Endapo Katiba Inayopendekezwa Itakataliwa

Buchanan

JF-Expert Member
Joined
May 19, 2009
Posts
13,192
Reaction score
1,982
Wakuu
Endapo UKAWA watapiga kampeni za kutosha hasa upande wa Zanzibar tunaweza tusipate Katiba mpya kwa kuwa 2/3 itakuwa haijapatikana.
End result ni kwamba tutabaki na Katiba ya JMT, 1977 ambayo ina mambo machache mazuri ukilinganisha na Katiba inayopendekezwa! Kwa mfano Katiba inayopendekezwa ina mambo yafuatayo mazuri sana:

1. Matokeo ya kura za Urais kupingwa mahakamani.

2. Mgombea huru.

3. Tume Huru ya Uchaguzi.

4. Zanzibar kukopa.

5. Zanzibar kujiunga na Jumuiya za Kimataifa.

6. Migongano ya Katiba ya JMT na ya Zanzibar imeondolewa.

7. Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais.

8. Kuondolewa mafuta na gesi kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano.

9. Nk.
Tukipiga kura ya HAPANA maana yake hayo mambo hapo juu tutayakosa na tutarudi kwenye Katiba ya sasa.

Watu wasifikiri kwamba Katiba inayopendekezwa itarudishwa Bungeni kufanyiwa marekebisho.
Ni heri tukubali Katiba inayopendekezwa, hayo madai mengine tuendelee kuyadai taratibu.
Otherwise, hata kama tukiikataa Katiba inayopendekezwa simply kwa kuwa haina Serikali 3 tutaendelea na Katiba ya sasa ambayo nayo haina Serikali 3.

Nawasilisha kwa mjadala zaidi.
 
Km vilaza wengi hivi nchini kupata mageuzi ni ngumu kwelikweli aise Nina wasiwasi na elimu yako.

I wonder kwamba Jf bado ina akina buchanan wa kumwaga hadi leo. Hivi alipewaje u mod huyu hapo kabla? Hajajua kua katiba pendekezwa inalinda watawala kuliko wenye nchi? Utafurahiaje katiba inayotaka wabunge wawe std VII au chini ya hapo?
 
Sio std Vii bali wajue kusoma na kuandika. Hata watoto wa chekechea wanajua kusoma na kuandika. Katiba kerli hiyo
 
  • Thanks
Reactions: ffn
Tatizo letu ni moja tu kwa watanzania walio wengi UJINGA (waliosoma+ambao hawajasoma)
 
Wakuu,
Endapo UKAWA watapiga kampeni za kutosha hasa upande wa Zanzibar tunaweza tusipate Katiba mpya kwa kuwa 2/3 itakuwa haijapatikana!
End result ni kwamba tutabaki na Katiba ya JMT, 1977 ambayo ina mambo machache mazuri ukilinganisha na Katiba inayopendekezwa! Kwa mfano Katiba inayopendekezwa ina mambo yafuatayo mazuri sana:
1. Matokeo ya kura za Urais kupingwa mahakamani,
2. Mgombea huru,
3. Tume Huru ya Uchaguzi,
4. Zanzibar kukopa,
5. Zanzibar kujiunga na Jumuiya za Kimataifa,
6. Migongano ya Katiba ya JMT na ya Zanzibar imeondolewa,
7. Rais wa Zanzibar kuwa Makamu wa Rais,
8. Kuondolewa mafuta na gesi kwenye Orodha ya Mambo ya Muungano,
9. Nk.
Tukipiga kura ya HAPANA maana yake hayo mambo hapo juu tutayakosa na tutarudi kwenye Katiba ya sasa.

Watu wasifikiri kwamba Katiba inayopendekezwa itarudishwa Bungeni kufanyiwa marekebisho!
Ni heri tukubali Katiba inayopendekezwa, hayo madai mengine tuendelee kuyadai taratibu!
Otherwise, hata kama tukiikataa Katiba inayopendekezwa simply kwa kuwa haina Serikali 3 tutaendelea na Katiba ya sasa ambayo nayo haina Serikali 3!

Nawasilisha kwa mjadala zaidi!

Watz tuna safari ndefu sana mpk kuja kujitambua! Inabd hiki kizazi kife labda kitakachofuatia kitakuwa kinajitambua! Mawazo ya mtu ambaye anaweza kupata hata sources of information kuhusu nchi inavyokwenda anazdiwa na mtu wa kijijini ambaye hawez kupata hata gazeti akalisoma! Wakati mwingne tuache mahaba na vyama vya siasa tuangalie maslahi ya taifa! KATIBA YA WANANCHI lazma ipatkane!
 
Km vilaza wengi hivi nchini kupata mageuzi ni ngumu kwelikweli aise Nina wasiwasi na elimu yako.

Wewe mwenye elimu isiyokuwa na wasiwasi si ungetoa hoja yako badala ya kejeli? Au kutoa kejeli ndio kuwa na elimu kwenyewe?
 
Watz tuna safari ndefu sana mpk kuja kujitambua! Inabd hiki kizazi kife labda kitakachofuatia kitakuwa kinajitambua! Mawazo ya mtu ambaye anaweza kupata hata sources of information kuhusu nchi inavyokwenda anazdiwa na mtu wa kijijini ambaye hawez kupata hata gazeti akalisoma! Wakati mwingne tuache mahaba na vyama vya siasa tuangalie maslahi ya taifa! KATIBA YA WANANCHI lazma ipatkane!
Haya niambie, Katiba ya Wananchi ni ipi? Je, ni ile inayokubali Serikali 3 au ile inayokubali Muungano wa "Nkataba?"
 
kazi kweli kweli! ina maana katiba ya wananchi hujui sifa zake na inatakiwa iweje? hujiulizi kwanini maoni ya wananchi kupitia tume ya warioba yametupwa na watawala?
Mjinga siku zote atabaki kuwa mjinga tu hata umwelimishe vipi.
 
Ili ujue hii ni nchi ya kiibilisi sheria ya kuwa dereva wa gari la serikali ni lazima uwe na form iv ila amwendeshe Mbunge mbulula daaaa mwanangu kua uyaone.
Kwa hiyo tukiikataa Katiba inayopendekezwa ndio itakuwa dawa yake?
 
kazi kweli kweli! ina maana katiba ya wananchi hujui sifa zake na inatakiwa iweje? hujiulizi kwanini maoni ya wananchi kupitia tume ya warioba yametupwa na watawala?
Mjinga siku zote atabaki kuwa mjinga tu hata umwelimishe vipi.
Kwa hiyo maoni aliyoyatupa Warioba sio maoni ya Wananchi?
 
Sio std Vii bali wajue kusoma na kuandika. Hata watoto wa chekechea wanajua kusoma na kuandika. Katiba kerli hiyo
Kwa hiyo tukiikataa Katiba Inayopendekezwa ndio tutakuwa tumetatua tatizo?
 
Wakuu,
Endapo UKAWA watapiga kampeni za kutosha hasa upande wa Zanzibar tunaweza tusipate Katiba mpya kwa kuwa 2/3 itakuwa haijapatikana!
End result ni kwamba tutabaki na Katiba ya JMT, 1977!.
Suala la kura kutosha halina mjadala kabisa!, kura zisipotosha, zitatosheshwa! na katiba mpya itapatikana!.
Pasco
 
I wonder kwamba Jf bado ina akina buchanan wa kumwaga hadi leo. Hivi alipewaje u mod huyu hapo kabla? Hajajua kua katiba pendekezwa inalinda watawala kuliko wenye nchi? Utafurahiaje katiba inayotaka wabunge wawe std VII au chini ya hapo?
Kwa hiyo wabunge wakiwa Form IV ndio Katiba itakuwa haiwalindi watawala?
 
Kwa hiyo maoni aliyoyatupa Warioba sio maoni ya Wananchi?

Wapishi, walinzi, masecretary na madereva siku hizi ni lazima wawe na elimu ya form iv. Cha kushangaza watunga utaratibu wa kuishi hakuna kiwango cha elimu wanawekewa. Kuanzia elimu ya awal anaweza kuwa mbuge kama ataimaliza na akajua kusoma na kuandika. Hii ni tz tu.
 
Suala la kura kutosha halina mjadala kabisa!, kura zisipotosha, zitatosheshwa! na katiba mpya itapatikana!.
Pasco
Kwa Zanzibar zinaweza hata iwe ngumu "kuzitosheleza" mkuu!
 
Wapishi, walinzi, masecretary na madereva siku hizi ni lazima wawe na elimu ya form iv. Cha kushangaza watunga utaratibu wa kuishi hakuna kiwango cha elimu wanawekewa. Kuanzia elimu ya awal anaweza kuwa mbuge kama ataimaliza na akajua kusoma na kuandika. Hii ni tz tu.
Naona wana-UKAWA wengi mmekaririshwa kwamba ubaya wa Katiba inayopendekezwa ni Elimu ya Mbunge!
 
Back
Top Bottom