kimbendengu
JF-Expert Member
- Jun 7, 2013
- 6,070
- 10,348
ebue duu hivi ulishindwa kwenda kupata ushauri kwa yahaya,didie,boke,kalou,hakuna ajuaye kesho
Ufala wa kushobokea kuoa wazungu umeanza kujionesha.Na kama Dunia tambara, langu lishatoboka Sina hata pa kulala,Nakesha kwa boka
Hii ni mistari iliyopo katika Wimbo wa SINA wa msanii wa Bongofleva,Harmonize.
Emmanuel Eboue Alicheza katika fainali ya Klabu Bingwa Ulaya 2006, alikusanya mamilioni ya pesa katika miaka 7 aliyocheza katika EPL, hi kwenye nyumba nzuri a kuendesha magari ya kifahari Mambo yamebadilika sasa kwa beki huyo wa zamani wa Arsenal.
Kwa sasa anaishi kwa kuwakimbia watu wa mahakama, muda mwingine analala kwenye sakafu za nyumba za rafiki zake, anasafiri kwa basi na hata pia kufua kwa mikono yakekwa sababu hana mashine ya kufulia Akihojiwa na gazeti la Daily Mirror Eboue,34, amesema kuwa hali hiyo inamfanya mpaka atamani kujiua.
Ninataka Mungu anisaidie." Anasema Eboue, Pekee yeye anaweza kuyaondoa haya mawazo kichwani mwangu Eboue amepoteza utajiri wake wote kutokana na usimamizi mbaya pamoja na kuachana na mke wake ambapo ametengwa mbali na watoto wake Watoto wake wote watatu,hajaonana nao tangu mwezi juni.
Mtoto wake wa kiume,Mathis anacheza katika Academy ya Arsenal.
Baada ya kushindwa ka vita ya talaka, mahakama iliagiza mali zake zote ziende kwa mkewe, Aurelie ambaye ni raia wa Ubelgiji Pia anataraji kukabidhi kwa mkewe jumba lake la kifahari lililopo Enfield,London, endapo atashindwa kufanya hivyo jaji atasaini kuruhusu madalali waende kumtoa.
Eboue anasema kuwa, sasa hana pesa ya kuwalipa mawakili ili kufattilia mali zake. Nipo ndani ya nyumba lakini ninaogopa.
Kwa sababu sijui muda gani polisi watakuja, Muda mwingine ninazima taa kwa sababu sitaki wajue kama nipo ndani," Alisema Kutokana na kuwa na elimu ndogo,alikuwa anatuma karibia mshahara wote kwa mkewe. Na wakati wowote mkewe alikuwa akimtaka asaini hati (Document) yoyote alikuwa anasaini.
Mipango yake ya kurudi katika EPL iliota mbawa msimu uliopita, alisajiliwa na Sunderland lakini hakucheza hata mechi 1 kufuatia kufungiwa na Fl FA kutokana na kushindwa kumlipa wakala wake wa Zamani
Cc ws14
mbona inaonesha kafungiwa kucheza mpira kwa mzozo na wakala wake!?Hakuna cha mental illness jiulize kwanini hachezi Mpira na haja staafu na hana majeruhi ?
Alisajiliwa na klabu yake mpya uturuki kwenye vipimo alifeli na taarifa za madaktari zinasema wame spot virus na wakaishia hapo hawakutaka kuendelea mbele ila vyombo vya habari za uturuki zikasema Ebou alifeli vipimo sababu alikutwa na HIV mbona hii habari ilikuwa hot news sana September,
Na saizi kwenye hii taarifa ya Ebou kufilisika wanasema hachezi mpira sababu yupo ill na wala sio majeruhi
Yaani Ebou wa miaka 30 na kitu apate mental illness kisa babu kafa acha masihara ww
HIV inamsumbua na anajuta saizi
Umeandika nilichokua nakifikiliaSi wazungu, wanawake wote hawana huruma na mwanaume yeyote labda awe mtoto wake.Ni vizuri kuishi kwa tahadhari sana na hawa wanawake
Acha uongo eboue alifungiwa kucheza mpira baada ya kusajiliwa na Sunderland mwaka 2016,March.Ndio uhalisia nakumbuka sijui miezi mingapi imepita ndio ilikuwa habari ya mjini ,alitaka kusajiliwa na klabu yake mpya ila alifeli vipimo sababu ya ugonjwa huo
Na stress akawa anajifungia ndani sana na alijaribu kujiua
Acha uongo eboue alifungiwa kucheza mpira baada ya kusajiliwa na Sunderland mwaka 2016,March.
Inasemekana alimtapeli agent wake... Alifungiwa na Fifa kutokucheza mpira kwa miaka kadhaa na mpaka sasa hana team... Alipewa long term Ban.
Muwe mnafuatilia habari acheni uongo na habari za kwenye kahawa.
Ingia hapa Eboue: Year-long ban like being in prison
Acha uongo hizo zilikuwa fake news kitu kilichomfanya asiwe na timu ni kufungiwa mwaka mmoja na FIFA baada ya kuzinguana na wakala wakeEboue
Gaza!Hivi George Best alikuwa Arsenal pia?
Habari imekaa kidaku zaidi.
Jamaa mali zote alikuwa anaandikisha jina mke wakeina maana mke wake kapewa kitu?.....mi najua mkiachana mali zinagawanywa nusu kwa nusu
Halafu mbona demu lenyewe baaayaaaKomenti yako nimecheka sana, jamaa tumuombee kwa mungu , so sad this story, mwanaume unampaje mke umiliki wa mali zote , upoyoyo huo, eti kila kitu unachonunua unaandika jina la mke, inaonekana alikufa kwa mkewe kabisa jamaa