Endapo Katiba Inayopendekezwa Itakataliwa

Okay, orodhesha lakini ujue kwamba hakuna Katiba yoyote duniani ambayo ina vifungu vinavyomfurahisha kila mtu!
Naomba nikuulize maswali yafuatayo kwa sasa tu. Na naomba unijibu vizuri kwa ustaarabu.
1. Katiba ni mali ya wananchi wote, na inafaa kuafikiwa na vikundi vyote vya kisiasa. Itakuwaje chama cha upinzani (CDM, CUF au NCCR, au vyote kwa pamoja) kikishika dola wakati hawakushiriki kuandika na hawaitambui katiba hii?
2. Itakuwaje Rais-mteule akitokea chama tofauti na kile chenye wabunge wengi bungeni? Huoni kama atalazimika kuchagua waziri mkuu na mawaziri wengine kutokea chama hicho chenye wabunge wengi bungeni, na hivyo basi hawezi kuendelea kuwa kiongozi wa serikali? Tuamue moja. kama rais ataendelea kuwa kiongozi wa serikali basi mawaziri wasitokane na wabunge la sivyo wadhifa huo wa kiongozi wa serikali apewe waziri mkuu, Rais abaki tu kuwa mkuu wa nchi na amiri jeshi mkuu. Lakini katiba mpya imeendeleza mfumo wetu wa kizamani ambao hautatekelezeka huko mbele kadri vyama vya upinzani vinavyoendelea kukua.
3. Kwa nini mambo mengi mazuri yaliyolenga kuwawezesha wananchi kuwawajibisha viongozi wao yameondolewa? We all have standards that we expect our leaders to live up to lakini hawa wameondoa hata kifungu cha kuwataka wabunge wawe na angalau elimu ya form 4. ni kwa nini? kumbuka hata kupata udereva serikalini wanasema lazima uwe umefika form 4. iweje mbunge aponee sharti hilo?
4. Kwa nini wabunge toka Zbar waendelee kushirikishwa kujadili mambo ya bara wakati wabunge wa bara hawashirikishwi kujadili mambo ya Zbar?
Nijibu hayo kwanza lakini yapo mengi tu!
PS: fahamu kwamba mimi siyo muumini wa serikali tatu!
 
Majibu ni kama ifuatavyo:
SWALI LA 1. CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI (=UKAWA) hawakufuzwa na mtu yeyote katika Bunge Maalum la Katiba bali walitoka wenyewe kwa sababu wanazozijua wao. They are not supposed to benefit from their own wrong in the first place! Kwa hiyo endapo Katiba itatungwa lakini wao hawakubaliani nayo hakuna njia nyingine ya kuwafanya waikubali! Hata katika kura za maoni haiwezekani kupata 100% ya wananchi wote kuikubali Katiba! Hata tukiweka SERIKALI 3 ndani ya Katiba hutapata 100% ya wananchi wanayoikubali Katiba! Kwa hiyo wana-UKAWA kuweni wapole tu, subirini muaibike kwenye kura za maoni!

SWALI LA 2: Mkuu mfumo usipotekelezeka basi itabidi Katiba ifanyiwe mabadiliko, as simple as that! Sijajua kwa nini wana-UKAWA wamekuwa na mawazo ambayo yamefika kwenye dead-end! Nikujulishe kwamba hakuna Katiba itakayo dumu milele bila kufanyiwa mabadiliko au kufutwa kabisa!

SWALI LA 3: Mimi nakubaliana na wewe kwamba kuna mambo mazuri yaliyoondolewa yanayowawajibisha viongozi, kwa mfano Wabunge kuwa "recalled" na wananchi. Japokuwa nakubaliana wa wazo la uwajibishaji wabunge, lakini sikubaliani na namna ilivyokuwa kwenye Rasimu ya Warioba, kwamba eti Mbunge asipoonekana Bungeni kwa miezi sita (6) basi awe "recalled!" Ni mawazo yangu kwamba Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba walitakiwa waboreshe kifungu hiki badala ya kukitoa kabisa!!
Kuhusu wabunge na elimu, nafikiri wananchi waachiwe waamue wenyewe kama wataongozwa na Form IV leaver, Mwenye Digrii au la!

SWALI LA 4: Si kweli kwamba Wabunge wa Bara hawakujadili mambo ya Zanzibar. Mambo yaliyojadiliwa ni Orodha ya Mambo ya Muungano, Zanzibar kuruhusiwa kukopa, Zanzibar kuruhusiwa kujiunga na Jumuiya za Kimataifa, nk. Pamoja na hayo yote Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011 imewapa Mamlaka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wale ambao ni miongoni mwa 201 kujadili masuala yote yaliyoletwa Bungeni, sioni kosa lao ni nini hapa!

Nawasilisha tafadhali!!
 
Wakuu
Endapo UKAWA watapiga kampeni za kutosha hasa upande wa Zanzibar tunaweza tusipate Katiba mpya kwa kuwa 2/3 itakuwa haijapatikana.
End result ni kwamba tutabaki na Katiba ya JMT, 1977 ambayo ina mambo machache mazuri ukilinganisha na Katiba inayopendekezwa! Kwa mfano Katiba inayopendekezwa ina mambo yafuatayo mazuri sana:

1. Matokeo ya kura za Urais kupingwa mahakamani.

2. Mgombea huru.

3. Tume Huru ya Uchaguzi.

4. Zanzibar kukopa.

5. Zanzibar kujiunga na Jumuiya za Kimataifa.

6. Migongano ya Katiba ya JMT na ya Zanzibar imeondolewa.

7. Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais.

8. Kuondolewa mafuta na gesi kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.

9. Nk.
Tukipiga kura ya HAPANA maana yake hayo mambo hapo juu tutayakosa na tutarudi kwenye Katiba ya sasa.

Watu wasifikiri kwamba Katiba inayopendekezwa itarudishwa Bungeni kufanyiwa marekebisho.
Ni heri tukubali Katiba inayopendekezwa, hayo madai mengine tuendelee kuyadai taratibu.
Otherwise, hata kama tukiikataa Katiba inayopendekezwa simply kwa kuwa haina Serikali 3 tutaendelea na Katiba ya sasa ambayo nayo haina Serikali 3.

Nawasilisha kwa mjadala zaidi.

Wazanzibari wanataka mamlaka kamili na sio kikopa.
 
Kwa hiyo wabunge wakiwa Form IV ndio Katiba itakuwa haiwalindi watawala?

Hoja ni kwamba, Std VII level anaweza kuhoji contents za mikataba inayoingiwa na nchi hii? Deo Sanga (CCM-Njombe Kaskazini) ambaye alirukaruka bungeni baada ya katina pendekezwa kupita, katoa hoja ngapi za mashiko bungeni?
 
Mbona kuna ma-Dr na ma-Prof bungeni lakini hatuoni michango yao?
Wengine ni wanasheria lakini wanaporomosha matusi kwa Waasisi wa Taifa hili tu Bungeni!
 
Unachekesha sana, ile rasimu ya jaji Warioba ni ya ukawa?
Kwani hiyo Rasimu ya Warioba imetaja "Mamlaka Kamili" ya Zanzibar? Au hujui maana ya "Mamlaka Kamili?"
 
Sikiliza uvumbuzi wa rasimu ya katiba, walio toa maoni katika pande mbili za muungano, Zanzibar asilimia 60 wanataka muungano wa mkataba, hivyo tunapoongelea mkataba ni zanzibar kuwa na mamlaka kamili, katika rasimu ya warioba ndio ilikuwa foundation ya zanzibar na Tanganyika kuelekea mamlaka kamili.
 
Takwimu za Warioba ziko highly questionable, ni kama vile walitafuta takwimu ili kujustify wanachotaka, wewe subiri tu kura za maoni, hizo zitakata mzizi wa fitna!
 
Majibu ni kama ifuatavyo:
SWALI LA 1. CHADEMA, CUF na NCCR MAGEUZI (=UKAWA) hawakufuzwa na mtu yeyote katika Bunge Maalum la Katiba bali walitoka wenyewe kwa sababu wanazozijua wao. They are not supposed to benefit from their own wrong in the first place! Kwa hiyo endapo Katiba itatungwa lakini wao hawakubaliani nayo hakuna njia nyingine ya kuwafanya waikubali! Hata katika kura za maoni haiwezekani kupata 100% ya wananchi wote kuikubali Katiba! Hata tukiweka SERIKALI 3 ndani ya Katiba hutapata 100% ya wananchi wanayoikubali Katiba! Kwa hiyo wana-UKAWA kuweni wapole tu, subirini muaibike kwenye kura za maoni!

SWALI LA 2: Mkuu mfumo usipotekelezeka basi itabidi Katiba ifanyiwe mabadiliko, as simple as that! Sijajua kwa nini wana-UKAWA wamekuwa na mawazo ambayo yamefika kwenye dead-end! Nikujulishe kwamba hakuna Katiba itakayo dumu milele bila kufanyiwa mabadiliko au kufutwa kabisa!

SWALI LA 3: Mimi nakubaliana na wewe kwamba kuna mambo mazuri yaliyoondolewa yanayowawajibisha viongozi, kwa mfano Wabunge kuwa "recalled" na wananchi. Japokuwa nakubaliana wa wazo la uwajibishaji wabunge, lakini sikubaliani na namna ilivyokuwa kwenye Rasimu ya Warioba, kwamba eti Mbunge asipoonekana Bungeni kwa miezi sita (6) basi awe "recalled!" Ni mawazo yangu kwamba Wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba walitakiwa waboreshe kifungu hiki badala ya kukitoa kabisa!!
Kuhusu wabunge na elimu, nafikiri wananchi waachiwe waamue wenyewe kama wataongozwa na Form IV leaver, Mwenye Digrii au la!

SWALI LA 4: Si kweli kwamba Wabunge wa Bara hawakujadili mambo ya Zanzibar. Mambo yaliyojadiliwa ni Orodha ya Mambo ya Muungano, Zanzibar kuruhusiwa kukopa, Zanzibar kuruhusiwa kujiunga na Jumuiya za Kimataifa, nk. Pamoja na hayo yote Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, 2011 imewapa Mamlaka Wajumbe wa Baraza la Wawakilishi pamoja na wale ambao ni miongoni mwa 201 kujadili masuala yote yaliyoletwa Bungeni, sioni kosa lao ni nini hapa!

Nawasilisha tafadhali!!

Nijuavyo mimi katiba inapoundwa inafaa kuangalia hali ya sasa na ya baadaye ili isiwe ni document inayobadilishwa ovyoovyo. Waasisi wa mataifa makuu kama vile Marekani walilijua hilo na ndiyo maana mpaka leo hujasikia katiba za nchi hizo zinafanyiwa fundamental changes, haswa kwenye structure of government. CCM walipitisha katiba yao wakijua they'll be in power till kingdom come!
Hukulielewa swali langu la mwisho. Muundo wa bunge ulioko kwenye katiba mpya unawawezesha wabunge wa Zbar kushiriki maamuzi ya bara ilhali wa bara hawawezi kushiriki maamuzi ya Zbar. Kwa nini iwe hivyo?
 
Tukiangalia hali ya sasa na ya baadaye Mfumo wa Serikali 3 utaua Muungano, lakini kwa wana-UKAWA kwa kuwa nia yao ni kuua Muungano kwa faida ya wale waliowatuma ndio maana hilo haliwakeri!
 
Kinachoweza kuvunja muungano ni will ya wananchi na siyo idadi za serikali. Ila kweli naamini serikali tatu zingeelekea kuvunjika kwa muungano. But thats not what we r discussing here. Mimi sisupport idea ya serikali tatu, lakini pia naona katiba hii pendekezwa ina mapungufu mengi kuliko hata ile iliyoletwa na tume ya mabadiliko ya katiba!
 
Kama ni habari ya WILL ndio maana tunazungumzia nia ya wana-UKAWA ni kutuletea Muungano usiotekelezeka na mwisho wake ni kuvunjika! Wewe umewahi kuona wapi Serikali haina vyanzo vya mapato inasubiri ichangiwe halafu Serikali hiyo ikawa imara? Vitu vingine havihitaji hata kwenda shule mnaving'ang'ania tu!

Kuhusu Katiba kuwa na mapungufu ni kwamba hata siku moja huwezi kuwa na Katiba inayokubaliwa na kila mtu! Haijawahi kutokea Duniani na haitatokea! Na kama wana-UKAWA mnataka kuwa na Katiba inayomfurahisha kila mtu basi mnafanya Kazi isiyowezekana, poleni sana!! Hata Katiba za vyama vyenu zinalalamikiwa, don't you ask yourselves why?
 
Hapo kwenye red hapo. Kwani kazi ya bunge maalum ilikuwa ni nini? Kuona jinsi serikali tatu zingetekelezeka bila kuleta even the slightest possibility ya muungano kuvunjika. kama ni kuongezewa vyanzo vya mapato, wangefanya hivyo ili serikali ya muungano itengemae zaidi na kuwa na nguvu kuliko hizi za washirika. Lakini sio kufuta kabisa uwepo wa serikali tatu! Only nyie wana-CCM wenye imagination ndogo ndio hamuoni kwamba serikali tatu kwanza ingetuwezesha kuingiza mfumo wa serikali moja kimyakimya!
 
hatutasusia wala kuabikia mtakaoaibika ni nyie wadhulumaji wa wananchi na wanyonyaji na wenye uchu wa madaraka nyie mmeweka kifungu cha mbunge hata akiwa standard seven ni sawa na mnataka dreva wa serikalini aishie form four mnashangaza sana tena mnastaajabisha hata watu wa nje wanashangaa sisiemu mlivyo na ubwanyanya hovyo

Mkuu,
Siku ya kuaibika wana-UKAWA kwa mara nyingine haiko mbali, jiandaeni na "excuses" kama kawaida yenu msusie kura za maoni!
 
Tatizo lenu UKAWA mnafikiri Rais ajaye naye atakuwa anawaalika Ikulu na kuruhusu maandamano ya kubughudhi wananchi kama Rais Jakaya Kikwete!
Mtamkumbuka sana JK, hao wengine hawatawavumilia michezo ya kitoto mnayoifanya hiyo!

Je Huyo Rais atakuwa ni KIONGOZI au MTAWALA? kwa hiyo na kina ulimboka na kubenea na wenzao nao watamkumbuka JK Au ni wewe na familia yako tu?

Kwa kweli Upumbavu ni mzigo mzito. Mtu anayeshupaza shingo ni mtu wa hovyo sana.
 
JK kawaendekeza basi mmekuwa watu wa kuleta vurugu tu nchini, mzee wa watu hana hiana anawaalika tu Ikulu pamoja na kejeli na dharau mlizomtwika! Hongera zake JK, mkia wa ng'ombe ukikatika ataona umuhimu wake!
 
Back
Top Bottom