hawa dada zetu waache kujiendekeza, ufuska ni tabia ya mtu wanatakiwa pindi wapatapo mikopo itumike vizuri sio kwenda kufanya shopping za kushindana kimavazi na kununua simu kali siku mbili tatu pesa imeisha wanaaanza umalaya! Pia wapatapo likizo watafute part time job na kipato kiwasaidie walkati wanasubiria mikopo!na wazazi na ndugu wengine waangalie pia namna ya kusaidia maana hii bodi ya mikopo ipo jina tu!
Hizi taarifa zinahitaji kufanyiwa utafiti zaidi ili kujua ukubwa wa tatizo. Offcourse katika mkusanyiko mkubwa kama ilivyo katika vyuo vingine huwezi kukosa watu wenye tabia hizo.
Kuna kasumba ya wadada poa kujipaisha ili kuvutia wateja. Kinachofanyika ni hawa dada poa wa Dom kuwa hadaa wateja wao kuwa ni wanafunzi wa udom. Wateja wao nao bila kufanya kutafakari hujikuta wakiamini hivyo na habari kuendelea kusambaa. Wabongo kwa kuamini umbeya:
nakubaliana na wewe hasa inapokuwa 'out of will' kwa kuchagua, ndiyo kila mmoja anatumia chake lakini kwa hawa hapana:waliamua kutumia akili lakini serikali na bodi ya mikopo zinawafanya watumie 'uchi' bila kupenda. Lazima tuichukie CCM kwavitendo na tuikatae hata kwa kura 2015.
kama wanafanya kwa hamu kama wewe unavyodhani mkuu sidhani kama ni tatizo kubwa kama unavyofikiri,WANAJIUZA ili wapate chochote kitu,sasa sijui mtu anaweza kujiuza kwa ajili ya erection tu.
Ni kweli kuna tatizo la mikopo.Ama mikopo haitoshi ama inachelewa kutolewa, lakini si wote wanatumia karama hii ya biashara ya ngono. Hii ni hulka ya mtu ama upeo wake wa kufikiria biashara gani atumie kutatua matatizo haya, akaona biashara rahisi ni ngono. Si watu wote hutumia njia moja kutatua tatizo la aina ileile. Tatizo la mikopo liko vyuo vyote vya Tanzania, lakini tatizo la biashara ya ngono inasemekana kuwa kubwa UDOM. Nadhani iko haja ya kufikiri zaidi ya mikopo na Bodi ya mikopo.
Nasisitiza kuwa hii ni hulka ya mtu. Wapo watu wametumia mbinu hii kujineemesha maisha hata bila ya tatizo la mikopo. Wapo wanafunzi wamefaulu kozi zao kwa kupatiwa misaada na wakufunzi kwa mtaji huu huu, wapo waliojengewa nyumba nzuri kuliko baadhi yanyumba za watumishi, wapo waliopandishwa vyeo kwa mtaji huu huu. Kuna watu familia zao zimeyumba sababu ya biashara hii. Tusilione tatizo hili kwa juu juu. Hawa watu wazima waliofanikisha mambo ya kwa njia hii walianza wakiwa umri sawa na wa waliovyuoni sasa. Mbinu iliyomsaidia mtu kufikia mafanikio fulani hataicha maishani. Jamii corrupt huzaa watoto corrupt. Yawezekana wanafunzi wanaojiuza wanatoka katika familia ambazo ama mama anajiuza, ama amepora mume wa mtu ama mama kapata cheo kwa njia ya upendeleo ama baba anahangaika na changu doa ametelekeza familia yake. Fanyeni utafiti zaidi ya kufikiria mikopo na bodi ya mikopo.
by Alex Nicholaus Thomas Mushi .
Kwa dhati ya moyo wangu nimesikitishwa sana na taarifa zilizozagaa kwenye vyombo vya habari kuhusu kujiuza kwa dada zetu wa UDOM. Wasomi ambao wana Dodoma na watanzania kwa ujumla walitegemea kujifunza kutoka kwao. Taarifa hizi zimenichochea kukaa chini na kuandika waraka huu huku nikizingatia ukweli kwamba UDOM ndipo nilikosomea masomo yangu ya shahada ya kwanza; mbali na matatizo yote yaliyonikumba katika safari hiyo ya kukamilisha shahada hiyo lakini nalazimika kusema kitu kwa faida yetu wote.
Ikumbukwa moja ya mategemeo ya jamii ya wana Dodoma kutoka kwenye chuo cha UDOM kilipo anzishwa mwaka 2007 ilikuwa ni kujionea jamii staarabu iliyoelimika na yenye kila sifa ya kuigwa, na pia jamii ya Dodoma ilitegemea watoto wao wangejionea namna wasomi hawa wanavyoishi kwa kusadifu kwa vitendo elimu, maadili na mila za nchi yao. Zaidi waliamini mambo hayo yangekuwa chachu ya kuwachochea vijana wao kuzingatia masomo ili na wao siku moja wafikie elimu hiyo ya Chuo lakini hali imekuwa tofauti kabisa. Leo jamii hii ya wana Dodoma wanashuhudia wasomi wanaoshinda mitaani wakiranda randa na nguo za kuogelea na za kulalia kana kwamba walikotoka hakuna wazazi, wanashuhudia wasomi wanaojiuza kama njugu.
Kiukweli siwezi hata siku moja kuruhusu kulea au kuipamba tabia hizo hata kama kuna sababu za msingi ambazo zinaweza zikawa zimesababisha tatizo hili kutokea. Kinachofanywa na dada zetu hawa ni kitendo ambacho kila mungwana anapaswa kukikemea kwa nguvu, na zaidi ya yote ni wajibu wetu wote kama vijana kurudia maadili yetu kama watanzania na kulaani kwa nguvu haya. Kama tutaruhusu tabia hii ikaota mizizi tutaandaa wasomi wasio waadilifu na wasio jiamini, tutandaa wasomi wenye shahada za kwenye chupi (nisamehewe kwa hiyo lugha lakini nimekosa neon linalokidhi ninachomaanisha),tutandaa wasomi walioathirika hivyo kupoteza nguvu kazi ya taifa, tutaandaa taifa la wavivu na wasifikiri kwa ufanisi.
Tukumbuke kuruhusu tabia hii kubobea ni kuruhusu kuporomoka kwa elimu ambayo ni msingi wa taifa lolote duniani. Na sidhani kama ni busara kuangalia umauti wa taifa letu kwa kuruhusu tabia hii kuota mizizi, kwani dhambi hiyo haitaishia chuoni tu, itaingia makazini na hapatakuwa na kazi zaidi ya uzinzi tu, baada ya hapo dhambi hii itasambaaa hadi kwa watoto na wajukuu wetu na hatimaye itakuwa ndio mfumo wetu wa maisha. Lakini mbali na yote niliyoeleza hapo juu ninayo yangu kwa serikali yangu, vijana hawa wa UDOM ni watoto wenu na wengine wameingia pale wakiwa hawana hata elimu ya kimaisha au ya kujitegemea, wengine wanakutana na kila aina ya tabia pale.
Mimi nilisha kuwa kiongozi wa mikopo UDOM-HSS kwa karibu miaka yote ya masomo yangu ya shahada ya kwanza, naelewa kiasi sababu na wakati dada zetu hawa wanapojiuza. Kipindi ambacho dada zetu hawa hujiuza huwa ni pale Bodi ya mikopo inapochelewesha mikopo ya wanafunzi, hali huwa mbaya kiasi dada zetu hawa ufika mahali wanalazimika kujidhalilisha ilimradi wapate chochote cha kujikimu. Na ukizingatia majumbani kwao hawa msaada wowote wanaoupata.
Mfano mzuri wa ucheleweshaji wa mikopo kwa wanafunzi wa kozi ya Uhusiano wa Kimataifa (BA IR) hawajapewa mikopo yao mpaka leo, na wanatakiwa kula, kunywa, kuwasiliana na kununua vitini vya masomo ili hali familia walizotoka ni masikini wa kutupwa. Haya yote ni mazingira hatarishi kwa dada zetu hawa. Serikali kama mzazi nakuomba mliangalie kwa umakini sana suala hili ili tuwaepushie wale wanajihusisha na tabia hii ya kuuza miili yao kutokana na kuishiwa au kukosa fedha za kujikimu Muda mwingine unaweza kusema serikali inafanya makusudi kuwacheleweshea mikopo yao wa sababu wanaonufaika sana na tabia hiyo ya dada zetu kujiuza ni wabunge wanapokuja kwenye vikao vyao vya bunge.
Kujiuza kwa dada zetu hawa ni dhahiri ni matokeo ya mambo kadhaa ambayo serikali haina budi kuyafuatilia kwa kina na hatimaye kutatua kwa ustawi wa tafa letu la Tanzania. Hatupaswi kufurahia tabia hii hata kidogo kwan kufanya hivyo kunaweza liathiri taifa letu kwa ujumla wake siku za usoni.
ukiona panafuka moshi ujue kuna moto
Mmhh apa sijakuelewa,ulitaka kusema nini vile.!?Juu ya hili hata chuo hiki kikiitwa Kikwete University roho yangu itakuwa nyeupe kama theluji.

Kila binadamu anatumia kiungo kimojawapo cha mwili wake ili kujipatia kipato chake ili aweze kuishi. Wapo wanaotumia akili zao kuuza katika soko na kujiapatia mahitaji yao.
Mfano wahasibu, wahandisi, wanasheria,madaktari orodha ni ndefu. Akili ni kiungo cha mwili kama kiungo kingine chochote. Waliojaliwa akili hawakujaliwa ukahaba. Lakini wapo waliojaliwa vipawa zaidi ya kimoja kama vile wenye jinsia mbili, huamua kutumia kimojawapo. Wapo wanaotumia miguu kucheza mpira au kukimbia au hata kuruka.
Hawa nao wanajipatia ujira utokanao na matumizi ya viungo vya miili yao kama atumiavyo kahaba kiungo chake. Wapo pia wanaotumia sauti zao kuimba na kuburudisha jamii kwa ujira wa kuuza kazi zao za sauti zao. Wapo wapiga mieleka, ngumi nk. Wote hawa tunasema wanatumia vipawa vyao kujiendeleza kwa faida yao.
Katika uchumi wa kiliberali chochote kinauzika na kunulika.Hawa dada zetu makahaba wanatumia viungo vya miili yao kama wanavyotumia watu wengine kuuza na kujipatia ujira. Katika soko kuna kuuza vitu (products)na huduma(service) Huduma ni kama benki, bima, hoteli ngono nk.
Uhuru tulipata mwaka 1961, wacha watu wawe huru kufanya walitakalo maadamu hawavunji sheria. Tabia ya mtu hutembea nayo popote anapoenda. Kama mtu ana tabia ya ukahaba (mjasiriamali wa ukahaba) hawezi kuiacha kwa sababu tu anasoma Chuo kikuu. Ni kama mtu mwingine yeyote anayeweza kuzungukwa na rasilimali nyingi lakini anashindwa kuzibadilisha kuwa vitega uchumi.
An Enterprenuer is the one who sees the opportunity that others don't see