Eliud Tongora kuipeleka CHADEMA Mahakamani

Eliud Tongora kuipeleka CHADEMA Mahakamani

MwitaOmondi

New Member
Joined
Jul 8, 2015
Posts
2
Reaction score
1
Mtangazania Jimbo la Musoma mjini kwa tiketi ya Chadema, Eliud Tongora (a.k.a. Mkorea) anajiandaa kuipeleka Chadema mahakamani ili alipwe pesa zake sh. 6,000,000/- (milioni sita) alizowapa viongozi wa Chadema wilaya ya Musoma mjini kwa madai kuwa angepitishwa bila kupingwa kugombea Ubunge Jimbo la Musoma mjini.

Jimbo la Musoma mjini ni Jimbo linaloongozwa na Mhe. Vincent Nyerere ambae hakupatikana mara moja kujibu madai haya. Habari za ndani zinaeleza kuwa Tongora kama anavyosema, aliahidiwa pia na viongozi waandamizi wa Chadema akiwemo Rebecca Mngodo, John Shibuda na Said Arfi kuwa angepitishwa kugombea Ubunge huo wa Musoma mjini kwenye vikao vya juu vya Chadema.

Mtangaza nia Tongora baada ya kutoona dalili zozote za ahadi yake kutekelezwa hasa baada ya Mbunge Vincent kuwa na mkutano wa hadhara wenye mafanikio, juzi Jumatatu tarehe 6/7/2015 ametishia kukipeleka Chama cha CHADEMA mahakamani au arudishiwe pesa zake. Viongozi wa wilaya wao wanadai walipokea pesa za Mtangazania huyo na si kwa kiasi anachodai kama mchango wake kwa Chama na si kama anavyodai hivi sasa.
 
Tutashuhudia mambo mengi sana mwaka huu
 
Siamini kama CDM wanafanya Ubunge ni bidhaa sokoni. Kaliwa huyoo, kapotea njia.
 
Hapa chama kina kulana tu. Alichoandika ni umbeya tu. Shibuda wapi na wapi na CDM. Alijitenga tangu mwanzo.

Na umejiunga tu kuja kumhusisha huyu na ubaya wako kwake.
 
Kaliwa tayari huyo au asubirie wakijiunga na chama kingine wanaweza kumpa nafasi ya kugombea ila sio kwa chadema
 
nan alimwambia kuwa chadema inanunuliwa mwehu huyo aende haraka tutamkuta
 
.... Arudi huko ccm. Sisi hapa MUSOMA mjini tunasema Vincent Nyerere MUSOMA mjini tena 2015
 
Mleta mada unaharufu ya unafiki afri shibuda wote wanajulikana ni kina nani hivi huyo jamaa mpaka anataka kugombea,ubunge cdm akijiu chama mpaka awape ela hao watu huu ni uongo na unafiki tena wewe unastahili kuwa kule wasaliti walipo
 
Kama alitoa kama rushwa ajiandae kwenda Lupango bahati nzuri sheria iliopo mpaka sasa kabla ya Membe hajawa rais inaeleza wazi kuwa mtoa rushwa na mpokea rushwa wote ni Lupango.

Klichobaki ni kwa mpokea fedha kuweka wazi kuwa fedha hizo alipokea kwa ajili ya nini,kwa kuwa mtoa rushwa ameshajisemea wazi kwa kinywa chake mwenyewe kuwa alitoa fedha hizo ili aweze kupewa nafasi ya kugombea ubunge ni vema akajisogeza mwenyewe Lupango kabla ya kufikiwa na vyombo vya dola.
 
madai kama haya ata Afande sele aliwahi kusema kuwa aliambiwa atoe hela ili wampitishe agombee ubunge kwa tiketi ya CHADEMA morogoro mjini alikataa wakamwambia agombee udiwani ubunge nafasi zimejaa
 
Mpuuzi tu wa kupuuzwa anatafuta umaarufu kupitia CDM na si mwanachadema sababu katibu Mkuu alishatangaza mapema kwa wanaohitaji kutia nia ubunge na udiwani wapeleke maombi makuu makuu mapema kwa ajili ya kufuatiliwa maadili yao na mienendo yao yeye hakulijua hilo
 
Back
Top Bottom