Ngoda, unatakiwa kufahamu yafuatayo:
- Elimu ya uraia ni uelewa na maarifa ya raia juu ya haki na wajibu wa raia vis-a-vis mamlaka za utawala. uelewa na maarifa ya umma hayana mipaka na hayamilikiwi na mtu au kundi lolote; serikali ni mojawapo ya makundi maslahi katika suala la elimu ya uraia hivyo haiwezi kuaminiwa kumiliki elimu ya uraia.
- Kutokana na hadhi na umuhimu wake, elimu ya uraia haimilikiwi na wala haiwezi kudaiwa kumilikiwa na mtu, kundi la watu wala chanzo chake; kudai kilichomo ndani ya waraka uliotolewa na wakatoliki mawazo ya wakatoliki kwa manufaa ya wakatoliki weneyewe, hivyo kila kundi au mtu anaweza kutoa 'elimu yake ya uraia' ni ama upotoshaji wa makusudi au ishara kuwa na uelewa ndogo kuhusu hoja/suala husika.
- Tangu mwaka 1990 serikali imeonyesha kutokuwa na nia ya kutoa elimu ya uraia, ikihofia kuondolewa madarakani; hivyo kutaka serikali ihodhi ukiritimba wa kutoa elimu ya uraia ni sawa na raia kudai waendelee (kushangilia) kuongozwa na mafisadi.
- Ki-msingi, kuendelea kushamili kwa ufisadi katika uongozi wa umma ni kutokana na uduni wa kiwango cha elimu ya uraia miongoni mwa watanzania na wananchi wa kawaida walio wengi.
- Je, unataka ufisadi uendelee?
- Kugawanyika kwa wananchi baina ya kundi linalosimamia kulinda maslahi ya umma na kundi pinzani dhidi ya hilo, tofauti na mawazo ya akina Kingunge, ni jambo la kheri kwa manufaa ya maendeleo ya Tanzania; nani yuko kundi la akina Kingunge Ngombara Mwiru?
Mkuu maelezo yako mazuri sana na umekita pale panapotakiwa haswaaa!..
Hakika mada hii ni muhimu sana kwetu sisi wote na ningeomba kila mmoja wetu achangie mada hii kuhusiana na ELIMU ya URAIA, kwani a lot is at stake 2010 na huko tuendako..
Kwanza kabisa nitasema kuwa Elimu ya Uraia inatanguliwa na mfumo mzima unaowaongoza wananchi (raia) na utawala (serikali) itakayoongoza - hakuna mwenye madaraka wala nguvu ya tunga elimu hiyo ila elimu hiyo inakuwepo tayari kwa wote wahusika..Hivyo somo zima linajijenga kama masomo mengine ya elimu kisayansi kukiwa na imani tofauti zinazopingana.
Kwa mfano mwalimu wa Chemistry hufundisha kile ambacho tayari kimekwisha gunduliwa na kuonyesha mifano yakinifu inayowezesha sayansi hiyo kufanya maajabu yake..Hivyo mwalimu wa somo hilo pia hupata elimu hiyo na kisha kuipokeza kwa mwanafunzi ambaye atakuja itumia elimu ktk maisha yake...mzunguko wa elimu hii hauna mwisho na kila siku elimu hii huzidi kuboreshwa kwa uvumbuzi wa matumizi mbali mbali kwa faida ya nchi, wananchi na viumbe vyote..
Tatizo letu kubwa la elimu ya Uraia nchini ni kwamba hatuna somo..Demokrasia tuliyokuwa nayo ni FEKI ni elimu feki isiyokuwa na utaalam wa kutengeneza a finished product bali tumeagiza Demokrasia toka nchi za nje na tukafungiwa kanyaboya kama biashara yetu ya ukulima ambapo sisi tunalima nakuuza malighafi kisha tunaagiza mali hiyo hiyo toka nje (ulaya) ikiwa finished product kwa matumizi yetu..
Hivyo tunajua kile tunachokitumia kinaitwa nini iwe nguo, shati au Kiatu lakini ukweli utabakia kuwa hatufahamu hatua zilizopita kutengeneza kiatu hicho... na hatuwezi ku improve production, quality au maintain kilichopo kwa sababu it's a foreign made product, sisi ni users end. Tulichokosea ni kuagiza hii finished product kwa jina Demokrasia bila kufahamu inatengenezwa vipi, au kieleimu imetengenzwa vipi ili tuwafundishe raia wetu zaidi ku kufahamu jinsi ya kuitumia tu mezani siku za Uchaguzi..
Hii ndio Demokrasioa tuliyokuwa nayo, Tumeiga kuwa nchi yenye demokrasia ina vyama vingi vya siasa lakini tukashindwa kuelewa kwamba vyama vingi vile vimetokana na tofauti ya Mirengo kama vile tunavyotofautiana ktk imani za dini..
Kwa hiyo kitu cha kwanza ni kulazimisha vyama vyote nchini viwe na mrengo ili wananchi wachague ni imani gani inayoongoka kwao kifikra..Kama dini ya Islaam isingekuwa na mrengo wake, dini ya Kikristu na mrengo wake pamoja na kwamba kinachotafutwa ni kitu kimoja (KUONGOKA) basi ingekuwa haiwezekani kabisa kwetu sisi kuweza kupata elimu ya dini hizo na vigumu kwa binadamu kuchagua dini anayoona kifikra na kiroho itamwongoa..
Kwa hiyo tafauti za dini zetu ndicho chanzo cha elimu ya dini kwa wananchi ili ipate waumini wake hivyo hivyo Demokrasia inatakiwa kuwa na imani hizo mbele ya waumini pamoja na viongozi wake.. Vyama vyetu havina tofauti hizi hata iwe za kimadhehebu tu kwani nimekuja kugundua kwamba vyama vyote nchini kwetu vina mrengo wa kati kushoto.. LIBERAL. sasa ikiwa vyama vyetu ni LEBERAL tutaweza vipi kutoa elimu ya Uraia zaidi ya mapendekezo ya kanisa jinsi ya kuwachagua viongozi wetu?.. kanisa limetoa waraka ule tuchague viongozi wazuri ikiwa na maana tu kwamba nchi yetu haina vyama tofauti,mirengo tofauti na tatizo letu sii vitu hivyo isipokuwa ni viongozi mabovu..
Kuamini hivyo tutakuwa tunazidi kujipotosha zaidi, na pengine inaweza kuwa advantage kwa CCM chama tawala kwa sababu itajenga imnai ya kwamba mrengo na sera sii hoja ya demokrasia isipokuwa viongozi bora ndio hujenga Demokrasia..
Wakuu zangu tuwe makini sana na somo hili la Uraia.. na tuwe makini sana kwa sababu tutajikuta ktk utamaduni wa imani za dini... Utamaduni ambao unatulazimisha sisi wote kuwa Waislaam au Wakristu kwa sababu tu wazazi wetu walikuwa dini hizo. Na elimu ya dini tunayoipata ni ile tu wanayotaka wazazi wetu tuipate iwe ya Biblia au msahafu na sii vyote kwa pamoja tupate kuchagua imani iliyo bora kwetu..yaani tunapata elimu ya dini moja.
Na hatuwezi kusema kuwa sisi ni huru ikiwa tutaabudu dini kwa sababu tu wazazi wetu walizaliwa ktk dini hizo.. Haki na Uhuru wa kweli ktk kuabudu ni pale mtoto anapoweza kupata elimu ya dini zote kisha akachagua yeye ni imani ipi itakayomwokoa au kumfikisha peponi..NDIVYO TULIVYO ni pamoja na kutofikiria uhuru wa mtoto kuchagua imani ya dini wakati tukijua fika kwamba kaburini atakwenda yeye peke yake na atahukumiwa yeye kwa madhambi yake na sii mzazi wake au familia..
Leo hii tanzania watu ni Mafuasi wa CCM au Chadema kwa sababu tu mzazi au ndugu zake ni wafuasi wa chama hicho. Tunafuata watu kujiunga na chama badala ya kukubali mafundisho ya chama ktk mrengo wake kutufikisha peponi (kutuletea maendeleo).
Kwa hiyo ELIMU ya Uraia inatakiwa kwanza tufahamu nini mrengo wa vyama vyetu.. CCM mrengo gani, mafundisho yake ni yapi na vipi tutaweza kuingia peponi (maendeleo ya nchi) na vyama vya Upinzani LAZIMA viwe vinapingana na imani hiyo ya CCM hata iwe kwa sera ili mradi kuleta utofauti kati ya kushoto na kushoto kati..au kwa mfano mzuri tunaoufahamu sisi wote iwe kama tofauti ya madhehebu mawili ya dini moja..lakini sio kutangaza Elimu ya Uraia wakati vyama vyote vinafundisha Imani (mrengo) mmoja na tofauti zao ni rangi ya mavazi na bendera...
Wananchi (Raia) tukishaelewa kuwa CCM wanafuata mrengo gani, Chadema, CUF na wapinzani wote wanafuata mrengo gani ndipo ELIMu ya Uraia itakapo weza kufundishwa kwa waanchi kwani utakuwa ukifundisha somo zima la Utawala iwe ktk mrengo wa Conservative (kulia), Progressive (Kushoto) au kati kushoto (Liberal) na wasiokuwa na dini, yaani Indepent...kwani kila mrengo unatuwezesha kuelewa faida, hasara na gharama ya kuchagua mrengo mmoja. Nyerere alipofungua chuo cha Kigambini kufundisha Ujamaa ni kwa sababu tulikuwa na mrengo mmoja nao ni Usoshalist! hivyo kiongozi unaweza kumchuja kwa wake ktk kujenga Ujamaa..Leo hii Obama anakisiwa kuwa Mjamaa (Soshalist) sii kwa sababu ya ufisadi au uwezo wake kuongoza isipokuwa ni wapi nahodha huyu analipeleka jahazi...Ufisadi is a crime na haki yake ni mahkamani tu hakuna waraka!
Kisha mwananchi ataweza kumchagua mgombea kwa imani kwamba huyu mtu ataweza kusimamia imani hii ya kulia au kushoto kulingana na mafundisho yake..Hivyo kipimo cha mgombea kitatokana na uwezo wake ktk kusimamia mafundisho yaliyofunzwa kwa raia wake kulingana na mrengo na sio kufanya Ukisiaji wa mtu kuwa anaweza kuongoza, kuwakilisha au kusimamia imani isiyokuwepo ila ahadi alizozitoa..
Mwisho, nitasema kwamba wasomi wengi wanshindwa kupiga kura kwa sababu hawaelewi mgombea anasimamia mrengo gani, chama kinasimama kwa vipaumbele vipi (nguzo zake), hivyo huwezi kumchagua mtu tu asimame kama Padre kwa sababu tu amedai kuwa ni Mkristu wakati wananchi wanafahamu fika kuwa mtu huyo hana elimu wala imani yoyote ya dini anayotaka kugombea Upadre..