Elimu ya juu huleta umasikini

Elimu ya juu huleta umasikini

Hapa ndio unafiki wa watanzania unapojidhihirisha! Sasa mnatajaje? Mtu asiposoma mnamwita kilaza/bashite wanaosoma, mnawaambia wanapoteza muda! Sasa mnataka nini?
Hahahahaha uwiiiiii jaman jaman
 
nombo toby kwani hata huko nje ya Tanzania let's say Marekani ama China askari, walimu ama nurses ni matajiri? Huwezi kuona umuhimu wa askari kwa maana unaishi kwa amani ila hujui hiyo amani inapatikana vipi. Huwezi kuona umuhimu wa mwalimu kwa maana sasa unajua kusoma na kuandika upuuzi kama huu na huwezi kuona umuhimu wa nurses kwa maana una afya njema kwa sasa...

You are still a little boy, nimekusamehe bure....
Nmekupenda buree bright one
 
MTU mwenye Mali huilinda Mali yake
MTU mwenye elimu .elimu yake humlinda
MTU mwenye Mali kadiri anavyoitumia hupungua
MTU mwenye elimu kadiri anavyoitumia huongezeka MTU mwenye Mali huwa na maadui wengi
MTU mwenye elimu huwa na marafiki wengi
Maneno yakisomi apo tuu ktk maneno utamjua mtu kichwani yupo vizur
 
Moja katika ushauri niliopewa na dingi ni kuwa unapoajiriwa ukishasign employment letter anza kujenga mazingira ya maisha yako ya kustaafu.

Pamoja na kua elimu inadumaza akili, lakini maisha yakianguka upande wa biashara na kilimo, unapoomba msaada kwa jamaa, kama una ki-elimu kidogo wanajua waanzie wapi kukusaidia, sasa ndugu maisha yanakupiga na vyeti ni vya Daudi Bashite.
 
Mimi bado naamini elimu ni ufunguo wa maisha ila kuna tofauti kubwa kati ya maisha ya zamani na maisha ya leo. Zamani elimu ilkua ikifungua maisha sawa sawa ulikua ukimaliza tu f4 lazima upate pa kujiweka sababu wasomi walkua wachache. Lakini Elimu kama ufunguo wa maisha ya sasa ni tofauti sana ikumbukwe kuwa kila nyumba kuna msomi either wa level ya cheti, stashahada au shahada na wengi wao wanatafuta ajira. Je serikali na kampuni bnafsi wanaweza kuajiri wasomi wote?. Ifikie wakati wazazi waanze kuwawezesha watoto wao ili waweze kujiajiri.
Ungekua jirani hapa,,,,ningemuagiza brian akununulie cocacola bariiiiid ushushie,,,umeongea point sana mkuu
 
Unachosema ni kweli, elimu inadumaza watu akili... Wanashindwa kufikiria vitu vya maendeleo na kutegemea kuajiriwa tu.

Nimewai ona kuanzia nurse hadi dactari tajiri. Ni jinsi anvyopanga maisha yake. Ukitegemea mshahara tu ndo unadumaa kiuchumi, ila kuna wanaofanya shughuli zingine pembeni. Aliekwambia mtu alie ofisini mda wote anashindwa kua na shughuli nyingine nani?? Unaajiri watu na kuendelea kula pesa pande zote mbili. Yaani kuna lecturers wapo vyuoni kila siku lakini pia ni wamiliki wa kampuni zinazoendelea vizuri, shule na mahoteli. Ni akili ya mtu pia...
Akili ya darasani ukiongeza na akili ya maisha unapata kitu amazing sana.
Yesiiii namna hii hivi ndo vichwa vinatakiwa kuolewa
 
Education is Power-Sir Francis Bacon.

Kuwa na Elimu tu ya Suala lolote ni Jambo la Msingi tofauti na Ujinga {Ignorance} katika namna yeyote ile.Ngugi wa Thong'o anakuambia "Hata umasikini ungeuzwa bei gani nisingeununua".Unapozungumzia vitu viwili ELIMU NA UTAJIRI kwa wakati mmoja ndiyo mwanzo wa kuifanya mada yako iwe Narrow sana Mkuu.

Hakuna Uhusiano wowote wa Elimu na Utajiri.Yaani namaanisha hivi,Unaweza kuwa na Elimu ya Juu kama ulivyoiita pale juu na usiwe tajiri.Pia unaweza kuwa Masikini na usiwe na Elimu ya Juu.

Kama kuwa na Elimu mbalimbali ni kuwa na Utajiri {Kwa maelezo yako pale juu} basi Maprofesa wote wangekuwa na Utajiri kwakuwa wao ndiyo wenye Elimu kubwa kuliko sie kina kabwela.

No research No right to speak.Kawafanyie tafiti Matajiri woote unaowafahamu ulimwenguni kote ambao kwa namna moja au nyingine hawakuipata Elimu sawasawa then uwaulize kuhusu Faida ya mtu kuwa na Elimu then usikie majibu watakayokupa.In short ni kuwa wengi wao wanajutia mno kutokuwa na Elimu so In general EDUCATION IS THE BEST THAN BEING IGNORANT BY ANY MEANS.

Suala lingine ni kwamba,Siyo lazima wote watakaosoma Elimu ya Juu wawe Matajiri.Wengine hawakwenda kuipata hiyo Elimu unayoiita ya Juu ili waje kuwa Matajiri.

I submit.
Point.vichwa safi kabisa mubashara safi mkuu
 
Mimi bado naamini elimu ni ufunguo wa maisha ila kuna tofauti kubwa kati ya maisha ya zamani na maisha ya leo. Zamani elimu ilkua ikifungua maisha sawa sawa ulikua ukimaliza tu f4 lazima upate pa kujiweka sababu wasomi walkua wachache. Lakini Elimu kama ufunguo wa maisha ya sasa ni tofauti sana ikumbukwe kuwa kila nyumba kuna msomi either wa level ya cheti, stashahada au shahada na wengi wao wanatafuta ajira. Je serikali na kampuni bnafsi wanaweza kuajiri wasomi wote?. Ifikie wakati wazazi waanze kuwawezesha watoto wao ili waweze kujiajiri.
Mshike sana elimu.tunasoma kuongeza maarifa sio kuwa matajiri
 
Ni kweli hakuna haja ya kuwa na wahitimu kibao wa elimu ya juu wasio na chochote cha kuchangia katika pato la nchi.Pia ni kweli tunge imarisha swala la veta na mafundi sanifu(mchundo) wa kutosha tungepiga hatua sana,maana hawa ndowatendaji kazi.

Pia ifahamike kwamba,swala la nchi za ulaya(USA) kufungua makampuni mengi Asia(China na India)sababu kubwa si tu wafanyakazi wa mishahara ya chini tu bali pia hata kodi za kufungua kiwanda ziko chini sana ukilinganisha na Africa.

Unaambiwa hivi,kufungua kiwanda Tanzania kodi zake ziko juu sana kuliko nchi zote za africa,sasa nani atakuja hapa kwetu.Ndosababu pia unaona viwanda hata vya magari vinafunguliwa Kenya na si Tanzania.Ukiwaeleza wana CCM wanakomaa na ujinga badala ya kuwasikiliza watu wanaoelewa.

Hatuwezi kuendelea kwasababu ya siasa nyingi na hatusikilizi wataalau wa ufundi na uchumi.Porojo za ki vyama na hasa CCM kutosikiliza wenzao hata kwa sekunde hazitatupeleka popote.

Chamsingi tuangalie,kama tunakodi nyingi zinazo either wakimbiza au kutokiwavutia wawekezaji,tuzirekebishe.
 
Mkuu nimekwelewa sana ila sijafiki swala la siasa ndani ya hoja yako
 
Ama kweli nimeamini hili jukwaa ni la watu wanaojitambua.kuna wadada wapo vzur asee ngoja ntafte mke jamii forum nazani atanzalia kipanga walahi heshima enu wadada wa jf msio olewa
 
Watu waliokosa elimu ndo wana maneno haya kwa sana ama waliokosa ajira ila wana vihela vidogo mfukoni. Hakna tajiri Wa kuandika maneno haya hapa maana anajua umuhimu Wa elimu ya juu kwa taifa . Yan mtu hajawahi kuvuka nje ya mipaka ya Tanzania na hana elimu yoyote ya kumpa ufaham Wa elimu na syllabus za wenzetu ila kwa kulinganisha elimu ya Tz na zingine ndo kazi yake , hivi unadhan Tanzania ndo imeweza kuwa na elimu ya kipekee na ya hovyo?? Tumeitoa wapi? Ebu twambie kuhusu elimu za nchi unazozikubali na mifumo yao na jinsi uinavyowasaidia kuwa matajiri! Hivi watu km wewe mtaacha lini kuwachukia wasomi wakati mnahangaika kuwapeleka ndugu na jamaa zenu mashuleni?? Vipi unajua Tz kuna wahitimu wangapi Wa degree au masters ukilinganisha na wale ambao hawana ili tujue kiwango cha maisha bora kati ya wasomi na wale failures?? Ndo wale mnaowasifia na kuwafanya role models wale failures wenye hela na badae mnaambiwa ni wauza madawa ya kulevya, makahaba, majambazi n.k mnashangaaaaa . Chuki dhidi ya wasomi haikufanyi kupewa degree ya bure.
 
Ss kila mtu akiacha kusoma,utajitibu mwenyewe ,miundo mbinu itajijenga,tekinolojia itajileta yenyewe,n.k watu wanasoma ili waje wahudumie jamii kwa matatizo ya kila siku wanayokumbana nayo sio utajir,hzo akili za utajiri ndo maana mwenyewe maskini,..
Kama hunawaona waalim matajir au madaktari au polisi tajiri ni ww,na punguza viroba hvo....
 
Una hoja kama utaliangalia hilo kwa haraka lakini ukifikiria zaidi yo wrong!!!

Okey watu waache,ualimu,udaktari,uasibu nk wakazisake pesa si ndio? Then mkishakua matajiri wote mkiugua nani atawatibu? Nyumba zenu nani atajenga? Umeme wenu nani atatengenezana nani atawafundisha hao, nk nk nk??

Hatuwezi kuwa matajiri wooote,tunaishi kwa kutegemeana, cha msingi waambie watu kuwa nini wafanye ili wajiongezee kipato zaidi na sio kuishia kuwa watumwa wa elimu.
 
Back
Top Bottom