Elimu yetu ni ya nadharia sana, tuongeze vitendo katika taaluma

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
57,595
215,272
Tuna jinasibu kuwa uchumi wetu unategemea kilimo wakati kijana anaemaliza darasa la 12 au kidato cha nne hana ujuzi wowote wa kilimo unaomzidi alieishia darasa la saba. Wakati kijana huyu alisoma shule ya mchepuo wa kilimo.

Kama mwanafunzi wa kidato cha nne atapewa kipande cha ardhi, mfano miguu mitatu kwa mitatu. Wakati huo aina ya udongo wa eneo hilo umeshajulikana kitaalamu. Kwani tunaelewa kuwa ni muhimu kufahamu aina ya udongo kabla hujapanda mazao.

Kipande hiki, kitumiwe kama project ya kilimo ambayo itatathiminiwa na mwalimu wa kilimo na 20% ya project itaingia katika matokeo yake ya mtihani. Katika project atafute mazao yanayokubali aina ya udongo, achague zao moja. Ajifunze jinsi ya kuotesha mbegu, kuzisia, umbali wa shina mpaka shina, aina ya mbolea, aina ya magonjwa yanayosumbua zao lile.

Kwa muda wake ajue jinsi ya kutunza zao lile na aandike portfolio yenye picha. Katika portfolio mwanafunzi aeleze na changamoto alizopitia na kama kama anaweza kuchagua zao lile kuwa zao la kilimo katika maisha yake na ni kwanini. Mwalimu apange muda wa kutembelea projects, kuuliza maswali na kutoa ushauri.

Ninauhakika vijana wa kidato cha nne wanaweza kumaliza shule na elimu ya vitendo katika kilimo. Na wabiashara pia wanaweza kuandika business plan kutoka kidato cha nne.
 
shule za kilimo uliyaja yote haya, sasa wameua misingi mizuri hiyo
Ilitakiwa hii elimu ya vitendo ipewe umuhimu kwani 70% hawaendelei na elimu ya juu. Wakibaki mtaani wana hang kwani hawana skills and knowledge za maisha mengine.

Siku hizi wazazi wanawaanzisha watoto darasa la kwanza akiwa na miaka 5. Mtoto anafika miaka 15 amemaliza darasa la 12 yuko nyumbani hana issue.
 
Ikiwezekana mwalimu amkaribishe afisa kilimo kutoa mwongozo kwa wanafunzi.
 
Back
Top Bottom