Elon Musk ametoa majibu kwa wamiliki wa magari ya Tesla waliopendekeza maboresho

Kichwa Kichafu

JF-Expert Member
Apr 13, 2017
44,574
188,785
Habari,

Mkurungezi mtendaji wa kampuni la Tesla Motors, Elon Musk amekubali kufanyia kazi mapendekezo juu ya uboreshaji wa gari za Tesla Model S.

Wateja wawili ambao wanamiliki gari za Tesla Model S, New York hivi karibu wameandika barua ya wazi kupita gazeti moja walipendekeza maboresho kwenye gari za Tesla na Elon Musk kupitia mtandao wa twitter amejibu kwa kusema mapendekezo hayo kwa kiwango kikubwa yatafanyiwa kazi ndani ya muda mfupi.

Mume na Mke wamesema kwenye gazeti hilo kuwa wote ni wanamiliki gari za Tesla japo hawakutaka majina yao kufahamika. Na kwenye gazeti hilo hawakuwa wanatoa makasiriko bali pia walimsifia Elon Musk kwa kusema amefanikiwa kuwaletea gari ambazo ni bora Marekani.

Miongoni mwa mapendekezo yaliyotolewa na wanafamilia hawa kwenye hilo gazeti ni kama:

1. Monitors na Sensors zimpe taarifa mapema dereva pale ambapo barabarani kuna msongamano wa magari na kama kuna kitu ambacho kinaweza kuligonga gari kwa mbele au nyuma.

2. Kifuniko mahali ambapo panatumika ku-charge gari kujifunga mara tu kifaa cha ku-charge kinapotenganishwa. (Disconnected)

3. Kupiga simu kwa kutumia sauti pale anapokuwa ndani ya gari moja kwa moja bila kuwa na haja ya kushika simu.

Gazeti hilo limeoneka limefanya kazi maana limegusa na kuleta attention hadi kwa Elon Musk ambaye ndio CEO wa kampuni hiyo ya magari ya umeme, Tesla.

Haijafahamika moja kwa moja mapendekezo yapi yataanza kufanyiwa kazi japo kampuni la Tesla kutoa ufafanuzi huo mfupi wa kuyafanyia kazi hivi karibu.

Chochote kikitokea tutaendelea kuhabarishana zaidi.

Nawasilisha Mzee Mkoloni.

Cc: Kichwa Kichafu.
 
Huyu jamaa afu juzi tu hapo alitoa challenge ya 1$M kwa atakayefanikisha ku hack gari zake, sijui mshindi kama alipatikana
Hata kabla ya challenge David Colombo, dogo wa miaka 19 alishaona flaws kwenye gari za tesla.

Alikuwa anaweza hack mfumo mzima wa gari za tesla.


 
Huyu jamaa afu juzi tu hapo alitoa challenge ya 1$M kwa atakayefanikisha ku hack gari zake, sijui mshindi kama alipatikana
Hii pia ni moja ya njia inayotumiwa na Kampuni la Tesla kufanya maboresho nakumbuka mara ya mwisho 2019 kuna hackers walizawadiwa gari Model 3 pamoja na $ 1Million baada ya kufanikiwa ku-hack moja ya gari za Tesla.
 
Back
Top Bottom