Elimu ya Tanzania imeshuka? Naomba Msaada | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Elimu ya Tanzania imeshuka? Naomba Msaada

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by blackwizard, Feb 14, 2012.

 1. b

  blackwizard Senior Member

  #1
  Feb 14, 2012
  Joined: Feb 8, 2012
  Messages: 163
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Nimejaribu kufuatilia elimu ya tanzania hasa kiwango cha degree, napata tabu kuona mwanafunzi wa chuo kikuu (ICT, ACCOUNTANCY etc) hawezi kufanya kazi za msingi kwenye fani yao. Hili limenitia wasiwasi maana hawa wahtiimu hurudi kufanya certificate ili waweze kufanya kazi iliyokusudiwa. Tatizo lilianza pale Wizara ya elimu ilipoamua kuwa na direct entry kwa vyuo vikuu bila kubadilisha mitaala ya vyuo hivyo. inaweza kuwa kutokana na matakwa binafsi ya waziri husika wa wakati huo. Hili sio la msingi ila inafahamika enzi za mwalimu ama wakati nasoma mimi wanafunzi wanaofanya vizuri walijiunga na vyuo vya ufundi ili wakimaliza wakajifunze utawala vyuo vikuu. Baada ya kubadilisha mfumo tukakuta wale wanafunzi wenye uwezo zaidi hawakupata nafasi ya kujiunga na vyuo vya juu balii wale vihiyo walioshindwa kujiunga na vyuo vya ufundi. nakubaliana na mtoa mada mmoja aliyesema waalimu waliosoma diploma ni wazuri kuliko wa degree. Hivyo nashauri mfumo wa elimu ya vyuo vikuu ubadilishwe mara moja. Hili litasaidia kuwapa wanafunzi uwezo wa utendji zidi ya generalknowledge. dunia nzimaimekubaliana kuacha mfumo wa kizamani wa kutoa general knowledge katika elimu na kutumia competant based training education (CEBET), na jukuu hilo kupewa NACTE. Chakushangaza vyuo nguli vyote vimegoma kufuata mfumo huo kwani bodi iliyoundwa kufuatilia mchakato huo ni mpya kwao. Sasa umaskini wa tanzania hautokani na mafisadi wala wizi wa madini ila elimu mbovu naomba wana jamii tupige kelele kwenye hili Tanzania ijikomboe. Alamsik "Black wizard"
   
Loading...