Mjadala: Kipi bora kati ya kwenda Chuo au Advance Level (Kidato cha Tano na cha sita) kwa mwanafuzi aliyemaliza Kidato cha Nne?

Kwa ushauri Wangu nenda chuo usome certificate ya accountancy kwa mwaka moja, endelea na diploma ya accountancy kwa miaka miwili, ingia degree ya accountancy uipige kwa miaka mitatu, malizia kwa mitihani ya bodi ya cpa.

Au

Nenda advance usomee combination ya E.C.A kwa miaka miwili, ingia degree ya accountancy uipige kwa miaka mitatu, malizia kwa mitihani ya bodi ya cpa.

Nakushauri uende chuo, nilipitia hio njia ya pili siwezi kutumia cheti cha advance kuomba kazi na kuna kazi kibao za ma assistant accountant ambao inabidi uwe na diploma,

Njia ya kwanza iko poa sana, inajenga kukujengea msingi mzuri wa taaluma ya uhasibu toka chini, itakua utarudia kusoma masomo mengi uliyosoma certificate ukiingia diploma, hivyo hivyo utarudia kusoma masomo mengi uliyosoma certificate na diploma ukiingua degree, yani vitu vichache sana vitakua vipya tofauti na yule aloetoka form 6 anakumbana na masomo mengi mapya.

Pia wale wa form 6 wakifika chuo wana ushamba flani hivi wa kuwa na maisha ya Uhuru kitu ambacho huwa kinaweza kuwashusba kitaaluma, mambo hayo wewe utakua umeshayazoea. Pia kuandaa vitu kama assignments, kufanya presentations, kufanya practical maofisini, n.k kwa wale wa form 6 inakuja kitu kipya kabisa ila kwa aliesoma certificate na diploma ni marudio na wala sio kitu kipya
 
kuchagua kwenda chuo kuna faida kwamba unaamua mapema unasoma nini na kuweka jitihada zako hapo, unqpata experience mapema ya kile qmbacho unasomea , pia kusoma kitu ambacho unakipenda ni furaha maana unakuwa kama hauoni ugumu qa masomo bali unaona unapambania career yako, binafsi nimeaoma chuo na diploma na nikaenda degree na huko tupo wengi tu mkopo utapata kilq kitu hakutokua nq tofauti yako nq wengine waliosoma advance , faida yako kwako itakua kwamba tayari unacheti chako ndani ukiamuq muda wowote upumzike au ufanye kazi unaweza ,
 
kuchagua kwenda chuo kuna faida kwamba unaamua mapema unasoma nini na kuweka jitihada zako hapo, unqpata experience mapema ya kile qmbacho unasomea , pia kusoma kitu ambacho unakipenda ni furaha maana unakuwa kama hauoni ugumu qa masomo bali unaona unapambania career yako, binafsi nimeaoma chuo na diploma na nikaenda degree na huko tupo wengi tu mkopo utapata kilq kitu hakutokua nq tofauti yako nq wengine waliosoma advance , faida yako kwako itakua kwamba tayari unacheti chako ndani ukiamuq muda wowote upumzike au ufanye kazi unaweza ,
Nashukuru ila course gani ina soko kwa kipindi hiki

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kozi zipo nyingi hasa kama wewe uliyechukua masoma ya science usiwe na wasi lakini nakishauri uchague kile unapenda ambacho unaweza kuwa na ufanisi mzuri katika hicho, tofauti yangi na wanafunzi wengine me nafahamu mambo mengi sana sababu nimesoma diploma alafu napenda nilichosoma kitu ambacho kinafanya napata marks nzuri sana na naelewa kwa upana ninachosoma sababu nina passion nacho hata ikitokea interview sina haja ya kujiandaa sababu nachosoma kipo kwenye damu, ukwel ni kwamba hakuna taaruma isiyo lipa , wew pambana kuwa mjuzi katika fani yako.
 
dogo mm staki mm staki wewe ukariri nenda advance ukupate scientific concept zitakazoweza uwende deep kwenye field za afya, kilimo, mifugo, uhandisi form four chuo utakaririshwa tu maana maarifa nimakubwa mda wakusoma unaingiliwa ili kurahisisha wepita advance japo kua wengi watasema kupoteza mda ila kwa sababu wengi huwa wapo shuleni ili waende chuo ila sio wakusanye taarifa kwa sisi ndo tulivyo matamanio yetu ni kazi ila mm nakushauri Kama unataka kujiongoza mwenyewe science itakusaidi Sana Kama utaisoma kwa kuelewa kwenye nyanja nyingi Sana ha
 
Dogo chuo utasoma tu ila ukisha kwepa advance kuisoma Tena itakua noma Sana we nenda hata Kama hutafanukiwa kwenda chuo kikuu lakini utakuwa unawanja mpana mno utapata hata uwezo kujitafutia maarifa mwenyewe kwa sababu science ndio primary
 
Pambana na advance kwanza ,chuo utasoma tu .Ukiwahi saizi chuo unakuwa kama mbuzi aliyejipeleka machinjioni kuna mda utafika utatamani hata ingekuwepo tuition ya chuo uanze kusoma
GLU ™
 
nina mdogo wangu anataka kusoma kozibza afya kulingana na matokeo haya mnamshaurije? mana alnambia akienda advance anahofia akipelekwa kozi za arts.
bios B
chemistry D
geo C
English C
Kisw B
History B
civics C
mathe F
phys F.
naombeni ushauri wenu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
nenda chuo, wanaosema advance utapata vitu vingi, watakupoteza ni kweli utapata vitu vingi ila ni useless, chuo unapata vingi na usefull, hata vya advance pia vinafundishwa chuoni tofauti mitihani tu, chuo kuna kupima umeelewa nn, advance kunakukomoana maana ile ni daraja tu la kwenda chuo na wanahitaji watu wabaki, wakati chuo daraja la kwenda kwenye maisha na chuo pia so hawatumii nguvu nyingi kukubakiza

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mimi ni mwanfunzi nimehitimu kidato cha nne last year, binafsi napenda mambo ya Afya na Engineer

Mimi nimebalance comb ya PCB NA PCM ila kuna baadhi ya watu wamenishauri niende Chuo wengine A level.

Swali: Kama nikienda Chuo kuna tofaut na wa A level na pia nikichukua course ya afya eg co Je, huko mbeleni naweza kusoma coz kama za it au la

Yani naomben mnijuze zaidi mdogo wenu.
 
Wewe kama wewe hujiamini. Usiruhusu watu wakufanyie maamuzi. Wewe roho yako inakusukuma ufanye kitu gani?

Hao watu baadae hawatakuepo. Fanya unachopenda bwana we. Ukifanya unachopenda utaonesha ufanisi ambao utakufanya uwe mtu mkubwa baadae.
 
Inategemea uwezo wako darasani, malengo yako na uwezo wako kifedha. Fanya maamuzi sahihi kwa kuzingatia hayo.
 
Nenda chuo moja kwa moja kama uwezo wa kifedha upo vizuri ili uanze kusomea fani yako mapema.

Uzuri ukienda chuo unaweza somea, say, diploma ya electrical engineering then ukiamua kubadili unaweza kusomea, mfano, bachelor ya mechanical engineering.

So unakuwa una fani mbili kwa wakati mmoja hadi kufikia degree yako ya kwanza, hapo kwenye soko la ushindani unakuwa upo vizuri maana unafit sehemu mbili kwa wakati mmoja.
Hata ukiamua kukomaa na fani ulisomea kwenye diploma yako kwa ngazi ya degree haina shida pia unazidi kuwa nondo zaidi.

Hata ukienda A'Level na ukafaulu vizuri basi wote mnakutana mbele kwa mbele kwenye kulijenga taifa letu.

SUKAH
 
Wisdom Flag,
Ukisoma diploma ya Clinical medicine(,CO-Clinical officer) kwenye degree unachukua ya udaktari (Doctor of medicine) huwezi kwenda kwenye degree ya IT kwa kutokea kwenye diploma ya Clinical medicine. Kama utataka degree ya IT chukua diploma ya maswala hayo hayo ya IT au computer science/Computer engineering.

Kuhusu kwenda advance au chuo kiuzoefu tunaona chuo kuna faida zaidi kwa sababu unaenda kupata taaluma inayoenda kutumika moja kwa moja kwenye maisha tofauti na kupata cheti cha form six tu ambapo utategemea tena majaliwa ya kufaulu form six ili uende chuo na hizi kozi za afya au engineering kwa degree zina ushindani mkubwa mno mnoo unaweza upate One ya 9 bado ukose hiyo kozi kwasababu vyuo vina nafasi chache na wanaoomba ni wengi.
 
Nikiulizwa swali la hivi siku zote najibu nenda chuo kachukue fani utapata kazi kwa kutumia cheti ulichonacho cha diploma.

Nimefika chuo kwa kupitia advance sitamshauri mwanafunzi wa kozi yangu apitie form six ingawa kunafaida ya kuwa nondo sana chuoni kiperfomance ila kimaisha unachelew sana
 
Wewe kama wewe hujiamini. Usiruhusu watu wakufanyie maamuzi. Wewe roho yako inakusukuma ufanye kitu gani?

Hao watu baadae hawatakuepo. Fanya unachopenda bwana we. Ukifanya unachopenda utaonesha ufanisi ambao utakufanya uwe mtu mkubwa baadae.
Noted mkuu
 
Back
Top Bottom