Ushauri: Niende kidato cha tano au chuo?

Kwenda fv utasoma miaka 2+3 jumla 5 unapata digree.


Chuo utasoma 3+3 jumla 6 unapata digree.
Kwani kasema lengo lake ni kupata degree??

Dogo aende chuo, apige certificate aende diploma then degree akitaka.

kwa nchi yetu hii unakua na uwanja mpana sana, kazi ikihitaji cert unaomba, ikihitaji dip unaomba, ikihitaji degree unaomba pia.

Nna washkaji wengi ambao wamepata kazi kwa dip au cert then wakiwa job wanaupdate cv zao.
 
Nenda chuo soma certificate na diploma. Utatoka na uwezo mkubwa zaidi kuliko aliyetoka A level na matakataka kibao kichwani akafaulu vizuri ila hatoyatumia.
Pia zingatia kufanya short courses na ukazane ufanye mitihani ya bodi ya uhasibu.

Fanya vizuri, toka Diploma nenda Degree. Soma zaidi na ufanye mitihani ya bodi pia. Hapo utamaliza Degree umeenda field jumla mara nne, uko certified na umesoma miaka 6 kitu kilekile utakuwa vizuri zaidi.

Sio ajabu kukuta mwenye Diploma anayesoma Degree akiwa na ajira (dada yangu kafanya hivi, akiwa first year akaomba kazi kimzaha akapata mkoani mbali uko akasitisha masomo akaenda, amekaa mwaka tu akaruhusiwa na mkurugenzi kumalizia Degree yake sababu chuo kilitaka kubadili mtaala asingekuja angeanza upya Degree).

Vilevile sio ajabu mwenye Degree kukataliwa kwenye job application hata akikubali mshahara wa Diploma. Na bado college mates wangu wengi waliopata ajira haraka ni waliopitia Diploma. Sasa mtu ana Dip ya DIT ya Computer Engineering kisha kaongeza Degree utamfananisha na mwenye Degree ileile aliyetoka A level PCM kwa ufaulu wa juu ila kakariri Benzene na Projectile Motion?
 
Daaah, umenifumbua kwa upana sana na nimeelew vizuri.
Asante sana🙏
 
Nenda f5 kijana, haya mambo ya certificate hadi digrii ni ujinga mtupu
 
Matokeo vipi? Kupenda kwako ni sawa ila kuna vigezo pia vya kusoma certificate au diploma. Kama una miswaki je?
 
Kwani kasema lengo lake ni kupata degree??

Dogo aende chuo, apige certificate aende diploma then degree akitaka.

kwa nchi yetu hii unakua na uwanja mpana sana, kazi ikihitaji cert unaomba, ikihitaji dip unaomba, ikihitaji degree unaomba pia.

Nna washkaji wengi ambao wamepata kazi kwa dip au cert then wakiwa job wanaupdate cv zao.
Hii imekaa sawa.
 
Back
Top Bottom