Elimu ya sasa hivi haisaidii mtu kuweza kujiajiri wala haitoi wahitimu wenye sifa stahiki

yuda75

JF-Expert Member
Aug 16, 2020
520
1,378
Elimu siku hizi ni ile bora ni graduate mjomba atanisaidia nipate kazi.

Kwanini nasema hivyo, nimeenda na kuona interview nyingi sana baadhi ya wahitimu wanaokuwa wamemaliza hawana uelewa wa walichosomea kutokana na ile kukaririshwa.

Mfano niliwahi sikia chuo fulani lecture fulani akitunga mtihani lazima ujibu kile alichofundisha sasa unashindwa kuelewa anapima uelewa wa mwanafunzi au uwezo wa mwanafunzi kukariri.

Zamani ukisikia mtu graduate ana degree ilikuwa unamuogopa sana sasa hivi graduate wa bachelor degree unaweza mpambanisha na mtoto wa dasasa la saba agha khan au tusiime na akakalishwa kuanzia kujitambulisha, ujuzi na uelewa wa mambo.

Je, kuna ukweli wowote?
 
Hata wa zamani wengi wao uwezo ulikuwa mdogo. Kazi wakaenda kujifunzia makazini.

Kiingereza chao pia kilikuwa tia Maji tia Maji. Haukuwa na uwezo wa kiakili wa kuona udhaifu wao

Ulishasikia wanasiasa wa zamani wakijieleza kwa kimalkia?
 
Hakuna ukwel wowote kuhusiana kulinganisha darasa la saba la degree holder wakawa sawa ww nadhan lengo lako ni kulnganisha uwezo kuongea kingereza na kujua lugha na ujuzi katka specialization ni tofauti kabisa.
 
Wapo baadhi ya graduate wapo vizuri kuanzia soft skills ikiwemo communication skills na hata katika professional zao.

Ila kuna wengine wana hali mbaya sana mpaka wao wenyewe wanakiri kuwa kwao mambo ni magumu (wengi wao ni waliosoma kozi ambazo hawakuzipenda au walisoma under influence ya watu fulani)

Tukirudi kwenye baadhi ya tahasisi zinazowatoa hao wahitimu hali ni mbaya hata kwa baadhi ya waalimu na mitaala pia.

Asilimia kubwa ya wale wanaojitambua ndiyo huanza kujiongeza mapema wakiwa vyuoni kwa kujifunza skills za ziada ila kundi lingine hubaki kusubiri amalize tu aondoke.

Graduates siyo wote ila asilimia kubwa ni wabovu
 
Hii lugha ya kimalkia hii inawafanya baadhi waonekane vlaza kwenye communication skills ila unakuta ni wazuri tu kichwani na sasa hiv ukipiga na kile cha kimarekani daah unawaua watu kabisa,cjui kwann inakuwa hiv
 
Hakuna mazoezi ya kuongea kingereza
 
Wapo baadhi ya graduate wapo vizuri kuanzia soft skills ikiwemo communication skills na hata katika professional zao.

Ila kuna wengine wana hali mbaya sana mpaka wao wenyewe wanakiri kuwa kwao mambo ni magumu (wengi wao ni waliosoma kozi ambazo hawakuzipenda au walisoma under influence ya watu fulani)

Tukirudi kwenye baadhi ya tahasisi zinazowatoa hao wahitimu hali ni mbaya hata kwa baadhi ya waalimu na mitaala pia.

Asilimia kubwa ya wale wanaojitambua ndiyo huanza kujiongeza mapema wakiwa vyuoni kwa kujifunza skills za ziada ila kundi lingine hubaki kusubiri amalize tu aondoke.

Graduates siyo wote ila asilimia kubwa ni wabovu
Wa vyuo gani mkuu ?
 
Kama bado tunaona kujua kuongea lugha ya kingereza bas ndo kuelimika vzr bas hii inamaansha bado tupo utumwani what matters unananin kichwan na unawezaje kutumia skills zako ulizosoma kua productive
Exactly, Mim kwa mtanzania kutokuongea kingereza vizuri sio big deal, sababu huku almost 99% tunaongea kiswahili mean sehemu ya kupractice kingereza ni finyu, ni Kama ulivyosema kujua kingereza hakuna uhusiano na akili
 
Serikali irejeshe walimu was zamani wote wale was miaka ya 70 kama wapo na wanaweza kufanya kazi wasaidiwe warudi kufundisha, hawa was siku hizi wnaofaulu kwa kutumia vikombora na vifaru kwenye nyeti hawawezi kuwa walimu bora tunadanganyana!

Kupima ufaulu kwa kuangalia mtihani was makaratasi tuu haisaidii kugundua uelimikaji was mhusika, tuwapime wahitimu wetu kwa assignment za muda mrefu ndipo tumpe cheti cha kuhitimu shule au chuo, kwa kufanya hivyo mwanafunzi atajituma kuelewa anachosomea na Si kukariri kwa ajili ya kufauru.
 
Si kweli kabsa kuwa

Elimu ya sasa hivi haisaidii mtu kuweza kujiajiri wala haitoi wahitimu wenye sifa stahiki,​

Kwa sababu inategemea unasomea kitu gani. Sio lazima kila unachokisomea unaweza kujiajiri kupitia hicho ulichosomea , ila tunategemea kutoka kwa huyo graduant kuwa na ufahamu na kujiamini katika kukabiliana na changamoto zinazo mkabili katika maisha ikiwemo kujitaftia kipato na kuwa na mawazo mapana zaidi juu ya hilo.
Na ndio maana ukifuatilia hata vyuoni unakuta kuna kozi una soma lakini mda mwingine hazilingani hata na degree program yako.
Lengo unakuta ni kumpanua kifikra na mtazamo mwanafunzi huyo , na kama umesoma hadi hiyo degree apo Lazma tu hicho kitu utakuwa umekutana nacho bila shaka...
Pia kusomea kozi usioipenda ama kufuata mkumbo huchangia zaidi kutoa wanafunzi wenye ufahamu mdogo kwenye hizo koz wanazosoma , na hii upelekea hata performance kuwa chini sana kwa wanafunzi wa aina hii , na ndio tunao wengi saana katka vyuo vyetu.
Lakini bado kuna umuhimu wa kusoma elimu ya degree na huwezi mlinganisha class seven na graduants maana tofauti yao ni muda tu na uwezo wa kufikiri katika namna ya kukabiliana na changamoto za kimaisha .
Ambalo ndio lengo kubwa.
 
Back
Top Bottom