Elimu ya vyuo Tanzania ni duni - Hakuna mkazo

Candid Scope

JF-Expert Member
Nov 8, 2010
11,883
6,884
Elimu ya vyuo Tanzania ni chini kutokana na kutokuwa na msukumo wa wanachuo uwepo madarasani. Mwanachuo aingie darasani au asiingie haiathiri cho chote kwa vyuo vya Tanzania.

Vyuo vya baadhi ya nchi mwanachuo akikosa kipindi kimoja lazima ajazie na kupewa onyo. Akikosekana maratatu na zaidi anaachishwa chuo. Je hili lipo bongo?
 
Peleka kwenye jukwaa husika plz................your JF senior expert member,shame to you!!!!
 
Darasani hawaingii, mbaya zaidi most of th time wanashinda kwenye migomo., unategemea nini?
Elimu Vyuo Tanzania ver ver poor :rip::rip:
 
Elimu ya vyuo Tanzania ni chini kutokana na kutokuwa na msukumo wa wanachuo uwepo madarasani. Mwanachuo aingie darasani au asiingie haiathiri cho chote kwa vyuo vya Tanzania.

Vyuo vya baadhi ya nchi mwanachuo akikosa kipindi kimoja lazima ajazie na kupewa onyo. Akikosekana maratatu na zaidi anaachishwa chuo. Je hili lipo bongo?

Naona KIU wanakuja vizuri. Wako strict kwenye suala la kuhudhuria darasani. Ukikosa zaidi ya mara tatu imekula kwako. Kila mwanafunzi anasaini kuhakikisha ameingia darasani. Na wanasema bila kuwa strict then hawata-achieve malengo waliyojiwekea.
 
Nilitaka tu wengi waone kisha tuihamishe.

Ni kweli wengi wetu ukiacha MMS,tupokwenye siasa, lakini hii haimaanishi kwamba ikiwa kwenye jukwaa husika basi watu hawaiona hii post yako..la hasha, tutaiona na ndio maana kukawa na majukwaa tofauti, so usipate shida kupost kitu kwenye jukwaa husika,coz mtu mwingine anapenda siasa na mara nyingi anaingia direct kwenye jukwaa,sasa akikuta baadhi ya mambo hayahusiani na siasa inakuwa kama unamkwaza..na ndio maana mchangiaji wa kwanza kawa ''mbogo''.

Back to the point ni kwamba elimu ya chuo hapa bongo haina vikwazo/restriction kwa wanafunzi,wale wanafunzi wanapotoka form 6(kumbuka wengi wao huwa wanazurura sana huku na huko kwenye matushion,wengine shule ndo hawaonekani kabisa coz of tusheni) sasa hali hii wakifaulu ndio wanajua njia bora ya kusoma. Darasa kwao ni kaa la moto,wanakuwa mtaani kutafuta life na mengineyo, isitoshe (sina hakika) mavyuoni sidhani kama kuna attendance kwa wanafunzi baada ya kipindi. Attendance ndio suluhisho la hii kitu. Attndc chini ya 75 percent huruhisi kufanya mtihani wa semister, na vilevile attndc intakuwa na some marks kwenye zile internal examz,hii ingekuwa imewashika madent wengi watoro-watoro!!
 
Naona KIU wanakuja vizuri. Wako strict kwenye suala la kuhudhuria darasani. Ukikosa zaidi ya mara tatu imekula kwako. Kila mwanafunzi anasaini kuhakikisha ameingia darasani. Na wanasema bila kuwa strict then hawata-achieve malengo waliyojiwekea.

Issue siyo kuingia darasani ila kimbembe chake utakachokipata kwa kujisomea mwenyewe. Shule za wenzetu (developed countries)siyo mwalimu tu kufika mbele anatowa lecture kuna mda wa kujadili issues ambayo unapunguza mzigo wa kujichimbia mwenyewe. Wanakuwa makini na kukomalia hivyo kwa sababu siyo yote yaliyo kwenye kitabu au hand-out tu ndo unatakiwa kusoma na kuelewa. Lucturer atatoa mifano mingi kutokana na mazingira yaliyopo mda huo ambayo itakufanya wewe mwanafunzi kuelewa topics na issues bila kusahau mapema. Siyo mambo ya madesa tena kwa wenzetu, hivyo lazima kuwepo darasani.
 
Naungana na mtoa hoja hapo juu.
Uduni wa elimu haupimwi kwa kuingia darasani peke yake. Unaanzia kwa uwezo wa waalimu wetu. Wengi wa waalimu wetu km ilivyo wanafunzi bado kwetu reference ni zile za miaka mingi iliyopita wakati wenzetu wanakwenda na kasi karibu kila mwaka editions zinabadilika ili kuweza kuchukua mabadiliko yanayotokea kwenye dunia.
Maabara zetu ni duni saaana. Kuna vitabu vichache hasa vile wanafunzi wanavyovihitaji.
Madarasani wanafunzi wamejazana. Ratio ya mwalimu na wanafunzi inasikitisha.
Syllabus nyingi ni copy na paste, hazibadiliki kuweza kumeza uhalisia.
Wanafunzi hawasomi vitabu in most cases. Kuna baadhi ya vyuo anasoma vislide viwili vitatu anataka akafanye mtihani na awe competent kwenye somo husika. Wengine kwao ni madesa tokea 70's, watu wanasoma maswali yaleyale na walimu huwa wanarudufu maswali.
Waalimu hawana muda wa consultations na wanafunzi. Wakimaliza darasani na kazi imeisha.
Wanafunzi wengi wa vyuo, wakiambiwa waandike kitu kidogo tu, hata persona; profile utajua-hii inamaanisha hata juhudi binafsi nazo ni tete. Na mengineyo mengi............................... ndio maana nchi maskini.
 
St joseph collage of eng huna attendance ya 85% hufanyi module exams na end exams'wanakufuta kabsa chuo so kila siku lazma uwe chuo'
 
Elimu ya vyuo Tanzania ni chini kutokana na kutokuwa na msukumo wa wanachuo uwepo madarasani. Mwanachuo aingie darasani au asiingie haiathiri cho chote kwa vyuo vya Tanzania.

Vyuo vya baadhi ya nchi mwanachuo akikosa kipindi kimoja lazima ajazie na kupewa onyo. Akikosekana maratatu na zaidi anaachishwa chuo. Je hili lipo bongo?

Hoja hii haina nguvu za kuhalalisha elimu dhoofu hapa Bongo! Maana hata nje ya nchi, tabia ya mahudhurio haina tofauti sana na hapa kwetu. .
 
Naona KIU wanakuja vizuri. Wako strict kwenye suala la kuhudhuria darasani. Ukikosa zaidi ya mara tatu imekula kwako. Kila mwanafunzi anasaini kuhakikisha ameingia darasani. Na wanasema bila kuwa strict then hawata-achieve malengo waliyojiwekea.

Issue siyo kuingia darasani ila kimbembe chake utakachokipata kwa kujisomea mwenyewe. Shule za wenzetu (developed countries)siyo mwalimu tu kufika mbele anatowa lecture kuna mda wa kujadili issues ambayo unapunguza mzigo wa kujichimbia mwenyewe. Wanakuwa makini na kukomalia hivyo kwa sababu siyo yote yaliyo kwenye kitabu au hand-out tu ndo unatakiwa kusoma na kuelewa. Lucturer atatoa mifano mingi kutokana na mazingira yaliyopo mda huo ambayo itakufanya wewe mwanafunzi kuelewa topics na issues bila kusahau mapema. Siyo mambo ya madesa tena kwa wenzetu, hivyo lazima kuwepo darasani.

Hiyo pia inafanyika KIU, amini usiamini. Najua wengi wanakishambulia kama chuo cha kata.
 
In either way, elimu yetu ni duni. Hivi ni wangapi wanamaliza vyuo vikuu hawajui kutumia computer? Watu wanaweza kulipuuza hili lakini reference nyingi zipo mtandaoni kuliko hata kwenye vitabu. Wengi wakijitahidi ni internet labda na Ms word. Teknolojia ipo nyuma.
 
Wachangiaji wote mna mawazo mgando.
Kuingia darasani kila siku siyo kufaulu, na mwanachuo ni mtu mzima, no need to control them, wao wanaelewa.
 
Wachangiaji wote enh!! Wewe pia ni muathirika wa mfumo mbaya wa elimu maana huwezi hata kusoma walichoandika watu hapo juu
 
Naona KIU wanakuja vizuri. Wako strict kwenye suala la kuhudhuria darasani. Ukikosa zaidi ya mara tatu imekula kwako. Kila mwanafunzi anasaini kuhakikisha ameingia darasani. Na wanasema bila kuwa strict then hawata-achieve malengo waliyojiwekea.

Hata pale UDBS kwenye madarasa ya masters walim wengi huwa wanachukua attendence, na usipoatend lectures you are ineligible ufanya mtihani!
 
Elimu ya vyuo Tanzania ni chini kutokana na kutokuwa na msukumo wa wanachuo uwepo madarasani. Mwanachuo aingie darasani au asiingie haiathiri cho chote kwa vyuo vya Tanzania.

Vyuo vya baadhi ya nchi mwanachuo akikosa kipindi kimoja lazima ajazie na kupewa onyo. Akikosekana maratatu na zaidi anaachishwa chuo. Je hili lipo bongo?

Ni kivumbi......... lecturer mwenyewe hana ratiba maalumu ya kuingia.... japo ratiba imebandikwa. Na asipokuja hatoi taarifa........... Kila kitu tia tia maji mwisho wa semester.... Nani wa kumshikia mwingine kengele.

Mtu wa ku-establish kwamba mwanafunzi hajaaingia darasani mara tatu ni lecturer husika ambae nae hana ratiba maalum za kuingia darasani. Ni full kivumbi..............
 
<br />
<br />
udbs na ile master isiyo na tofauti na bcom enh!
 
Vyuo vingi vina sheria inayodhibiti attendence za wanafunzi lakini hakuna ufuatiliaji! Cha muhimi watu wanatakiwa waelewe kilichowapeleka shule kazi huanza pale wanafunzi wa aina hiyo wanapoingia kwenye sokol la ajira
 
Back
Top Bottom