Elimu ya Uraia Tanzania | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya Uraia Tanzania

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Eryk, Mar 30, 2007.

 1. E

  Eryk Member

  #1
  Mar 30, 2007
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  Nashangazwa sana na wasomi hawa wa chuo hiki kikongwe na tunaamini kinatoa wahitimu wengi bora wenye kuiletea sifa kubwa taifa letu nmaanisha chuo kikuu cha Dar es salaam.

  Katika uchaguzi mkuu pale chuoni kulikuwa na kila aina ya shamlashamla za uchaguzi kama ilivyo kwa chaguzi zingine za kitaifa.

  Sina ugomvi na wagombea mana kili mmoja alitoa sera zake lakini sifikirii kwamba wadau wenyewe wa uchaguzi walikuwa makini na wanachokifanya. Wengi wao inaonyesha walikuwa hawafati mikutano ya wagombea bali walifata muziki.

  Nasema hivi si tu kwa kuwa walijaa sana kwenye makampeni la hasha! Kinachonishangaza ni idadi ya wapiga kura ni ndogo sana ukilinganisha na idadi ya wanachuo. Maana sidhani kama wapiga kula walizidi 5000 kati ya wanafunzi zaidi ya 18000. Sielewi hawa wengine 13000 walikuwa chin ya umri wa kupiga kura ama mwamko mdoga wa kupiga kura.

  Mi nadhani kama utaratibu huu utaendelea basi tutendelea kulia demokrasia milele maana sehemu ambayo tunaamini ni kitovu cha viongozi wa nchi yetu hawajui nini maana ya kupiga kura basi taifa linaelekea kubaya!!!. Uchaguzi huru na wa haki inapaswa kili mdau awajibike toka mwanzo wa mchakato adi mwisho.

  Eti jamani turudi shule ya msingi kufundisha wanachuo Uraia ni nini!!?
   
 2. H

  HKiboka Member

  #2
  Mar 30, 2007
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mmmmh! watanzania mmesikia habari za wale mnao waona wasomi?hawapigi kura!na kampeni zao ni za muziki!
  TUMEPOTEZA!
   
 3. J

  Julian Emmanuel Member

  #3
  Mar 30, 2007
  Joined: Mar 6, 2007
  Messages: 38
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ndugu mtoa mada nadhani maelezo yako yanaweza kuthibitisha kuwa kweli chuo unachokizungumzia kinatoa wasomi wazuri.

  Kampeni ni "interview", sasa labda nikuulize swali kuwa wewe ni mkurugenzi mkuu kampuni fulani ukaitisha interview ya kuajiri mtumishi katika kampuni yako, bilashaka watu wakaomba ukachagua watu ukawaita kwenye usaili. katika kuwasaili ukagundua wote walioitwa kwenye interview hakuna mwenye sifa au uwezo wa kufanya hiyo kazi je utafanyaje?

  Utaajiri mmoja wao kwasababu kampuni inataka kuajiri au utawakataa wote na kutangaza nafasi upya?, au fikiria wewe si mfanyakazi wa hiyo kampuni ila umepewa jukumu la kuchagua aliye bora na ukaletewa orodha ya watu uchague kwenye hao na kutoa mapendekezo na ukagundua hakuna anayefaa je utampendekeza mmoja wao hata kama hafai au utawaeleza orodha mliyonipa sijaona anayefaa kama umepewa nafasi ya kusema hivyo ila kama hujapewa hutachagua mtu maana utakaa kimya.

  Kuhusu demokrasia napenda nikueleze kuwa demokrasia kwa maana yako unayoichukulia si kuchagua katika orodha uliyoletewa tu bali kutokuchagua pia kama hujaridhika na wanaorodha. Si demokrasia kumlazimisha mtu kuchagua asichokitaka.

  lakini katika hali halisi vilevile napenda nikueleze kuwa hakuna demokrasia ya kweli. Chukulia mfano wa Mbunge kuwa yeye ndio msemaji wa kundi fulani la watu? sasa huyo mtu kwanza ana**** zake na kila mtu katika kundi hilo anafikra zake sasa je anawasilisha fikra za nani? kama anawasilisha fikra za kundi huwa wanakaa saa ngapi kujadili na kufikia cha kupeleka bungeni ukiwa kama msimamo wa kundi?.

  Ningependekeza kuwa kabla ya kuwahukumu hawa jamaa ningependa uwaulize kwanini hawakupiga kura hiyo inaweza kukupa dira tofauti na mtizamo kuwa ukisikiliza kampeni lazima uchague mmoja wao au kwa lugha nyingine kuwa ukisikiliza "promotions za bidhaa" lazima ununue.

  Wasomi wengi wanasema msomi aliyeelimika hadanganywi kwa peremende kama siasa za tanzania zinavyoendeshwa. msomi huwezi kumuahidi matokeo akakuamini bali umuahidi mipango umuahidi mikakati ya utekelezaji ndio utajie matokeo akuamini, msomi huwezi kusimama kwenye jukwaa ukiomba uraisi kwa kumkashifu mgombea mwenzako akaona unafaa bali kwa kuchambua ubora wako binafsi.

  Ndugu yangu mimi bado nawaona hawa jamaa wademikrasia kweli maana mbali na kuwa wao hawakuridhika na "sample" walizoletewa na ikawalazimu kutochagua bado wamekaa kimya kuheshimu mitizamo ya wengine
   
 4. H

  HKiboka Member

  #4
  Mar 30, 2007
  Joined: Feb 6, 2007
  Messages: 13
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mimi nimechangia kwa dhana ya uchaguzi tu! japo kichwa cha mwanzilishi hakiendani na kile alicho kiandika!

  Kwani Julian katika jamii hiyo ya wasomi hakuna watu bora? au ni njia gani zinazotumika kuwapata wagombea?je wale waliopiga kura wao wanamtizamo gani? Ni kweli kupiga kura ni hiari ya mtu na ni haki ya mtu! ina maana gani kwa watu waonekanao wasomi kushindwa kutekeleza wajibu au kutumia haki yao kuwachagua viongozi wao? Kweli watakua ni msaada kwa watanzania wengine ambao kuwathamini pale watakapo ombwa ushauri juu ya chaguzi za kitaifa kama hawawezi kuchaguana miongoni mwao?

  Ni kweli kuwa kuwakilisha mawazo ya watu ni kazi ngumu, na kamwe mbunge hawezi kuwakilisha mawazo ya watu wote kwa kuwa watu wanamawazo/mtizamo tofauti juu ya jambo moja.Tatizo ni je mawazo yanayowasilishwa yana manufaa kwa umma au mtu binafsi?Kama ni manufaa ya mtu binafsi basi mbunge hafai na kama yana manufaa kwa umma basi mbunge huyo ni SAFI kabisa!
  Mchumi mmoja aliwahi kusem (samahani kwa kuchanganya lugha, ni kitu ambacho binafsi sikipendi ila nanukuu) "When seven Economists meet,there are eight definitions of any of there disscusion issue that is why economists as other human beings have got a room to differ" Kwa hiyo utofauti wa mawazo hauepukiki,ila swali ni yapi manufaa ya tofauti za mawazo hayo?
   
 5. E

  Eryk Member

  #5
  Apr 4, 2007
  Joined: Mar 23, 2007
  Messages: 6
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
  napenda kusaidia dada juliana maana ameshindwa kuelewa kwamba wale wanaochaguliwa sinkwa faida yao bali ni kwa faida ya jamii nzima ya wale mnaowaita wasomi kama ulininukuu vizuri nilisema kuwa suala la uchaguzi ni jukumu la wadau wote wa ule uchaguzi sio kwamba waliteuliwa waapigiwe kura la hasha bali zilitoka nafasi kwa ajili ya wanaotaka kugombea kufananisha uchaguzi na interview inaonyesha jinsi gani unahitaji Elimu hii ya uraia!>sifikirii kuwa dawa ya kupambana na viongozi wasiowaadilifu ni kukaa kiya na kususia kupiga kura kama unavyodai maana kutokana na Elimu ya URAIA nguvu ya jamii si nyingine bali ni demokrasia haswa linapofika suala la uchaguzi.Je wataka kuniambia kwamba katika wasomi wote hao hakuna anaefaa kwa uongozi!?wako wapi!?wale waliojasili na wenye mayo wa kutumikia chuo chao na watu wake wamejitokeza Mmesusa mbona hakujitokeza kugombea kama wale waliogombea mliona hawafai!!!?nasisitiza ELIMU YA URAIA inahitajika maana ule uchungu wa nchi yetu unapotea.Ndio maana niliuliza uraia ni nini nikijua wengi mmesahau maana halisi ya uraia!!!
   
 6. Yona F. Maro

  Yona F. Maro R I P

  #6
  Sep 3, 2007
  Joined: Nov 2, 2006
  Messages: 4,237
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 0
  Ninablog nikiwa Singida.

  Nimekuta harakati nyingi zinazohusiana na uchaguzi mkuu, utakaofanyika Desemba 14. Yupo Mhindi mmoja hapa anasumbua akili za watu kwa wingi wa hela alizonazo. Ukweli ni kwamba wananchi wa Singida wamekubali awe Mbunge wao si kwa sababu ya sera zake. Ni kwa sababu ya pesa! Hii ni ajbau maana ukimsiliza Mgombea huyu utashangaa kapita pitaje hadi kuteuliwa kuwa mpeperushaji wa bendera ya chama Kikongwe kama CCM? hajui kujieleza na akisimama anachokijua ni kutaja ahadi za miradi ya mamilioni atayoifanya akiwa Mbunge.

  Ni wazi, nimegundua, Vijana wengi wa MJi huu na mkoa kwa ujumla hawana elimu ya Uraia. Wengi wanafuata mkumbo na hawajuai umuhimu wao kushirikji katiuika masuala ya siasa. Utakuta wamejaa kijiweni wakilaumu kwa nini huyu bwana (Mhindi) kapitishwa na chama chake awe mgombea...wanalalamika sana. Ajabu ni kwamba ukiwauliza kama wamejiandikisha kupiga kura, watakwambia "hilo halihusiani na wala si muhimu...kura moja itaathiri nini?"

  Naam.Hiyo ndio Singida, mji wenye vijana wanaojua umuhimu wa kulalamikia wagombea, lakini wasiojua umuhimu wa kupiga kura!

  Tatizo hili la kukosa elimu ya uraia haliko hapa SIngida tu, limeenea mahali pengi. Watu hajaelimiaka kuhusu siasa. Ndio maana ukiwauliza wazee wa hapa watakwambia kuwa "Kuchagua chama kingine cha siasa mbali na Chama hatamu, uanachagua vita!" Hizo ndio propaganda ziznazotumiwa kuwapoteza wananchi hapa.

  Lakini naambiwa Mbowe amegeuza fikra za vijana wa mji huu na lolote linaweza kutokea kwa maana ya CCM kupoteza umaarufu hapa
   
 7. Mkaa Mweupe

  Mkaa Mweupe JF-Expert Member

  #7
  Jun 9, 2009
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 654
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Waungwana, ninalo jambo ambalo linanitatiza na kunisikitisha kama na wewe unatilia maanani.

  Hivi karibuni swala la ushabiki wa kitaifa limeongezeka katika nchi yetu ya Tanzania. Watu wengi wamekuwa na mwamko wa kupeperusha bendera ya nchi katika matamasha mbalimbali zikiwamo sherehe za kitaifa na hata katika michezo. Ila la kusikitisha ni jinsi ambavyo bendera yetu inavyopeperushwa.

  Namna sahihi ya kupeperusha bendera ya Tanzania ni kama ifuatavyo. Vigezo vya kuzingatia:
  1. Rangi ya buluu inakuwa chini
  2. Rangi nyeusi inakuwa inaeleke juu, yaani inaongezeka kadiri blue inavoongezeka
  3. Rangi ya kijani inakuwa juu


  Jambo la kusikitisha, katika sherehe za mei mosi mwaka huu vibendera vilivyotumika katika maadhimisho hayo viliwambwa vibaya. Je, kwa staili hii waTanzania tutaweza kushindana katika maswala ya Quality Assuarance? Inaelekea kila jambo linafanyika bora liende.

  Waungwana naomba mchango wenu.
   
 8. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #8
  Aug 16, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Kimsingi ni jambo zuri wakati jumuiya na taasisi mbalimbali zaonyesha hamu ya kutoa elimu ya uraia kwa watanzania. Lakini ni vyema tuelewe kuwa elimu ya uraia ni suala la kudumu (long term), na ni muhimu kuwe na utaratibu, program na silabasi maalum.

  Ili mambo hayo yawezekane ni lazima kuwe na msimamizi mmoja ambaye atasimamia, atahakiki na kutoa elimu hiyo bila kujali tofauti zetu, kama vile dini, kabila, jinsia, rangi na n.k. Na kwa vigezo hivyo sioni jumuiya, taasisi au NGO yeyote itakayoweza kupewa kuongoza shughuli hizo ispokuwa Serikali chini ya wizara husika. Hii itasaidia kuleta imani kwa walengwa, bila kuwa na hisia mbovu kwani pindi wakoseapo ni rahisi kuwasuta na kufikia muafaka wa marekebisho.

  Na katika misingi hii, ninawaelewa kabisa akina Kingunge, Makwaia na wengine walioiomba kanisa katoliki kufuta waraka wao juu ya elimu ya uraia kwa uchaguzi 2010. Kifupi waraka huo nimeusoma na unamantiki hasa kwa kuzingatia hali halisi ya ufisadi inayoendelea hapa nchini. Lakini hebu fikiria, kama mimi na kikundi changu cha jummuiya ya "wakati wa ukombozi ni sasa" na ufisadi ukawa si ajenda namba moja kwetu, ila wale wagombea ubunge wasio weusi ndio wakaniudhi zaidi na nikaamua kutoa elimu ya uraia katika mantiki hiyo. Je nitakuwa na kosa? Na ni nini kipimo cha usahihi, nusu sahihi, robo sahihi wa elimu yangu ya uraia katika kijitabu changu. Ni Katoliki, Bakwata, wananchi au serikali itayokuwa na jukumu la kupima usahihi wa silabasi yangu?

  Tukilielewa hili tutafumbua macho na kujua kwanini Kingunge ameuita warakaa wa Katoliki juu ya elimu ya uraia kuwa ni "udini". Wahenga wasema jihadhari kabla ya hatari, na hilo ndilo analolifanya Kingunge. Kama wazee hawa hawatapiga kelele kwa vitendo kama hivi basi itakuwa vigumu kuelewa ni nini shughuli za serikali na ni nini shughuli za taasisi za kidini. Na tukifikia hapo, basi tutakuwa na serikali ndani ya serikali, kitu ambacho ni hatari sana. Kwa sababu serikali itapoteza dira, na kuwa kama mwanasesere na badala yake kuendeshwa na taasisi, hususan za kidini kama vatikan na n.k.

  Nchi yetu ipo katika mtikisiko kwa mengi yaliyotokea na yanayotoke, ufisadi, rushwa, kukithiri kwa umasikini na heka heka mbaya za chaguzi. Lakini jibu la mtikisiko huo si kuzipa nafasi taasisi za kidini na nyinginezo kuteka shughuli za serikali kwa njia ya mapinduzi baridi, bai ni kupitia wananchi kuishinyikiza serikali ili ibadilike. Ni lazima tuelewe kuwa hata hizo taasisi za dini hutumia wananchi kuishinyikiza serikali ila hazifanyi hivyo mpaka zitugawe kwanza. Ni vipi tutakuwa pamoja ikiwa mashinyikizo ya taasisi za kidini ni lazima yaanzie Kanisani au msikitini.

  Ni katika mazingira haya, Kingunge na washiriki wake daima watakuwa sahihi. Shughuli za serikali ni lazima ziachiwe serikali. Na hili la elimu ya uraia ni la serikali, basi silabasi yake itatolewa na serikali na sio kiholela.
   
 9. M

  Mvutakamba Member

  #9
  Aug 16, 2009
  Joined: Jul 31, 2009
  Messages: 58
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unataka chanzo kipi ndicho kipewe mamlaka ? Kikundi chao akina Kingunge ? Hapa hatujadili kusimamisha waraka tuna jadili kutaka kujua maeneo gani hayapata waraka ili upelekwe .Elimu ua Bure na message naona inashika moyo kama moto wa porini .Waraka haujavunja Katiba na hausemi nani achaguliwe wa dini gani hapana bali kiongozi safi machoni pa watu wake .

  Mod hii na Kingunge na mwazo yale dumavu peleka vikae pamoja
   
 10. Sophist

  Sophist JF-Expert Member

  #10
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 26, 2009
  Messages: 3,087
  Likes Received: 1,731
  Trophy Points: 280
  Ngoda, unatakiwa kufahamu yafuatayo:

  1. Elimu ya uraia ni uelewa na maarifa ya raia juu ya haki na wajibu wa raia vis-a-vis mamlaka za utawala. uelewa na maarifa ya umma hayana mipaka na hayamilikiwi na mtu au kundi lolote; serikali ni mojawapo ya makundi maslahi katika suala la elimu ya uraia hivyo haiwezi kuaminiwa kumiliki elimu ya uraia.
  2. Kutokana na hadhi na umuhimu wake, elimu ya uraia haimilikiwi na wala haiwezi kudaiwa kumilikiwa na mtu, kundi la watu wala chanzo chake; kudai kilichomo ndani ya waraka uliotolewa na wakatoliki mawazo ya wakatoliki kwa manufaa ya wakatoliki weneyewe, hivyo kila kundi au mtu anaweza kutoa 'elimu yake ya uraia' ni ama upotoshaji wa makusudi au ishara kuwa na uelewa ndogo kuhusu hoja/suala husika.
  3. Tangu mwaka 1990 serikali imeonyesha kutokuwa na nia ya kutoa elimu ya uraia, ikihofia kuondolewa madarakani; hivyo kutaka serikali ihodhi ukiritimba wa kutoa elimu ya uraia ni sawa na raia kudai waendelee (kushangilia) kuongozwa na mafisadi.
  4. Ki-msingi, kuendelea kushamili kwa ufisadi katika uongozi wa umma ni kutokana na uduni wa kiwango cha elimu ya uraia miongoni mwa watanzania na wananchi wa kawaida walio wengi.
  5. Je, unataka ufisadi uendelee?
  6. Kugawanyika kwa wananchi baina ya kundi linalosimamia kulinda maslahi ya umma na kundi pinzani dhidi ya hilo, tofauti na mawazo ya akina Kingunge, ni jambo la kheri kwa manufaa ya maendeleo ya Tanzania; nani yuko kundi la akina Kingunge Ngombara Mwiru?
   
 11. Z

  Zawadi Ngoda JF-Expert Member

  #11
  Aug 16, 2009
  Joined: Aug 13, 2009
  Messages: 2,290
  Likes Received: 175
  Trophy Points: 160
  Sophist, ni vyema kufahamu kuwa long term problems lazima zitatuliwe na long term program. Tatizo hujafahamu madhgara ya long term propblems kutatuliwa na short term programs. Tusitatue tatizo kwa kuongeza tatizo. DDT ni dawa nzuri kwa kuuwa mbu, lakini sasa hivi imepigwa marufuku kwa sababu ilikuwa na madhara makubwa kuliko faida zake.

  Dawa ya kanisa katoliki kutatua tatizo lililopo ni sawa na DDT. Ina madhara zaidi kuliko faida na mbaya zaidi ni pale ambapo haitaweza kuwafikia watu wote kutokana na kuwa na watanzania 30% wenye imani hiyo. Hapa utakuwa mwepesi kusema kuwa kila mtanzania anakaribishwa, lakini kabla hujaenda mbali, hebu jiulize kuwa ni jukwaa gani linatolewa elimu hiyo?

  Elimu ya uraia ni elimu ihusuyo haki ya raia katika nchi yake, hivyo mlengwa ni lazima awe na imani na mtoaji wa elimu hiyo. Kuna watu ambbao hawana imani kabisa nakanisa katoliki na huwezi kuwalazimisha. Kwa majibu rahisi hapa utasema, shauri yao kama hawataki ni basi. Lakini kumbuka ya kwamba, haki ya kupata elimu ya uraia ni haki ya watanzania wote. Na hapo ndio Kingunge anapopapigia kelele.

  Tufumbue macho na kuona mbali, vinginevyo tutaletaa ushindani katika mambo ambayo hayahitaji ushindani.
   
 12. Lunyungu

  Lunyungu JF-Expert Member

  #12
  Aug 16, 2009
  Joined: Aug 7, 2006
  Messages: 8,836
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145

  Penye ukweli tutasema ,kazi ya kuleta mageuzi Singika haijafanywa na Mbowe kama yeye ila na Chama chake kupitia TUndu LIssu ambaye kwa kweli sasa anajulikana kuliko hata mkuu wa Mkoa .Kafungua minyororo ya dhuluma kila kona kwa kuwapelekesha ki sheria na siasa za uwazi .
   
 13. M

  Mkandara Verified User

  #13
  Aug 16, 2009
  Joined: Mar 3, 2006
  Messages: 15,443
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Mkuu maelezo yako mazuri sana na umekita pale panapotakiwa haswaaa!..
  Hakika mada hii ni muhimu sana kwetu sisi wote na ningeomba kila mmoja wetu achangie mada hii kuhusiana na ELIMU ya URAIA, kwani a lot is at stake 2010 na huko tuendako..

  Kwanza kabisa nitasema kuwa Elimu ya Uraia inatanguliwa na mfumo mzima unaowaongoza wananchi (raia) na utawala (serikali) itakayoongoza - hakuna mwenye madaraka wala nguvu ya tunga elimu hiyo ila elimu hiyo inakuwepo tayari kwa wote wahusika..Hivyo somo zima linajijenga kama masomo mengine ya elimu kisayansi kukiwa na imani tofauti zinazopingana.

  Kwa mfano mwalimu wa Chemistry hufundisha kile ambacho tayari kimekwisha gunduliwa na kuonyesha mifano yakinifu inayowezesha sayansi hiyo kufanya maajabu yake..Hivyo mwalimu wa somo hilo pia hupata elimu hiyo na kisha kuipokeza kwa mwanafunzi ambaye atakuja itumia elimu ktk maisha yake...mzunguko wa elimu hii hauna mwisho na kila siku elimu hii huzidi kuboreshwa kwa uvumbuzi wa matumizi mbali mbali kwa faida ya nchi, wananchi na viumbe vyote..

  Tatizo letu kubwa la elimu ya Uraia nchini ni kwamba hatuna somo..Demokrasia tuliyokuwa nayo ni FEKI ni elimu feki isiyokuwa na utaalam wa kutengeneza a finished product bali tumeagiza Demokrasia toka nchi za nje na tukafungiwa kanyaboya kama biashara yetu ya ukulima ambapo sisi tunalima nakuuza malighafi kisha tunaagiza mali hiyo hiyo toka nje (ulaya) ikiwa finished product kwa matumizi yetu..

  Hivyo tunajua kile tunachokitumia kinaitwa nini iwe nguo, shati au Kiatu lakini ukweli utabakia kuwa hatufahamu hatua zilizopita kutengeneza kiatu hicho... na hatuwezi ku improve production, quality au maintain kilichopo kwa sababu it's a foreign made product, sisi ni users end. Tulichokosea ni kuagiza hii finished product kwa jina Demokrasia bila kufahamu inatengenezwa vipi, au kieleimu imetengenzwa vipi ili tuwafundishe raia wetu zaidi ku kufahamu jinsi ya kuitumia tu mezani siku za Uchaguzi..

  Hii ndio Demokrasioa tuliyokuwa nayo, Tumeiga kuwa nchi yenye demokrasia ina vyama vingi vya siasa lakini tukashindwa kuelewa kwamba vyama vingi vile vimetokana na tofauti ya Mirengo kama vile tunavyotofautiana ktk imani za dini..

  Kwa hiyo kitu cha kwanza ni kulazimisha vyama vyote nchini viwe na mrengo ili wananchi wachague ni imani gani inayoongoka kwao kifikra..Kama dini ya Islaam isingekuwa na mrengo wake, dini ya Kikristu na mrengo wake pamoja na kwamba kinachotafutwa ni kitu kimoja (KUONGOKA) basi ingekuwa haiwezekani kabisa kwetu sisi kuweza kupata elimu ya dini hizo na vigumu kwa binadamu kuchagua dini anayoona kifikra na kiroho itamwongoa..

  Kwa hiyo tafauti za dini zetu ndicho chanzo cha elimu ya dini kwa wananchi ili ipate waumini wake hivyo hivyo Demokrasia inatakiwa kuwa na imani hizo mbele ya waumini pamoja na viongozi wake.. Vyama vyetu havina tofauti hizi hata iwe za kimadhehebu tu kwani nimekuja kugundua kwamba vyama vyote nchini kwetu vina mrengo wa kati kushoto.. LIBERAL. sasa ikiwa vyama vyetu ni LEBERAL tutaweza vipi kutoa elimu ya Uraia zaidi ya mapendekezo ya kanisa jinsi ya kuwachagua viongozi wetu?.. kanisa limetoa waraka ule tuchague viongozi wazuri ikiwa na maana tu kwamba nchi yetu haina vyama tofauti,mirengo tofauti na tatizo letu sii vitu hivyo isipokuwa ni viongozi mabovu..

  Kuamini hivyo tutakuwa tunazidi kujipotosha zaidi, na pengine inaweza kuwa advantage kwa CCM chama tawala kwa sababu itajenga imnai ya kwamba mrengo na sera sii hoja ya demokrasia isipokuwa viongozi bora ndio hujenga Demokrasia..

  Wakuu zangu tuwe makini sana na somo hili la Uraia.. na tuwe makini sana kwa sababu tutajikuta ktk utamaduni wa imani za dini... Utamaduni ambao unatulazimisha sisi wote kuwa Waislaam au Wakristu kwa sababu tu wazazi wetu walikuwa dini hizo. Na elimu ya dini tunayoipata ni ile tu wanayotaka wazazi wetu tuipate iwe ya Biblia au msahafu na sii vyote kwa pamoja tupate kuchagua imani iliyo bora kwetu..yaani tunapata elimu ya dini moja.

  Na hatuwezi kusema kuwa sisi ni huru ikiwa tutaabudu dini kwa sababu tu wazazi wetu walizaliwa ktk dini hizo.. Haki na Uhuru wa kweli ktk kuabudu ni pale mtoto anapoweza kupata elimu ya dini zote kisha akachagua yeye ni imani ipi itakayomwokoa au kumfikisha peponi..NDIVYO TULIVYO ni pamoja na kutofikiria uhuru wa mtoto kuchagua imani ya dini wakati tukijua fika kwamba kaburini atakwenda yeye peke yake na atahukumiwa yeye kwa madhambi yake na sii mzazi wake au familia..
  Leo hii tanzania watu ni Mafuasi wa CCM au Chadema kwa sababu tu mzazi au ndugu zake ni wafuasi wa chama hicho. Tunafuata watu kujiunga na chama badala ya kukubali mafundisho ya chama ktk mrengo wake kutufikisha peponi (kutuletea maendeleo).

  Kwa hiyo ELIMU ya Uraia inatakiwa kwanza tufahamu nini mrengo wa vyama vyetu.. CCM mrengo gani, mafundisho yake ni yapi na vipi tutaweza kuingia peponi (maendeleo ya nchi) na vyama vya Upinzani LAZIMA viwe vinapingana na imani hiyo ya CCM hata iwe kwa sera ili mradi kuleta utofauti kati ya kushoto na kushoto kati..au kwa mfano mzuri tunaoufahamu sisi wote iwe kama tofauti ya madhehebu mawili ya dini moja..lakini sio kutangaza Elimu ya Uraia wakati vyama vyote vinafundisha Imani (mrengo) mmoja na tofauti zao ni rangi ya mavazi na bendera...

  Wananchi (Raia) tukishaelewa kuwa CCM wanafuata mrengo gani, Chadema, CUF na wapinzani wote wanafuata mrengo gani ndipo ELIMu ya Uraia itakapo weza kufundishwa kwa waanchi kwani utakuwa ukifundisha somo zima la Utawala iwe ktk mrengo wa Conservative (kulia), Progressive (Kushoto) au kati kushoto (Liberal) na wasiokuwa na dini, yaani Indepent...kwani kila mrengo unatuwezesha kuelewa faida, hasara na gharama ya kuchagua mrengo mmoja. Nyerere alipofungua chuo cha Kigambini kufundisha Ujamaa ni kwa sababu tulikuwa na mrengo mmoja nao ni Usoshalist! hivyo kiongozi unaweza kumchuja kwa wake ktk kujenga Ujamaa..Leo hii Obama anakisiwa kuwa Mjamaa (Soshalist) sii kwa sababu ya ufisadi au uwezo wake kuongoza isipokuwa ni wapi nahodha huyu analipeleka jahazi...Ufisadi is a crime na haki yake ni mahkamani tu hakuna waraka!

  Kisha mwananchi ataweza kumchagua mgombea kwa imani kwamba huyu mtu ataweza kusimamia imani hii ya kulia au kushoto kulingana na mafundisho yake..Hivyo kipimo cha mgombea kitatokana na uwezo wake ktk kusimamia mafundisho yaliyofunzwa kwa raia wake kulingana na mrengo na sio kufanya Ukisiaji wa mtu kuwa anaweza kuongoza, kuwakilisha au kusimamia imani isiyokuwepo ila ahadi alizozitoa..

  Mwisho, nitasema kwamba wasomi wengi wanshindwa kupiga kura kwa sababu hawaelewi mgombea anasimamia mrengo gani, chama kinasimama kwa vipaumbele vipi (nguzo zake), hivyo huwezi kumchagua mtu tu asimame kama Padre kwa sababu tu amedai kuwa ni Mkristu wakati wananchi wanafahamu fika kuwa mtu huyo hana elimu wala imani yoyote ya dini anayotaka kugombea Upadre..
   
  Last edited: Aug 16, 2009
 14. Bigirita

  Bigirita JF-Expert Member

  #14
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 13,976
  Likes Received: 688
  Trophy Points: 280
  In a serious note: tuna walimu wazuri wa uraia na elimu ya sisa za tz ndani ya jf. Kuna mijadala mizuri sana yenye diversity of political views amd opinion.
  Utajiri huu utatusaidiaje sisi ambao ni supppsedly wanaharakati na sio wapiga porojo, kama wenzetu, watanzania, ambao ni wengi kuliko sisi kwa mamilioni mengi
  Hawatapata japo kiduchu ya hazina hii.

  Napendekeza tuanzish
  e jarida la jf uraia. Kwa lugha rahisi na tamu,
   
 15. B

  BENE Member

  #15
  Feb 16, 2010
  Joined: Jan 21, 2010
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hilo neno my dear
  hiyo ingetouch kila eneo
  jarida litembee kuazia shuleni hasa secondary mpaka vyuoni na wale wa ngazi ya chini kabisa
  good idea i like it
   
 16. D

  Donrich Senior Member

  #16
  Mar 28, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Kwa kuwa muda uliobaki kuelekea uchaguzi mkuu ni mchache,na kwa kuwa tume ya uchaguzi ambayo ndiyo yenye dhamana ya kutoa elimu ya uraia kwa wapiga kura imeshindwa kutimiza wajibu wake.

  Je waheshimiwa wajumbe hamdhani kuwa sasa ni wakati muafaka wa viongozi wa vyama hasa upinzani kuanza kuwahamasisha wapiga kura kujiandikisha kwenye daftari la kudumu la wapiga kura.kwa mikoa iliyobaki zoezi ambalo linatakiwa kwenda sambamba na kuwaelimisha wapiga kura kutorubuniwa kuuza shahada zao muda wa kupiga kura muda utakapofika.
   
 17. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #17
  Mar 29, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 180
  CCM hawatoi elimu ya uraia. Sasa hivi wanazunguka mitaani wanaandikisha wanachama wapya hasa vijana. Kwao elimu ya uraia ni hatari.
   
 18. Geza Ulole

  Geza Ulole JF-Expert Member

  #18
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 31, 2009
  Messages: 11,066
  Likes Received: 3,999
  Trophy Points: 280
  Wajameni, mie naomba kuwakilisha hili ninashangazwa na uelewa wa watu juu ya kitendo cha CHADEMA kumsusia Kikwete, hivi cha ajabu nini? katika demokrasia kunaruhusiwa kutofautiana na nashangaa pale ati watu wanasema Kikwete kakosewa heshima ina maana huyu Mkulu kaweka maskio pamba kutosikia malalamiko juu ya matokeo ya uchaguzi usio wa haki? uliomuweka madarakani? au ndo mambo ya kutumia uelewa mdogo wa wengi wa wananchi kuendelea kutawala kimabavu kwa kuwaita CHADEMA ni watovu wa nidhamu? Hivi Watanzania ni kweli tunadhani CCM itatoka madarakani bila vuguguvu la kuishurutuisha CCM? hebu nipeni chama kimoja Afrika kilichotoka madarakani bila ya kujitolea kwa wananchi kupigania haki yao? na kama kipo basi angalia historia lazma kutakuwa ama na nguvu za jeshi au za taasisi za dini zilizotoa msisimuko na kwa Tanzania vyote hivyo vipo mikononi mwa CCM! Vita ya demokrasia inabaki mikononi mwa sisi wananchi na kwa bahati mbaya elimu ya walio wengi juu ya demokrasia ni finyu! watu wanatafsiri ati ni kumkosea heshima Rais na si kuangalia agenda kuu ya mgomo ule yaani katiba mpya na tume huru ya Uchaguzi! nadhani muda utafika tutaona wanachofanya CHADEMA ni kwa faida yetu na si mzaha! CCM ishawarubuni CUF, TLP na NCCR-Mageuzi watu hawaoni kuwa upinzani unakufa na tunaelekea chama kimoja sasa! jamani tuamke Kikwete hajatukanwa na katiba inaruhusu na ni haki ya mtu kutomsikiliza mwingine hata kama ni Kikwete! Huo utovu wa nidhamu unaozungumziwa ni katika kuikandamiza demokrasia na tusipumbazwe na kudanganyika katiba Mpya na Tume Huru ni muhimu kama kweli tunataka mabadiliko na ustawi wa jamii bora katika nchi ya demokrasia na itikadi nyingi! Hebu jaribuni kuangalia "Making of constitution" in youtube kuona jinsi Kenya walivyojitolea na uangalie jinsi tulivyo mbali kufikia walipo kidemokrasia!
   
 19. e

  emma 26 Senior Member

  #19
  Nov 21, 2010
  Joined: Oct 29, 2010
  Messages: 108
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  ehe sisi tlp tumenyamaza uwanja wenu
   
 20. Kardo Joseph

  Kardo Joseph New Member

  #20
  Oct 6, 2011
  Joined: Oct 6, 2011
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ukifuatia mchakato wa uchaguzi mdogo wa ubunge katika jimbo la Igunga uliomalizika hivi karibuni na matokeo yake kutangazwa, inaonesha dhahiri utofauti wa matokeo kwa upande wa mjini na vijijini. Kwa tathimini ya haraka tu tena bila kukaa darasani inaonekana watanzania wengi na hasa waishio vijijini bado hawatambui kuwa nchi yetu ipo katika mfumo wa vyama vingi vya siasa, wanachotambua mpaka sasa ni kwamba nchi yetu ni ya chama kimoja ambacho ni chama tawala. Kwa maana hii kuna haja ya kuwepo kwa jitihada za pekee kutoka katika kila chama ama kwa pamoja kwa makubaliano ya vyama vyote kuendesha elimu ya urai kwa watanzania wote na hasa waishio vijijini ambako bado hawajaelewa nchi yetu iko wapi kwa sasa. Kuna pahala pengine vijijini bado wanatambua kuwa Rais wa nchi yetu ni Marehem Baba wa Taifa. Kama zoezi hili likifanyika kwa ufasaha pengine matokeo yake yakajieleza vema katika chaguzi zijazo.
   
Loading...