Emmanuel Eboue hali mbaya, Mke amfilisi

MAPENZI YALIVYOACHA KIDONDA KATIKA MAISHA YA EBOUE

NA MESHACK MELELE

Haya mapenzi ni kitu gani kwani? mbona kwangu yamekosa thamani, nayempenda hanipendi nishawaza mpaka nimechoka ni swali alilouliza msanii Mb doggy katika wimbo wake wa mapenzi kitu gani.

Akajibiwa na bendi ya msondo ngoma kuwa mapenzi ni kizungumkuti hayana kanuni, leo unaweza kupendwa kesho ukakataliwa, usijiulize sana tambua umefanyiwa sub bila refa kupiga filimbi achia jezi tu mwanangu.

Haya ndio mapenzi yaliyomfanya staa wa zamani wa klabu ya Arsenal Emmauel Eboue kuomba hifadhi ya kulala sakafuni sebuleni kwa jirani licha ya utajiri alioutengeneza katika nyasi za wazungu pindi akicheza soka.

Ilikua ni mwaka 2017 baada ya mahakama kuamua kila kitu alichokuwa nacho, akikabidhi kwa mkewe wa kizungu aliyeomba taraka, Eboue alibaki hana kitu kwani mali nyingi alizokuwa nazo aliandikisha kwa jina la mkewe, mapenzi upofu.

Yalimpofusha macho Eboue, hakuona kama kuna siku ingekuja kutokea wangetengana na mkewe Aurelie, kwake aliona mwisho wao ungetenganishwa na kifo tu.

Taraka kwake iligeuka maumivu makali sana kama mithili ya kisu cha moto kilichopita katikati ya moyo wake, Aurelie kipenzi chake aligeuka adui yake wa kwanza duniani, hakuamini kuwa kama ndiye yule aliyemvisha pete mwaka 2014.

Aurelie mwanamke mrembo aliyempa maana ya maisha Eboue, sasa akamfanya kuyaona maisha hayana maana tena akatamani kujinyonga, aliona maisha hayana maana tena bila Aurelie kipenzi cha moyo wake.

Imani yake kwa mkewe ilikua kubwa sana kuna kipindi kupitia kinywa chake alitamka kuwa katika mshahara wa euro milioni nane kwa mwaka aliokuwa anapata, alikua anampatia mkewe euro milioni saba kwa ajili ya watoto na familia, Eboue alishikwa akashikika.

Eboue haswa alimuona Aurelie kama jua katika giza lake, maji katika jangwa lake sukari katika chai yake, sasa jua likazima, Eboue akakosa mwanga hapo ndipo alipoanza kupotea, hakujua ashike wapi.

Kila aliyempa ushauri aliona ni kama anamkejeli tu akajenga ukuta wa woga katika fikra zake, mpaka pale alipopata nguvu ya kunyanyuka na kuiambia jamii magumu anayopitia.

Jamii ambayo kwa kiasi ilimpa kitambaa cha kuyafuta machozi yake, ikamwambia bado ana nafasi ya kwanza upya kuliko kujinyonga, klabu ya Galatasaray wakaahidi kumpa kazi ya kufundisha watoto wadogo.

Zaidi ya yote kipenzi chake cha utotoni stephanie Boede mwanamke aliyempenda Eboue kabla hajatoka kabla pesa haijajenga urafiki naye, na kumwona stephanie si mwanamke wa hadhi yake, akakubali kuolewa na Eboue mei 2019, akanza safari mpya katika maisha yake.

Mapenzi kitu gani mwambie Mb doggy tumeshindwa kumjibu, ila la zaidi atambue kuwa kuna mwanamke anaweza akakujenga, na pia kuna mwanamke anaweza akakubomoa na kukuacha na kidonda kama alichoachiwa Eboue kwa Aurelie.

Spidernyoka
Credit kwa
insta@Sportscover123

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Waambie walete story mpya hii ya ebue tushaichoka
 
Story nzuri ya Eboue umechanganya na nyimbo za mb doggy na maneno yako mwisho ujinga mtupu
 
Back
Top Bottom