Endapo hii ndoto inatoka kwa Mungu, basi hatuna budi kuliombea Taifa. Hatari itatokea karibuni

TheDreamer Thebeliever

JF-Expert Member
Feb 26, 2018
2,490
3,534
Habari wadau!

Leo nimeota ndoto mbaya sana, nimeona watu waume kwa wake wakiwa wanalia, nimeona machozi na damu katika ndoto. Nimeona mji ukiwa umetulia tulii mara ghafla fujo ikatawala,taharuki ikaukumba mji wote.

Ndoto yenyewe:

Nimeota nimeenda kumtembelea jamaa yangu anayeishi maeneo ya katikati ya mji. Baada ya maongezi ikabidi nimuage nakushuka chini ya ghorofa na kuanza safari ya kurudi nyumbani.

Wakati nafika chini nje tu ya lile jengo nikaona kitu cha ajabu sana, yaani mtaa mzima hakuna gari wala mtu anayekatiza. Ikanibidi nisogee mbele kutafuta gari ya kunirudisha nyumbani nikaongoza na barabara ya lami inayopita pembeni mwa lile jengo nikasogea mpaka mbele.

Ghafla naona kuna kundi kubwa la vijana wakiwa wamevaa T-shirt nyekundu zenye maandishi meupe japo sikuweza kuzisoma kwa haraka haraka kilichoandikwa kwenye Tshirt zile pia wamevaa na vitambaa vyenye ufito wa bluu na nyeupe kichwani mwao wanakimbia kwa kasi kuja nilipo mimi,ila kuna kila dalili kwamba walikuwa wanakimbizwa lakini sikupata kuwaona watu waliokuwa wanawakimbiza.

Sikuchelewa ikabidi na mimi nianze kukimbia kuepuka lile kundi kubwa ,nageuka nyuma nikimbie nakuta ule upande wa juu wa barabara nilipotikea kuna kundi kama lile ila hawa hawakimbizwi inaonyesha wamesimama tu wanaimba nyimbo zao tu huku wakiruka ruka.

Hapo nikaona bora nikimbie katika uelekeo tofauti na yale makundi mawili, nikapita barabara ya kati kwa pembeni nikaona jengo refu la ghorofa nikakimbia na kuingia mpaka ground floor.

Nafika ground floor nikajihisi nipo salama sasa maana nimeyakwepa makundi yale yote mawili na tayari mkojo ulikwisha nibana kwa hofu iliyonipata, bahati nzuri natazama mbele naona kijana mmoja na binti wamekaa kwenye vingazi vya kupanda floor ya kwanza wakiwa wamepakatana kwa mahaba kabisa ikabidi nisogee ili niwaulize wapi kuna choo kwenye ile ghorofa maana mkojo ulikuwa imenibana.

Ile najaribu kuwasogelea tu niwaulize nikagundua kwamba yule kijana alikuwa anatokwa na machozi na yule mdada damu zilikuwa zinamtoka mpaka amepoteza fahamu.

Oooh nikaona isiwe tabu huyu naye bila shaka ndio wale wale ikabidi nifungue kitasa cha mlango wa mbele yangu niingie ndani nijifungie na funguo.

Haraka haraka nikafungua mlango wa chumba cha karibu yangu na kujifungia kwa ndani.Ile nageuka nyuma tu baada ya kuingia ndani ya kile chumba nakuta watu wamejaa ndani ya kile chumba na wamekikazia macho wakiashiria nitoke nje .

Natazama mkono wangu wa kulia kwa chini naona kuna mshikaji amekee kwenye zulia na watoto wawili wadogo ,jamaa anasimama na kusema "hakuna shida hakuna shida",mara wote mule ndani wanatulia wanaacha kunikazia macho.

Ikabidi nitafute sehemu ndani ya ile seating room nikae ,nikachagua kukaa karibu na yule mshikaji ambaye bila shaka ni mzanzibar kwa muonekano .Wakati natafuta nafasi ya kukaa mara ghafla kipande cha tofali kikarushwa kikavunja dirisha kubwa la mita tatu la pale seating room watu wote wakaogopa lakini hakuna hata mmoja aliyetamani kutoka pale ndani maana bado palikuwa salama licha ya dirisha kuvunjwa.

Ghafla baada ya lile jiwe kurushwa na kuvunja kioo cha dirisha kubwa ikasikika sauti kubwa ikisema "Katiba Mpya".Hapo hapo usingizi ukakatika na ndoto ikaisha ndio nilipogundua kuwa ilikuwa ni ndoto nikatafuta biblia yangu na kuanza kusali.
 
Umeoshawahi kuota ndoto ngapi na zikatokea?
Huwa mgeni akitaka kuja nyumbani kwangu lazima nitaota na kesho yake lazima mgeni huyo aje.Kama ndugu au rafiki ajatembelea kwangu mda mrefu kama atakuja bila kunipigia simu lazima usiku nimuote amekuja na kweli kesho anakuja ,ila hii ndoto tofauti .

Kifupi nina uwezo wa kuona kesho nani atakuja nyumbani kwangu hata kama hatonitaarifu.
 
Habari wadau!

Leo nimeota ndoto mbaya sana, nimeona watu waume kwa wake wakiwa wanalia, nimeona machozi na damu katika ndoto. Nimeona mji ukiwa umetulia tulii mara ghafla fujo ikatawala,taharuki ikaukumba mji wote.

Ndoto yenyewe:

Nimeota nimeenda kumtembelea jamaa yangu anayeishi maeneo ya katikati ya mji. Baada ya maongezi ikabidi nimuage nakushuka chini ya ghorofa na kuanza safari ya kurudi nyumbani.

Wakati nafika chini nje tu ya lile jengo nikaona kitu cha ajabu sana, yaani mtaa mzima hakuna gari wala mtu anayekatiza. Ikanibidi nisogee mbele kutafuta gari ya kunirudisha nyumbani nikaongoza na barabara ya lami inayopita pembeni mwa lile jengo nikasogea mpaka mbele.

Ghafla naona kuna kundi kubwa la vijana wakiwa wamevaa T-shirt nyekundu zenye maandishi meupe japo sikuweza kuzisoma kwa haraka haraka kilichoandikwa kwenye Tshirt zile pia wamevaa na vitambaa vyenye ufito wa bluu na nyeupe kichwani mwao wanakimbia kwa kasi kuja nilipo mimi,ila kuna kila dalili kwamba walikuwa wanakimbizwa lakini sikupata kuwaona watu waliokuwa wanawakimbiza.

Sikuchelewa ikabidi na mimi nianze kukimbia kuepuka lile kundi kubwa ,nageuka nyuma nikimbie nakuta ule upande wa juu wa barabara nilipotikea kuna kundi kama lile ila hawa hawakimbizwi inaonyesha wamesimama tu wanaimba nyimbo zao tu huku wakiruka ruka.

Hapo nikaona bora nikimbie katika uelekeo tofauti na yale makundi mawili, nikapita barabara ya kati kwa pembeni nikaona jengo refu la ghorofa nikakimbia na kuingia mpaka ground floor.

Nafika ground floor nikajihisi nipo salama sasa maana nimeyakwepa makundi yale yote mawili na tayari mkojo ulikwisha nibana kwa hofu iliyonipata, bahati nzuri natazama mbele naona kijana mmoja na binti wamekaa kwenye vingazi vya kupanda floor ya kwanza wakiwa wamepakatana kwa mahaba kabisa ikabidi nisogee ili niwaulize wapi kuna choo kwenye ile ghorofa maana mkojo ulikuwa imenibana.

Ile najaribu kuwasogelea tu niwaulize nikagundua kwamba yule kijana alikuwa anatokwa na machozi na yule mdada damu zilikuwa zinamtoka mpaka amepoteza fahamu.

Oooh nikaona isiwe tabu huyu naye bila shaka ndio wale wale ikabidi nifungue kitasa cha mlango wa mbele yangu niingie ndani nijifungie na funguo.

Haraka haraka nikafungua mlango wa chumba cha karibu yangu na kujifungia kwa ndani.Ile nageuka nyuma tu baada ya kuingia ndani ya kile chumba nakuta watu wamejaa ndani ya kile chumba na wamekikazia macho wakiashiria nitoke nje .

Natazama mkono wangu wa kulia kwa chini naona kuna mshikaji amekee kwenye zulia na watoto wawili wadogo ,jamaa anasimama na kusema "hakuna shida hakuna shida",mara wote mule ndani wanatulia wanaacha kunikazia macho.

Ikabidi nitafute sehemu ndani ya ile seating room nikae ,nikachagua kukaa karibu na yule mshikaji ambaye bila shaka ni mzanzibar kwa muonekano .Wakati natafuta nafasi ya kukaa mara ghafla kipande cha tofali kikarushwa kikavunja dirisha kubwa la mita tatu la pale seating room watu wote wakaogopa lakini hakuna hata mmoja aliyetamani kutoka pale ndani maana bado palikuwa salama licha ya dirisha kuvunjwa.

Ghafla baada ya lile jiwe kurushwa na kuvunja kioo cha dirisha kubwa ikasikika sauti kubwa ikisema "Katiba Mpya".Hapo hapo usingizi ukakatika na ndoto ikaisha ndio nilipogundua kuwa ilikuwa ni ndoto nikatafuta biblia yangu na kuanza kusali.
mnaambiwa maharage si mboga bado mnakula ,angalia sasa shida
 
Back
Top Bottom