ManiTek TV
JF-Expert Member
- Jun 3, 2011
- 410
- 159
Mnigeria Saheed Adepoju, mwanzilishi na CEO wa kampuni ya Encipher Group anatekeleza ndoto ya kuinyanyua Afrika katika Teknolojia kwa kuzalisha kompyuta aina ya tablet, tablet hiyo si miongoni mwa tablet ambazo zinaweza kushindana na iPad, Nexus au Galaxy Tab lakini ni tablet iliyobuniwa Afrika na kutengenezwa na Waafrika, katika kundi (batch) la mwanzo la uzalishaji kampuni ya Encipher Group imezalisha na kuuza Inye 100, sasa Kampuni hiyo inalenga kutoa tablet yao ya toleo la pili ambayo tayari wameishaitangaza.
Inye ina maana ya namba moja kuwa lugha ya kienyeji huko Nigeria inayojulikana kama Igala. Tablet hiyo ya Android ina disk ya ukubwa wa 16GB na RAM 512mb, pia ina betri yenye 2600 mAh. Vile vile Encipher Inye ina Wi Fi na 3G, na mambo yote ya msingi ambayo yanatarajiwa kwenye tablet yoyote ile kama vile sehemu ya kuwekea kadi aina ya MicroSD, tundu ya headphone na spika.
Kwa specs za tablet mpya ya Encipher Inye 2, fuata link ya chini usome makala hii kwa ukamilifu:
Gajetek - Gajet na Teknolojia: Encipher Inye Tablet ya Afrika
