CHADEMA KUMPA KAMANDA VICENT NYERERE MTIHANI ARUMERU MASHARIKI:
SIFA NADRA ZINAVYOZIDI KUDHIHIRISHA KWAKE KULE ARUMERU MASHARIKI WATANZANIA TUJUE MWALIMU KAFUFUKA UPYA BUTIAMA KWA PICHA YA HUYU KIJANA NA JOHN MNYIKA WOTE WA CHADEMA
CHADEMA kwa uhakika Tanzania nzima imefurahishwa kwa namna mnavyompa uzoefu wa hali ya juu ki-uongozi kijana wetu mpendwa Vicent Nyerere.
Mbali na nyinyi kumpa mtihani kule Arumeru Mashariki, hadi sasa tunachokiona kwake ni pamoja na:
1. Ubunifu wa hali ya juu namna gani kuwa Kampen Manager hodari,
2. Uwezo mkubwa wa kushirikiana na wenzie pamoja na wenyeji wa Arumeru,
3. Kucheza kama mwana-timu na wala katu hakimbii na mpira wa kisiasa uwanja mzima goli hadi goli kama Maradona enzi hizo,
4. Hajajiruhusu kuwa mfungwa wa kujiona mtu mwenye upekee wowote ule,
5. Kwake siasa za majungu na fitna katu,
6. Hupokea maelekezo na kufanya mara tatu ya ufanisi uliotarajiwa,
7. Hajitokezi sana kwenye vyombo vya habari na hupenda kuka 'viti vya nyuma' na wala si kujikweza,
8. Hashiriki siasa za sura-mbili na majungu kwa wakati mmoja ... yaani huyu kijana!!!
.... Wengine huku nje ya uwanja tunaoendele kumsoma bila ya yeye kujua lolote lile wenzenu tunajihisi kama vile mbali na misimamo thabiti ya Mhe Makongoro Nyerere kule Mara hidi ya mdugu UFISADI, kwake huyu kijana kila leo tunazidi kumuona Baba wa Taifa Julius K. Nyerere kazaliwa upya katika nyumba yetu.
Kwa tathmini zangu hizi juu yake tena bila upendeleo wowote; wenzangu ngojeni mtaona huko mbele ya safari. Ndani ya CHADEMA kuna nyota ya mashariki na ishara zake zote.
Ndio, nasema hivi kijana huyu afundishwe kitu UONGOZI WENYE UADILIFU uliotukuka maana hiyo ndio bidhaa kubwa ajabu iliokosekana Tanzania hadi leo hii na kufanya chama hiki pekee ndicho kibakie tumaini la MWISHO kwetu sisi wananchi tusiokua na kitu!!