Mjadala: Kipi bora kati ya kwenda Chuo au Advance Level (Kidato cha Tano na cha sita) kwa mwanafuzi aliyemaliza Kidato cha Nne?

rajesh

Member
Sep 30, 2014
17
0
1589185676542.png

BAADHI YA MASWALI YALIYOULIZWA NA WADAU KUHUSU JAMBO HILI
Mimi ni mwanfunzi nimehitimu kidato cha nne last year, binafsi napenda mambo ya Afya na Engineer

Mimi nimebalance comb ya PCB NA PCM ila kuna baadhi ya watu wamenishauri niende Chuo wengine A level.

Swali: Kama nikienda Chuo kuna tofaut na wa A level na pia nikichukua course ya afya eg co Je, huko mbeleni naweza kusoma coz kama za it au la

Yani naomben mnijuze zaidi mdogo wenu.
---
Habari zenu wakubwa.

Mimi naomba ushauri wenu nimehitimu kidato cha nne mwaka jana na nilipata division 2 nikiwa science na nina ufaulu ufuatao: Chem C, bios C, phy D, math D and so on.

Niliomba NACTE, Clinical officer ila bado post zao bado na za NECTA zimetoka nimepangiwa. Sasa sijui nifanyeje coz advance deadline tarhe 24/7 na chuo ni wa tisa. Ushauri wenu please
---
Habarini wakuu,

Nimekuja mbele yenu kuomba ushauri kwa hili.

Mimi ni muhitimu wa kidato cha 4 2015, posti zimetoka na nimepangiwa HGK. Hapo hapo nilisha apply Chuo Kozi ya Clinical Medicine. Je, niende Advance au nisubiri posti za Chuo?

Matokeo yangu yalikuwa hivi: Phy D, Chem C, Bios B, Hist C, Geo C, Kisw C, Eng C, Civ D, Math F.

Wasiwasi wangu nahofia kutokuchaguliwa chuo. Je, nifanyaje??

Nawasilisha kwenu wakuu.
1589188323695.png


BAADHI YA MAONI, USHAURI ULIOTOLEWA NA WADAU WA JF

1. WANAOUNGA MKONO SUALA LA KWENDA CHUO
Kama unandoto za udaktari baadae nenda chuo, mimi nimemaliza uhasibu SAUT na nimesoma science adv. Faida.

Kwanza unasomeshwa na serikali kozi za afya utachangia kidogo sana, pili hauna risk ya kupoteza future yako na kuja kuwa mwalimu si unajua kazi ya TCU au kufeli kabisa na kuanza na Cheti, tatu ukiomba TCU kuendelea baada ya Dip hautapelekwa kozi yoyote eti kisa vyuo vimejaa na ufaulu wa science mwaka huu upo juu bali lazima wewe upate nafasi ya kusomea udaktari.

kwanza tofauti na flesher na utashuhudia fleshers wanavyoenda biashara wakati wewe na mkopo utapata licha ya wao kusoma science.

Angalizo: usipofaulu phy, chem na Bios olevel kwa kuanzia kiwango cha C poteza ndoto za degree ya udaktari bali ukimaliza Dip ya CO utaweza kuendelea na kada nyingine za kiafya kwa ngazi za juu ila siyo MD.mengine mengi tu sifahamu endelea kutafuta msaada zaidi
---
Kuuliza tu hili swali. wewe una akili....KASOME CHUO....Ukimaliza tofauti na f.6 wewe utakuwa na skills za kuweza kuajiriwa lakini pia with a diploma utaingia kwenye kundi la wenye sifa ya kuitwa mwanataaluma yaani Professional kwa kimombo....faida nyingine utakayoipata ni kubobea ktk fani utakayoichagua hivyo kukupa fursa ya kufaulu saana degree yako kwa kuwa mengi utakayoyasoma kwenye diploma ndio hayo hayo, yanayoongezeka kwenye degree ni machache mno!
---
Nenda chuo moja kwa moja kama uwezo wa kifedha upo vizuri ili uanze kusomea fani yako mapema.

Uzuri ukienda chuo unaweza somea, say, diploma ya electrical engineering then ukiamua kubadili unaweza kusomea, mfano, bachelor ya mechanical engineering.

So unakuwa una fani mbili kwa wakati mmoja hadi kufikia degree yako ya kwanza, hapo kwenye soko la ushindani unakuwa upo vizuri maana unafit sehemu mbili kwa wakati mmoja.
Hata ukiamua kukomaa na fani ulisomea kwenye diploma yako kwa ngazi ya degree haina shida pia unazidi kuwa nondo zaidi.

Hata ukienda A'Level na ukafaulu vizuri basi wote mnakutana mbele kwa mbele kwenye kulijenga taifa letu.

SUKAH
---
Wisdom Flag,
Ukisoma diploma ya Clinical medicine(,CO-Clinical officer) kwenye degree unachukua ya udaktari (Doctor of medicine) huwezi kwenda kwenye degree ya IT kwa kutokea kwenye diploma ya Clinical medicine. Kama utataka degree ya IT chukua diploma ya maswala hayo hayo ya IT au computer science/Computer engineering.

Kuhusu kwenda advance au chuo kiuzoefu tunaona chuo kuna faida zaidi kwa sababu unaenda kupata taaluma inayoenda kutumika moja kwa moja kwenye maisha tofauti na kupata cheti cha form six tu ambapo utategemea tena majaliwa ya kufaulu form six ili uende chuo na hizi kozi za afya au engineering kwa degree zina ushindani mkubwa mno mnoo unaweza upate One ya 9 bado ukose hiyo kozi kwasababu vyuo vina nafasi chache na wanaoomba ni wengi.
---
Nenda chuo kijana, ukitoka hapo unaweza ukafanya kazi ya profession yako au utakayopendezewa nayo.

Au unaweza ukaunga bachelor degree moja kwa moja
na mkopo kama kawaida unapata.
---
Mdogo wangu ushauri ninaokupa njoo chuo either afya ya binadamu au ya wanyama we njoo mi nipo chuo cha mifugo nimeona uzuri wa chuo haina haja ya kukesha njo ufaidi elimu kwa vitendo sawa?

Ushauri ndo huo
2. WANAOUNGA MKONO SUALA LA ADVANCE
Advance ina hadhi yake bwana asikwambie mtu.

Chuo kikuu nilikutana na watu kutoka diploma walikuwa na viherehere na kujifanya wao ni werevu kuliko freshers.

Lakini baada ya muda tukawapiku maarifa na kuwa mabingwa kuliko wao.

Infact, unapata advantage mara mbili : Unapata hadhi ya kufika kidato cha sita, na ukifika chuo kikuu unakuwa na ujuzi sawa sawa na yule aliyetoka diploma, au unakuwa mjuvi zaidi yake.

Sio swala la nani kajua lini, ila nani anajua nini.

Kwenda advance kisha kufika chuo kikuu ni faida mara mbili.

Utaepuka fedheha ya kuonekana kilaza aliyefeli kidato cha nne.
---
komaa na Advnce, achana chuo utapoteza hela zako bure halafu elimu yenyewe diploma, piga kitabu advance kwa sababu ukimaliza utaenda degree direct na utasoma kilaini maana kutakuwa na mkopo.
---
Ukienda chuo ukiwa umemaliza form IV utasoma certificate ya clinical medicine mwaka 1, then utafanya diploma miaka 2. Baada ya hapo ndio utakuwa eligible kufanya degree of medicine.

Ukimaliza degree utakuwa general doctor tu sawa na huyu aliyesoma miaka 2 ya advanced halafu akaenda degree. Uzuri wa kufanya advanced unapata motivation ya kwenda degree haraka.
---
Acha walioenda shule waje, kwa ujumla kila kimoja kina umuhimu na faida zake.
A level inakuandaa zaidi kukabiliana na masomo ya chuo kwa wigo mpana, Diploma ni nzuri inakupa fani kuhusu eneo flani hata kama ukiishia hapo, una kaujuzi au kauelewa ka kazi tofauti fa A level.

Kama lengo ni kufika mbali kielimu bila kukatisha au kufanya kazi hapo katikati na una kichwa kizuri, nenda A level, lakini kama ni shake well before use, bora jiendee diploma, lakini napo uweke msisitizo na kuzingatia masomo haimaanishi huko ni mteremko.

Kila la kheri.
---
Nenda Advance ukimaliza, ndo utaenda Chuo kusomea hiko unachokitaka.

Ukisema uende Chuo now, ukasomee uhasibu, hapo unaweza kuanzia Certificate...sasa umalize Certificate, uje Diploma, uende Degree. (Miaka hiyo balaa).


Soma Advance, ni nzuri. Itakutoa haraka.
---
exactly! Kuna gap kubwa kati ya f4 na f6! Kunakuwa na knowledge leap! Mfano hesabu ukienda A level unasoma vitabu say Beckhouse 1 and 2.

Unaona kuna gap kubwa na vitabu vya O level... hivyo hivyo kwenye Biology... Plant and animal biology, gap kubwa na vitabu vya f4 etc.

Ukitoka form 6 university education inaungika vizuri.. ie continuation ni smooth
===
PIA UNASHAURIWA KUSOMA MJADALA HUU:
Kuna umuhimu wa kidato cha tano na sita? - JamiiForums
 

juma mkilindi

Senior Member
Jul 1, 2015
167
0
Nimemaliza form four mwaka jana.

Nikafaulu kwa daraja la merit (Nina B+ya bios na English, B ya history, Civ na phy, na C kwa masomo yaliyobakia ikiwemo math, phy, Geo na kisw)

Nilipangiwa EGM huko kagera ila matarajio yangu ni kua doctor.. nilishaapply chuo kwa course ya clinical officers kwa ngaz ya diploma kutokana na kua watu wengi walinishauri hivyo ila mpaka xx selection hazijatoka.

Wazazi wangu pamoja na ndugu wengine wanataka niende advance ila mm nilitaka kusoma PCB na wala cio EGM. .

Sasa naomba wadau mnisaidie kua niende tu shule nikapige EGM au nasubir selection?

Karibuni wadau..
 

Cereal Killer

Senior Member
Aug 17, 2015
131
225
Mkuuu adavance sio mchezo na unaweza ukaenda pcb na ukafaulu alafu ukaishia kuchaguliwa kozi nyingine..subiri selection mkuu
 

Ntaluke.N.

JF-Expert Member
Jun 21, 2015
1,341
1,500
Najua malengo yako ni mazuri,ila ushauri wangu ni kuwa ungeenda advance huku ukiendelea kusubiri majibu ya chuo,nasema hivyo kwasababu huwezi jua ya chuo ila kwa sasa changamukia fursa iliyopo kwa sasa.
 

wamidosho

JF-Expert Member
Feb 16, 2015
405
500
Njoo advance me mwenyewe nilikuwa na mawazo kama yako...uku ni juhudi zako tu mwenyewe mwisho wa siku unatoboa
 

barutirashid

JF-Expert Member
Jun 24, 2014
328
225
Kk advance uko kagera sidhani.
mm last year nimeacha pcb tunduru.nipo Clinical medicine mwaka wa 2.
Just ushauri tu.njoo huku.
 

Kaina

JF-Expert Member
Jul 3, 2015
371
500
Kwa sasa nenda Advanve kwanza wakat unasubiri matokeo ya chuo. Ukichaguliwa chuo ndo uache Advance maana unaweza kupoteza vyote! Pia kubadikisha combi kutoka EGM kwenda PCB inawezekana sana hata mimi nillibadilishaga cha msingi hiyo combi unayoitaka iwepo hapo shuleni. Work on this plz
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom