipimo kikuu. |
| 7 | Teknolojia ya kutathmimi | Kipimo ni sehemu jazwa tu | Uwepo wa Dashbord,AL based analytic na ufuatiliji wa matokeo |
| 8. | Kipimo cha kubadilika/kujifunza | Hakionekani | Ni bora kizingatiwe. |
| 8 | Ushirikishwaji wa timu | Haupo | klla mtu kwenye timu huchangia tathmini ya mwenzao |
| 9. | Motisha kwa wasiojaza fomu ya ESS | Watu huachwa nyuma/hata kutishiwa kusimamishiwa mishahara bila namna bora na ikawa hivo kwa wasiojaza taarifa | Uwepo uwazi wa mtu kukata rufaa baada ya matokeo aliyoyapata. |
| 10 | Uwiano wa mabadiliko | Cheo kupanda kinachukua muda mwingi mno kwa kipimo hiki.Maana sehemu pembezoni husahaulika. | Kwa Uhalisia wa kazi hauhitaji muda mwingi mtu kupanda cheo. |
Kwa hiyo mfumo huu wa ESS hauna kipimo cha utu,matumizi halali ya pesa kwenye miradi,na mgawanyo wa majukumu kulingana upatikanaji wa kazi,kwa mfano mtu mmemwajiri na hakuna kazi mnamlazimisha jaza tu,jaza tu ifike angalau 60% ili apande,kwa hiyo hauna uhalisia bali upande mmoja tu unaamua kutegemea na msimamizi pasipo kuzingatia hadhi na mantiki ya Jambo mpaka lipelekewe kuwa lazima na litaftiwe adhabu(manyanyaso),Je akiwashtaki mmemwajiri more than 8 hours kwa kukaa tu kama mfungwa wa akili ofsini,Je yeye ni wa mshahara tu? hamuoni ninyi ndo mna makosa hata ya kumlipa mshahara?Peace of mind is more prices hasa tutakapokuwa tumethamini elimu vitendo kwa kutoiua na kuirithisha kizazi kwenda kizazi kwa vitendo katika mazingira karakana na mazingira kazi.Kwa viongozi wa baadhi ya nchi wamefanya kazi kubwa hasa ni ile namna ya kufika uchumi wa juu kwa mazingira yasiyo rafiki kutoka mataifa ya nje lakini tukibotesha na haya mengine tunayopigia kelele tutafika pazuri zaidi.
Lakini zipo nchi(Uholanzi) zinazowalipa wasio na kazi na hata ghiriba ya kufukuzwa kazi bila kosa lazima miezi miwili mshahara wako ulipwe na 70% kwa mwezi mpaka kuisha mzigo wote kwa kipindi cha mkataba endapo taasisi imefeli yenyewe.Na zipo zingine nyingi zina mfumo bora wa kuwatambua watumishi wao wanaopanda madaraja,mfano Singapore,Canada na Swedeni kusema zote karatasi haitoshi ila muda unatosha.

- Singapore,Wana Mfumo wa tathmini wanaouita Performance management system(PMS),Deep system,Malengo yaliyowekwa kwanza ya pamoja kwenye vituo vya kazi,Ukaguzi wa kimkakati,unaoenda sambamba na muda wa mradi kutoka kwa wasimamizi kuhusu utekelezaji wa malengo hayo.
- New Zealand 🇳🇿,wana mfumo katika eneo siri wanaouita Performance improved framework(PIF),mfumo huu huendeshwa kwa ushirikiano mkubwa kati ya mtumishi na msimamizi na ni tathmini zinazoendeshwa kwa maadili ya eneo la kazi linaloendana na uhalisia wa muda na bajeti.
- Canada,wao wana mfumo uitwao Results- based Management(RBM),ufuatiliaji wa matokeo,tathmini ya kuendeleza na usawa na uwazi.
- Denmark,wana mfumo wa tathmini uitwao Public sector perfomance management(PSPM).Uwajibikaji wa taasisi,Kuweka malengo ya muda mrefu na kuunga mkono na data halisi.
- Australia,wao wanao mfumo wa kutathmimi wanaouita Australian Public Service performance frame work,Mfumo uliojikita hasa kutambua mchango wa mtumishi kwa wananchi kutokana na kazi za wananchi.Tathmini ya utendaji na maoni ya wananchi.
Nashauri, japo wapo wanaoweza pinga utaratibu wa Mungu,wapendao imani ya Mungu na mafundisho bora (Philosophy) wawatambue watu wote katika mema,Wapo kwa mfumo huu watasema wazi kuwa Hatuchezi ng'oo wakiwa upande wa Kazi na utu(Derby ya Mama) tusonge mbele licha ya mazingira yetu kuwa bado tuvumiliane kuliko kutuletea magari ya washa washa kwenye vituo vya kazi(Jangwani na sehemu zingine) kwa makosa ambayo hatujakaa tukayarekebisha kwanza sisi wenyewe.
ASANTENI,msiwafanyie jambo linalo ashiria ukatili wowote jamani,Kalooism ina amini Ufundi wa chombo kwa mtu hupimwa na wapita njia,wakikikubali chombo, hicho ndicho chombo kwa air.(Wema wa Mungu-Umewazunguka).Think Big is rated to Rev.......