Kinana, Mbowe, Vuai, Mnyika, Chenge na Heche wajifungia kwa vikao vya saa 4 Courtyard

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,365
8,097
Nini kinaendelea? Hili ni swali linalogonga vichwa vya Watanzania wengi wenye shauku ya kujua majadiliano baina ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yatahitimishwa lini.

Jana vigogo wa vyama hivyo wasiozidi 15 walijifungia kwa saa nne katika Hoteli ya Courtyard jijini hapa, kuendeleza majadiliano yaliyoanza miezi sita nyuma.

Majadiliano ya kwanza yalifanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Mei 20 mwaka huu kwa Rais Samia Suluhu Hassan akiambatana na viongozi waandamizi wa CCM na Serikali, ambao walikutana na ujumbe wa viongozi wa CHADEMA, ulioongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

======================

Tangu wakati huo, inaelezwa timu za viongozi wa vyama hivyo vyenye wanachama na wafuasi wengi nchini, zimekuwa zikikutana kwa siri kubwa katika majadiliano ambayo yamekuwa na lengo la kuboresha mazingira ya kisiasa nchini.

Usiri wa vikao hivyo umekuwa ukitawala pande zote na taarifa zao zimekuwa zikifunikwa na zile za kikosi kazi kilichokuwa na jukumu la kupitia maoni ya wadau wa demokrasia ambacho ripoti yake ikiwa na masuala mbalimbali, imekabidhiwa hivi karibuni kwa Rais Samia.

Jana, vigogo wa CCM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti-Bara, Abdulrahman Kinana na upande wa Chadema, ukiongozwa na Mbowe waliongoza wajumbe wao kujifungia katika kikao hicho cha siri.

Kikao hicho, kilianza saa sita adhuhuri mchana na kukamilika 10:06 jioni katika hoteli hiyo.

Awali, kabla ya kuanza kwa kikao hicho, viongozi wa CCM walikuwa wa kwanza kuwasili wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge aliyewasili saa 5:14 asubuhi.

Saa 5:17 alifika Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai akiwa na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.

Gazeti hili lililokuwa limeweka kambi katika hoteli hiyo, lilimshuhudia Mbowe akiwasili saa 5:46 asubuhi akipishana dakika 11 na Kinana aliyefika saa 5:55 na wote walipoingia walikwenda moja kwa moja kwenye ukumbi wa Welington ambako kikao hicho kilifanyika.

Baada ya vigogo hao kuingia, saa 5:59 na saa 6:02 mchana, waliingia Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na John Heche mtawalia. Heche ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.

Saa 6:07 mchana, wanasheria wa Chadema, Jeremiah Mtobesya na Jonathan Mdeme nao waliingia katika kikao hicho.

“Huu ni mwendelezo wa vikao vyetu, ni nini kimejadiliwa, subirini muda ukifika mtaambiwa,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, ambaye hakutaka kuzungumza kwa undani.

Hata hivyo, taarifa ambazo gazeti hili linazo ni kwamba, majadiliano hayo yamefikia hatua nzuri na yatakapokamilika yatawekwa hadharani.

“Watu walijua baada ya kikosi kazi haya majadiliano hayapo, la hasha! Yanaendelea kama kawaida na sasa yapo hatua nzuri.”

“Mwisho Watanzania wataelezwa nini kinaendelea na bila shaka tutafanya mkutano na waandishi kwa pamoja,” alieleza kiongozi mmoja wa CCM ambaye si miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo.

“Mama kama alivyoahidi, anaendesha nchi kwa 4R, akiamini hiyo ndiyo njia ya kuwaleta wananchi pamoja. Nchi ni yetu sote na kila mmoja ana wajibu wa kuijenga.”

4R hizo ni (Reconcilation - maridhiano, Resiliency - ustahamilivu, Reforms -mabadiliko na Rebuilding - kujenga upya) ambazo alizielezea katika makala yake maalum aliyoandika kuadhimisha miaka 30 tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamud Shaka alipoulizwa na gazeti hili alisema hana uhakika kama kuna kikao hicho kwani, yeye si mjumbe wa vikao hivyo.

“ Lakini ninachojua kama wamekutana ni mwendelezo wa majadiliano na kama kimefanyika muda ukifika tutawajulisha.”

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa kuhusu kikao hicho hakuwa tayari kufafanua chochote zaidi ya kusema: “Aliyekwambia kuwa kuna kikao kimefanyika, atakuwa na uwezo wa kukueleza zaidi. Asante.”

Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, waliokuwa wa kwanza kutoka ndani ya ukumbi ni Mbowe na ujumbe wake ikiwa ni saa 10 jioni kisha wakafuatia Kinana na wenzake. Wakati wote wa kikao hicho ukiendelea, hali ya ulinzi ilikuwa wa kawaida na shughuli nyingine zilikuwa zikiendelea kama kawaida, huku magari ya viongozi hao yakijazana eneo la mapokezi.

MWANANCHI
 
Mawazo huru

"MBOWE anafanya kazi na ofisi kubwa KU push ajenda mwiba kwa kinyonga cha kijani,HASA kitabu kipya!

"Kijani wanapoza joto kwa ku buy time kwa vikao ILI warudishe ushawishi kwa wananchi wakijua kitabu kipya ni mwiba kwao""

"Mikutano ya Chadema ikiruhusiwa itafunika habari za kinyonga"

"Ile kesi ya covid-19 imekaa vibaya,wanamtaka hao covid-19 waendelee kubaki au wakitemwa wachaguliwe WENGINE ILI uhalali wa kisheria wa Bunge uwepo ILI lisipoteze uhalali kisheria kimataifa HASA kidemokrasia wasije pia kosa misaada na mikopo kutoka kwa wahisani"
 
Nini kinaendelea? Hili ni swali linalogonga vichwa vya Watanzania wengi wenye shauku ya kujua majadiliano baina ya viongozi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), yatahitimishwa lini.

Jana vigogo wa vyama hivyo wasiozidi 15 walijifungia kwa saa nne katika Hoteli ya Courtyard jijini hapa, kuendeleza majadiliano yaliyoanza miezi sita nyuma.

Majadiliano ya kwanza yalifanyika Ikulu ya Chamwino, Dodoma, Mei 20 mwaka huu kwa Rais Samia Suluhu Hassan akiambatana na viongozi waandamizi wa CCM na Serikali, ambao walikutana na ujumbe wa viongozi wa CHADEMA, ulioongozwa na Mwenyekiti wao, Freeman Mbowe.

======================

Tangu wakati huo, inaelezwa timu za viongozi wa vyama hivyo vyenye wanachama na wafuasi wengi nchini, zimekuwa zikikutana kwa siri kubwa katika majadiliano ambayo yamekuwa na lengo la kuboresha mazingira ya kisiasa nchini.

Usiri wa vikao hivyo umekuwa ukitawala pande zote na taarifa zao zimekuwa zikifunikwa na zile za kikosi kazi kilichokuwa na jukumu la kupitia maoni ya wadau wa demokrasia ambacho ripoti yake ikiwa na masuala mbalimbali, imekabidhiwa hivi karibuni kwa Rais Samia.

Jana, vigogo wa CCM wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti-Bara, Abdulrahman Kinana na upande wa Chadema, ukiongozwa na Mbowe waliongoza wajumbe wao kujifungia katika kikao hicho cha siri.

Kikao hicho, kilianza saa sita adhuhuri mchana na kukamilika 10:06 jioni katika hoteli hiyo.

Awali, kabla ya kuanza kwa kikao hicho, viongozi wa CCM walikuwa wa kwanza kuwasili wakiongozwa na aliyewahi kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Andrew Chenge aliyewasili saa 5:14 asubuhi.

Saa 5:17 alifika Naibu Katibu Mkuu wa zamani wa CCM-Zanzibar, Vuai Ali Vuai akiwa na baadhi ya viongozi wengine waandamizi wa chama hicho.

Gazeti hili lililokuwa limeweka kambi katika hoteli hiyo, lilimshuhudia Mbowe akiwasili saa 5:46 asubuhi akipishana dakika 11 na Kinana aliyefika saa 5:55 na wote walipoingia walikwenda moja kwa moja kwenye ukumbi wa Welington ambako kikao hicho kilifanyika.

Baada ya vigogo hao kuingia, saa 5:59 na saa 6:02 mchana, waliingia Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika na John Heche mtawalia. Heche ni mjumbe wa kamati kuu ya chama hicho.

Saa 6:07 mchana, wanasheria wa Chadema, Jeremiah Mtobesya na Jonathan Mdeme nao waliingia katika kikao hicho.

“Huu ni mwendelezo wa vikao vyetu, ni nini kimejadiliwa, subirini muda ukifika mtaambiwa,” alieleza mmoja wa wajumbe wa kikao hicho, ambaye hakutaka kuzungumza kwa undani.

Hata hivyo, taarifa ambazo gazeti hili linazo ni kwamba, majadiliano hayo yamefikia hatua nzuri na yatakapokamilika yatawekwa hadharani.

“Watu walijua baada ya kikosi kazi haya majadiliano hayapo, la hasha! Yanaendelea kama kawaida na sasa yapo hatua nzuri.”

“Mwisho Watanzania wataelezwa nini kinaendelea na bila shaka tutafanya mkutano na waandishi kwa pamoja,” alieleza kiongozi mmoja wa CCM ambaye si miongoni mwa wajumbe wa kamati hiyo.

“Mama kama alivyoahidi, anaendesha nchi kwa 4R, akiamini hiyo ndiyo njia ya kuwaleta wananchi pamoja. Nchi ni yetu sote na kila mmoja ana wajibu wa kuijenga.”

4R hizo ni (Reconcilation - maridhiano, Resiliency - ustahamilivu, Reforms -mabadiliko na Rebuilding - kujenga upya) ambazo alizielezea katika makala yake maalum aliyoandika kuadhimisha miaka 30 tangu kurejea kwa mfumo wa vyama vingi vya siasa nchini.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Shaka Hamud Shaka alipoulizwa na gazeti hili alisema hana uhakika kama kuna kikao hicho kwani, yeye si mjumbe wa vikao hivyo.

“ Lakini ninachojua kama wamekutana ni mwendelezo wa majadiliano na kama kimefanyika muda ukifika tutawajulisha.”

Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika alipoulizwa kuhusu kikao hicho hakuwa tayari kufafanua chochote zaidi ya kusema: “Aliyekwambia kuwa kuna kikao kimefanyika, atakuwa na uwezo wa kukueleza zaidi. Asante.”

Baada ya kumalizika kwa kikao hicho, waliokuwa wa kwanza kutoka ndani ya ukumbi ni Mbowe na ujumbe wake ikiwa ni saa 10 jioni kisha wakafuatia Kinana na wenzake. Wakati wote wa kikao hicho ukiendelea, hali ya ulinzi ilikuwa wa kawaida na shughuli nyingine zilikuwa zikiendelea kama kawaida, huku magari ya viongozi hao yakijazana eneo la mapokezi.

MWANANCHI
Kesi ya c19 imeshika pabaya, ukiwatoa c19 takwa la Kamati ya Fedha bungeni litaleta ukakasi ulaya.
 
Mamlaka inauliza CDM ikiwa COVID watatimuliwa, je watapeleka wabunge wapya?

Mikutano ndo imeanza hivyo baada ya CDM kustuka kuwa hapakuwa na Sheria yeyote ilowazuia kufanya mikutano.

Uwepo wa CHENGE ni kuthibitisha unabii juu ya kupatikana KATIBA mpya itokanayo na Rasimu alosimamia Judge WARIOBA by 2026.

Soon utamwona Mzee WARIOBA ndani ya Tume na mchakato ukianza.

Bt HORSE amenusa harufu ya.......mwaka ujao, tuendelee kuomba maana majirani hawatupendi na hawatotupokea kikinuka.
 
Ndio màana mazoezi kila kona!!
Kumbe wanajua!!
 
Back
Top Bottom