Elimu yetu: Kuuza miili UDOM ni matokeo...

Elimu yetu: Kuuza miili UDOM ni matokeo...

MUSHI UDOM 08

Member
Joined
Apr 10, 2011
Posts
10
Reaction score
16
by Alex Nicholaus Thomas Mushi .

Kwa dhati ya moyo wangu nimesikitishwa sana na taarifa zilizozagaa kwenye vyombo vya habari kuhusu kujiuza kwa dada zetu wa UDOM. Wasomi ambao wana Dodoma na watanzania kwa ujumla walitegemea kujifunza kutoka kwao. Taarifa hizi zimenichochea kukaa chini na kuandika waraka huu huku nikizingatia ukweli kwamba UDOM ndipo nilikosomea masomo yangu ya shahada ya kwanza; mbali na matatizo yote yaliyonikumba katika safari hiyo ya kukamilisha shahada hiyo lakini nalazimika kusema kitu kwa faida yetu wote.

Ikumbukwa moja ya mategemeo ya jamii ya wana Dodoma kutoka kwenye chuo cha UDOM kilipo anzishwa mwaka 2007 ilikuwa ni kujionea jamii staarabu iliyoelimika na yenye kila sifa ya kuigwa, na pia jamii ya Dodoma ilitegemea watoto wao wangejionea namna wasomi hawa wanavyoishi kwa kusadifu kwa vitendo elimu, maadili na mila za nchi yao. Zaidi waliamini mambo hayo yangekuwa chachu ya kuwachochea vijana wao kuzingatia masomo ili na wao siku moja wafikie elimu hiyo ya Chuo lakini hali imekuwa tofauti kabisa. Leo jamii hii ya wana Dodoma wanashuhudia wasomi wanaoshinda mitaani wakiranda randa na nguo za kuogelea na za kulalia kana kwamba walikotoka hakuna wazazi, wanashuhudia wasomi wanaojiuza kama njugu.

Kiukweli siwezi hata siku moja kuruhusu kulea au kuipamba tabia hizo hata kama kuna sababu za msingi ambazo zinaweza zikawa zimesababisha tatizo hili kutokea. Kinachofanywa na dada zetu hawa ni kitendo ambacho kila mungwana anapaswa kukikemea kwa nguvu, na zaidi ya yote ni wajibu wetu wote kama vijana kurudia maadili yetu kama watanzania na kulaani kwa nguvu haya. Kama tutaruhusu tabia hii ikaota mizizi tutaandaa wasomi wasio waadilifu na wasio jiamini, tutandaa wasomi wenye shahada za kwenye chupi (nisamehewe kwa hiyo lugha lakini nimekosa neon linalokidhi ninachomaanisha),tutandaa wasomi walioathirika hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa, tutaandaa taifa la wavivu na wasifikiri kwa ufanisi.

Tukumbuke kuruhusu tabia hii kubobea ni kuruhusu kuporomoka kwa elimu ambayo ni msingi wa taifa lolote duniani. Na sidhani kama ni busara kuangalia umauti wa taifa letu kwa kuruhusu tabia hii kuota mizizi, kwani dhambi hiyo haitaishia chuoni tu, itaingia makazini na hapatakuwa na kazi zaidi ya uzinzi tu, baada ya hapo dhambi hii itasambaaa hadi kwa watoto na wajukuu wetu na hatimaye itakuwa ndio mfumo wetu wa maisha. Lakini mbali na yote niliyoeleza hapo juu ninayo yangu kwa serikali yangu, vijana hawa wa UDOM ni watoto wenu na wengine wameingia pale wakiwa hawana hata elimu ya kimaisha au ya kujitegemea, wengine wanakutana na kila aina ya tabia pale.

Mimi nilisha kuwa kiongozi wa mikopo UDOM-HSS kwa karibu miaka yote ya masomo yangu ya shahada ya kwanza, naelewa kiasi sababu na wakati dada zetu hawa wanapojiuza. Kipindi ambacho dada zetu hawa hujiuza huwa ni pale Bodi ya mikopo inapochelewesha mikopo ya wanafunzi, hali huwa mbaya kiasi dada zetu hawa ufika mahali wanalazimika kujidhalilisha ilimradi wapate chochote cha kujikimu. Na ukizingatia majumbani kwao hawa msaada wowote wanaoupata.

Mfano mzuri wa ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi wa kozi ya Uhusiano wa Kimataifa (BA IR) hawajapewa mikopo yao mpaka leo, na wanatakiwa kula, kunywa, kuwasiliana na kununua vitini vya masomo ili hali familia walizotoka ni masikini wa kutupwa. Haya yote ni mazingira hatarishi kwa dada zetu hawa. Serikali kama mzazi nakuomba mliangalie kwa umakini sana suala hili ili tuwaepushie wale wanajihusisha na tabia hii ya kuuza miili yao kutokana na kuishiwa au kukosa fedha za kujikimu Muda mwingine unaweza kusema serikali inafanya makusudi kuwacheleweshea mikopo yao wa sababu wanaonufaika sana na tabia hiyo ya dada zetu kujiuza ni wabunge wanapokuja kwenye vikao vyao vya bunge.

Kujiuza kwa dada zetu hawa ni dhahiri ni matokeo ya mambo kadhaa ambayo serikali haina budi kuyafuatilia kwa kina na hatimaye kutatua kwa ustawi wa tafa letu la Tanzania. Hatupaswi kufurahia tabia hii hata kidogo kwan kufanya hivyo kunaweza liathiri taifa letu kwa ujumla wake siku za usoni.

……………"ukiona panafuka moshi ujue kuna moto"…………
 
loan board wanaususika kwa asilimia 100, kuna watu hadi leo hawajawekewa hata sh sasa unategemea nn wakati na yeye anataka kuendelea kusoma
 
Hizo ndio faida za Sera ya uchangiaji wa Elimu ya JUU,na huo ni mwanzo mengi mtayaona subirini tu!
 
Hizi taarifa zinahitaji kufanyiwa utafiti zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo. Offcourse katika mkusanyiko mkubwa kama ilivyo katika vyuo vingine huwezi kukosa watu wenye tabia hizo.

Kuna kasumba ya wadada poa kujipaisha ili kuvutia wateja. Kinachofanyika ni hawa dada poa wa Dom kuwa hadaa wateja wao kuwa ni wanafunzi wa udom. Wateja wao nao bila kufanya kutafakari hujikuta wakiamini hivyo na habari kuendelea kusambaa. Wabongo kwa kuamini umbeya:
 
hawa dada zetu waache kujiendekeza, ufuska ni tabia ya mtu wanatakiwa pindi wapatapo mikopo itumike vizuri sio kwenda kufanya shopping za kushindana kimavazi na kununua simu kali siku mbili tatu pesa imeisha wanaaanza umalaya! Pia wapatapo likizo watafute part time job na kipato kiwasaidie walkati wanasubiria mikopo!na wazazi na ndugu wengine waangalie pia namna ya kusaidia maana hii bodi ya mikopo ipo jina tu!
 
Hapa JF sio mahali pa mzahamzaha mwana JF hebu toa mawazo ya kujenga jamii yetu na kuboresha maadili ya wana UDOM sio uingize mizaha yako hapa, sio mahali pake!
 
Hizi taarifa zinahitaji kufanyiwa utafiti zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo. Offcourse katika mkusanyiko mkubwa kama ilivyo katika vyuo vingine huwezi kukosa watu wenye tabia hizo.

Kuna kasumba ya wadada poa kujipaisha ili kuvutia wateja. Kinachofanyika ni hawa dada poa wa Dom kuwa hadaa wateja wao kuwa ni wanafunzi wa udom. Wateja wao nao bila kufanya kutafakari hujikuta wakiamini hivyo na habari kuendelea kusambaa. Wabongo kwa kuamini umbeya:
Mkuu kwa hiyo huamini!! Aisee!!Kuna kazi. Basi nenda Dodoma ukashuhudie kuingia na kutoka chuoni na mengine mengi!!
 
Hapa JF sio mahali pa mzahamzaha mwana JF hebu toa mawazo ya kujenga jamii yetu na kuboresha maadili ya wana UDOM sio uingize mizaha yako hapa, sio mahali pake!

Perception zako tu haina mzaa hata kidogo
 
Kila binadamu anatumia kiungo kimojawapo cha mwili wake ili kujipatia kipato chake ili aweze kuishi. Wapo wanaotumia akili zao kuuza katika soko na kujiapatia mahitaji yao.

Mfano wahasibu, wahandisi, wanasheria,madaktari orodha ni ndefu. Akili ni kiungo cha mwili kama kiungo kingine chochote. Waliojaliwa akili hawakujaliwa ukahaba. Lakini wapo waliojaliwa vipawa zaidi ya kimoja kama vile wenye jinsia mbili, huamua kutumia kimojawapo. Wapo wanaotumia miguu kucheza mpira au kukimbia au hata kuruka.

Hawa nao wanajipatia ujira utokanao na matumizi ya viungo vya miili yao kama atumiavyo kahaba kiungo chake. Wapo pia wanaotumia sauti zao kuimba na kuburudisha jamii kwa ujira wa kuuza kazi zao za sauti zao. Wapo wapiga mieleka, ngumi nk. Wote hawa tunasema wanatumia vipawa vyao kujiendeleza kwa faida yao.

Katika uchumi wa kiliberali chochote kinauzika na kunulika.Hawa dada zetu makahaba wanatumia viungo vya miili yao kama wanavyotumia watu wengine kuuza na kujipatia ujira. Katika soko kuna kuuza vitu (products)na huduma(service) Huduma ni kama benki, bima, hoteli ngono nk.

Uhuru tulipata mwaka 1961, wacha watu wawe huru kufanya walitakalo maadamu hawavunji sheria. Tabia ya mtu hutembea nayo popote anapoenda. Kama mtu ana tabia ya ukahaba (mjasiriamali wa ukahaba) hawezi kuiacha kwa sababu tu anasoma Chuo kikuu. Ni kama mtu mwingine yeyote anayeweza kuzungukwa na rasilimali nyingi lakini anashindwa kuzibadilisha kuwa vitega uchumi.

An Enterprenuer is the one who sees the opportunity that others don't see
 
Nadhani hili linavisu vyuo vyote sema tu vyombo vya habari havijaamua kufuatilia kwa karibu kama ilivyofanya UDOM
 
They always think with their vaginas NOT their Head
Samahani wadau sijaelewa vizuri mambo kadha wa kadha.
Hivi UDOM ni chuo cha vijana wa kike pekee.
Je bodi ya mikopo hufanya upendeleo kuchelewesha mikopo ya wanafunzi wa kike ilhali wale wa kiume inafika kwa wakati?
Je wanafunzi wa kiume wao pia wanajiuza kutoa 0713 ili kujikimu au wanafanyaje!
Yaweza ikawa kusoma chuo kikuu ni sawa na kuvuta bange.
Nisaidieni kupata majibu ili nami nitoe mchango wangu wa maoni.
 
Nadhani hili linavisu vyuo vyote sema tu vyombo vya habari havijaamua kufuatilia kwa karibu kama ilivyofanya UDOM

It is much wiser to walk away in silence then to speak the negative words in and on your mind. Once you unleash your words from out of your mouth, you cannot retract them, nor prevent them from entering into another set of ears. The process of your perception is already in motion. Use your wisdom to be the lever that gives stability to your humble attitude.
 
Hizi taarifa zinahitaji kufanyiwa utafiti zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo. Offcourse katika mkusanyiko mkubwa kama ilivyo katika vyuo vingine huwezi kukosa watu wenye tabia hizo.

Kuna kasumba ya wadada poa kujipaisha ili kuvutia wateja. Kinachofanyika ni hawa dada poa wa Dom kuwa hadaa wateja wao kuwa ni wanafunzi wa udom. Wateja wao nao bila kufanya kutafakari hujikuta wakiamini hivyo na habari kuendelea kusambaa. Wabongo kwa kuamini umbeya:

Uko sahihi kabisa. Mtaani watu wanaperception kuwa akijiita mwanafunzi anaonekana yupo juu. Kozi kuna watu nilikuwa nakaa nao nearby chuo nao walikuwa wanajiita wanafunzi. Sual la dada zetu lipo but not to that extend.
 
Sikubali na mleta mada, kuwa lawama zote ni kwa bodi ya mikopo(HESLB)..Kama msomi tusaidie;
-Unanadhani ni wanafunzi wangapi wanapokea mikopo?
-Ni chuo cha Dodoma(UDOM) pekee ambapo wanafunzi huishiwa pesa?
-Ni wanafunzi wa kike tu ndio husumbuliwa na shida hii?

Ni kweli kuna baadhi ya wanafunzi kweli wanatumia kiasi fulani cha pesa ya mkopo kusaidia familia na shughuli nyinginezo kama hizo lakini si wote.

Wimbi kubwa la wanafunzi (hasa wa kike) ni ushuhuda tosha wa matumizi mabaya ya pesa hizo, mf. matumizi ya starehe, saluni, vitu vya thamani kama simu, n.k kuendana na wakati..i can tell you ni kweli ni mkopo 7500/=Tshs kwa siku na japo inaonekana "ndogo" kwa wanafunzi hebu wapatie hapa "uswahili kwetu" uone matumizi yatakavyopangwa.

Sidhani, kama wanafunzi wote wenye "kuishiwa pesa" huwa wanajiuza!Hebu tujiuliza hata katika nchi nyingine wanfunzi wa chuo huishi na kujikimu kwa njia zipi za kimaadili, mf. mzuri ni hapo Nairobi, Kenya..baadhi hufanya part time jobskatika migahawa, hoteli n.k
Je, ni watoto wetu wa kike wangapi, wana uthubutu huu?
Wengi huingia katika tabia hii(escort) kwa mkumbo, na makundi (mf. UDSM, SAUT, n.k)

Ninaamini kwa mwanafunzi wa chuo(wa kozi yeyote ile) unaweza kutafuta kujikimu kwa njia yeyote ile lakini si ya kutouthamini utu(dignity) wako.
 
Mkuu MUSHI UDOM 08 , makala yako imegusa moja tu ya sababu (tena isiyo na nguvu) juu ya sababu ya wadada kujiuza miili yao. Sababu ni nyingi mno, hizo lawama umezitupia sehem moja ni half the truth.

Wadada wa vyuo vya Tanzania (naamini hata vyuo vingine) sababu yao ya kujiuza mara nyingi hufanana. Na miaka ya karibuni kasi ni kubwa sana ukifananisha na miaka ya nyuma... Labda ndio mana sasa hivi ina make headlines.
 
Hizi taarifa zinahitaji kufanyiwa utafiti zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo. Offcourse katika mkusanyiko mkubwa kama ilivyo katika vyuo vingine huwezi kukosa watu wenye tabia hizo.

Kuna kasumba ya wadada poa kujipaisha ili kuvutia wateja. Kinachofanyika ni hawa dada poa wa Dom kuwa hadaa wateja wao kuwa ni wanafunzi wa udom. Wateja wao nao bila kufanya kutafakari hujikuta wakiamini hivyo na habari kuendelea kusambaa. Wabongo kwa kuamini umbeya:

Ili kukubalika huwa wanajipa hadhi ya jamii nyingine,ndio maana wengi wakitongozwa husema eti mimi nipo chuo.!!,huwa hawataji chuo gani mpaka umuulize mara ya pili ndipo atakuwambia nipo chuo fulani tena mwaka wa kwanza au wa pili.!!!
 
Mkuu kwa hiyo huamini!! Aisee!!Kuna kazi. Basi nenda Dodoma ukashuhudie kuingia na kutoka chuoni na mengine mengi!!
Hii mada tulishaichangia sana humu, mm nakaa Dodoma na UDOM nafika hizi habari ni za UONGO hasa kwa mtu ambaye hajapitia katika Elimu ya Vyuo au kupitia JKT ndio maana anakitaja Chuo hiki
Mji huu wengi wa wasichana sasa hivi wanavaa hizo nguo za ajabu ajabu (vimini, skin tight /Jeans), ila siku wanarudi makwao ndipo utakapogundua wanavaa kiheshima
. Kwa hiyo usishangae kukutana nao njiani wamevaa kiajabu lakini sio ukimsimamisha anakubali kwa bei yoyote (buku 5)
Hivi Mwanachuo ana paper asubuhi aache kusoma aje mjini kufanya ufuska sijawaona ila nimesikia hukokwenye mabweni yao ambako ni Vyuo vingi tu hufanya hivyo
Baada ya migomo ambayo iliisha mwaka jana kuna masharti walipewa ambayo ilikuwa kutokuvaa nguo hizo, kufuga rasta nk na kweli walitulia mpaka Chuo kikawa kichungu
Kwa sasa medicine wanakaa College ya education na wanafanya kwenda chuoni kwao na kurudi. Isipokuwa kwa mwaka wa kwanza watakaa college kwao. Kuhusu mavazi mara nyingi huwa wanayo aina fulani ya sare yao. Kabla ya kuchanganywa hapo Education, walikuwa hawaruhusiwi kuvaa mapensi, jinsi, vimini, cap(kofia za chepeo) Manguo ya ajabu ajabu yalipigwa marufuku kwao toka zamani. Katika College walikokuwa wanafuatiliwa ni wao na nadhani ni kwa sababu ya maadili ya kazi zao. Uchache wao pia ulikwa unachangia kwani niliwahi kuambiwa na mtu anaesoma College hiyo kuwa hata uzururaji mjini hawakuruhusiwa, ila ni kwa taarifa maalum. Kama yupo mtu humu Jf anasoma medicine atatupa ukweli. 7. (kwa wanaokwenda social science) Chagua mavazi ya heshima kwani ukidhani unakwenda kujiachia unawezaukajikuta unarudi nyumbani siku hiyo hiyo, Kwa wanadada, vimini, suruali za kubana, nguo za ajabu ajabu waachie wadogo zako. Kama huna za kushonesha anza kuzitafuta. Kwa wanakaka, punguza idadi ya majinzi
( Hasa kwa
wanaokwenda social science), mitindo ya kata K, kusuka nywele, kuvaa heleni potezea kwenu.
, Nasikitika kuwaelezea vijana kwamba yale mavazi yetu na magwanda yetu tunayapenda saaaaaaaanaaa, ila dah, naogopa kusema kwamba tuyapumzishe tu nymbani, kwani hali ni mbaya sana. Ushabiki wa vyama vya siasa (Hasa vidole viwili) kwa Chuo chenu ni utata. Hata hivyo nisikukatisheni tamaa kwani hatujui mazingira yatakuwaje. We have to be situational sometimes
 
Ni combination of factors the foremost ikiwa ni matokeo ya kusupport sera za chama mfilisi Ccm. Wale wanafunzi wanatakiwa kusoma bure na kulipwa allowances zao in time, other reasons include utamu wa tendo lenyewe na maisha ya kuiga iga ya wadogo zetu.!
 
loan board wanaususika kwa asilimia 100, kuna watu hadi leo hawajawekewa hata sh sasa unategemea nn wakati na yeye anataka kuendelea kusoma

Kichwa kizidi kuniuma kwa kuwaza jambo hili. Kama wanachuo wa jinsi ya kike wametumia uke wao kukamilisha mahitaji yao ya kimasomo pindi wawapo chuoni. Swali gumu lisilo na majibu ya moja kwa moja kutoka kwangu, je wa jinsi ya kiume watatumia mbinu gani ili waendelee na elimu?

Kwa kuwa za akina dada hazibanduki hivyo mteja anapaswa kutumia na kuiacha kwa ajili ya mteja mwingine, je wa jinsi ya kiume wataweza kutoa walichonacho ili wapate fedha?

Maswali ni mengi ila ili ni bomu litakalolipuka muda na wakati usiojulikana.
 
Back
Top Bottom