Umewahi kuona Katiba isiyokuwa na mambo ya utawala?Humu wengi hamjitambui...
Katiba pendekez imejaa mambo mengi ya kiutawala zaid ata ya tume ya warioba; ccm kama ccm kwel ni chama cha wanyonge na kinaenzi mazuri yote ya Mwl nyerere wangeacha mambo yote ya tume kwny katiba pendekez labda, lakin kumuachia paka achunge samaki(chenge ) ni kujidanganya.
Navyoona mim ktk awamu itayomalzka vbaya hii ndo namb1, waswahil usema ukchangiliwa sana usubr kuzomewa, rais j.k alkua na wafyas weng sana 2005 lakn sasa hawapo tena...
Mkuu Ike, heshima, adabu usiwaite wasio na elimu ya darasani ni mbumbu!, kwani mababu zetu waliishije kabla ya ujio wa wazungu na elimu zao za Darasani!, tafuta historia ya Africa kabla ya ujio wa wazungu!. Mpaka kesho mzungu na elimu yake yote ya darasani, hajaweza kujua pyramids zilijengwaje na hiyo mijabali ilitoka wapi?, ilikatajwe, ilisafirishwaje, na ilipandishwa vipi hadi kule kileleni mwa pyramids!.Wewe unajisikiaje kuongozwa na mbumbu?
Wana-UKAWA ndio wameridhika na hali iliyopo, ndio maana wanataka tupige kura ya HAPANA ili tubaki na Katiba ya sasa!
BUCHANAN hakuna thread unayotoa yenye mrengo mzur kila wakat upo biased,kwanza nikufahamishe kuwa hoja ya katiba mpya ililetwa na upinzan na zaid ya 75% ya ccm walikataa rais akatumia busara zake sasa unaposema kuwa CHADEMA hawataki katiba mpya sikuelewi kabisa.Pia unapotaja masuala ya matokeo ya rais kupingwa mahakaman ni kitu kizur sikuelewi na unacheza na akil za watu maana jinsi wanavyopatikana hao majaji hawawez kumhukumu vibaya aliyewateua kwahiyo yatakuwa kama ilivyo sasa,baraza la vijana kama wamesha kiuka msingi wa demokrasia kunauwezekano wa kuwaweka watoto wao kama viongoz.
kuhusu 50% kwa 50% katiba haijaeleza inavyo patikana maana bunge la ccm siliamini wanaweza kuweka wake na watoto wao kike ilikutimiza hamcn kwa hamcn.mwisho mkubali kuwa upinzan ni wachache ila wana hoja za kisomi zenye mantiki,upinzan hawana haja ya kupiga kampen n kuelimisha
Mkuu Pasco,Mkuu Ike, heshima, adabu usiwaite wasio na elimu ya darasani ni mbumbu!, kwani mababu zetu waliishije kabla ya ujio wa wazungu na elimu zao za Darasani!, tafuta historia ya Africa kabla ya ujio wa wazungu!. Mpaka kesho mzungu na elimu yake yote ya darasani, hajaweza kujua pyramids zilijengwaje na hiyo mijabali ilitoka wapi?, ilikatajwe, ilisafirishwaje, na ilipandishwa vipi hadi kule kileleni mwa pyramids!.
Tafuta historia za dola za kale za Axum, Chaka Zulu, Monomotapa, Pete, Bunyoro, Nyanyembe, act ujiulize kiwango cha civilization ile kilitoka wap bila elimu ya darasani!.
Kachimbe historia za kina Socrates, Plato, Mfalme Suleiman, Mtemi Mirambo, Manka Musa, Mkama Rumanyika, Kabaka Mutesa, Mtwa Mkwawa, Munyigumba, Kinjekitile Ngwabi! Chabruma, Mangi Sina, Isike, waliwafanya nini wazungu na elimu zao za Darasani, ilihali , hao hawakusoma darasa hata moja?!.
Nenda kwenye historia ya Tanganyika uone michango ya watu kama kina Sheik Amri Abeid, Hasan Bin Amir, Suleiman Takadir, na wengine wengi tuu wa ilmu za madrasa huku dasani ni safari, lakini wamefanya makubwa kumsaidia Msomi Julius kuleta uhuru wa nchi hii!.
Nimalizie kwa kukuomba linganisha michango ya Professor Maji Marefu na Darasa lake la Saba msilikize lake msilikize kwa makini anavyochangia bungeni, halafu linganisha na Professor Juma Kapuya, professor wa darasa uniambia nani anachangia michango ya maana!.
Mmoja wa wanamuziki maarufu kabisa duniani, Michael Jackson, ulizia alisoma hadi darasa la ngapi?.
Mtanzania tajiri kabisa kuliko Watanzania wote kwa utajiri wa kihalali na kihaki, akiachana na mijizi, mijambazi, na mifisadi, ni Said Salim Bakhressa, ulizia alisoma hadi darasa la ngapi?.
Nimekereka sana kutuita sisi tulio ishia la saba ni ma mbumbu!.
Pasco
Wakuu
Endapo UKAWA watapiga kampeni za kutosha hasa upande wa Zanzibar tunaweza tusipate Katiba mpya kwa kuwa 2/3 itakuwa haijapatikana.
End result ni kwamba tutabaki na Katiba ya JMT, 1977 ambayo ina mambo machache mazuri ukilinganisha na Katiba inayopendekezwa! Kwa mfano Katiba inayopendekezwa ina mambo yafuatayo mazuri sana:
1. Matokeo ya kura za Urais kupingwa mahakamani.
2. Mgombea huru.
3. Tume Huru ya Uchaguzi.
4. Zanzibar kukopa.
5. Zanzibar kujiunga na Jumuiya za Kimataifa.
6. Migongano ya Katiba ya JMT na ya Zanzibar imeondolewa.
7. Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais.
8. Kuondolewa mafuta na gesi kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.
9. Nk.
Tukipiga kura ya HAPANA maana yake hayo mambo hapo juu tutayakosa na tutarudi kwenye Katiba ya sasa.
Watu wasifikiri kwamba Katiba inayopendekezwa itarudishwa Bungeni kufanyiwa marekebisho.
Ni heri tukubali Katiba inayopendekezwa, hayo madai mengine tuendelee kuyadai taratibu.
Otherwise, hata kama tukiikataa Katiba inayopendekezwa simply kwa kuwa haina Serikali 3 tutaendelea na Katiba ya sasa ambayo nayo haina Serikali 3.
Nawasilisha kwa mjadala zaidi.
UKAWA walitakiwa kubaki Bungeni ili kuyasema hayo yote!Hayo yote Bwana bucha,yalikuwemo kwenye rasimu,watawala walichofanya ni kuondoa vipengele vitakavyowabana katika maadili na uwazi,hebu jiulize kwanini mikataba ya wawekezaji ni siri?kuna nini?ndiyo ujue kuwa watawala huwa wana hisa kwenye hiyo mikataba,utakuta ili mwekezaje apate hiyo fursa sharti atoe % Fulani kwa wakubwa na ndiyo maana kiasi ambacho serikali inapata kinakuwa kidogo sana.
Na wawekezaji wanakuwa na kiburi sana hata cha kuwadhulumu wananchi ardhi huku watawala wakifurahia kwani wanapata kitu hapo,kwahiyo hii katiba pamoja na mambo mazuri machache ya kutudanganyia,imetengenezwa kulinda mafisadi.
Kwa hiyo tukiikataa Katiba inayopendekezwa ndio itakuwa dawa yake?
Kwa Zanzibar zinaweza hata iwe ngumu "kuzitosheleza" mkuu!
UKAWA walitakiwa kubaki Bungeni ili kuyasema hayo yote!
Ili ujue hii ni nchi ya kiibilisi sheria ya kuwa dereva wa gari la serikali ni lazima uwe na form iv ila amwendeshe Mbunge mbulula daaaa mwanangu kua uyaone.