Mjadala: Kipi bora kati ya kwenda Chuo au Advance Level (Kidato cha Tano na cha sita) kwa mwanafuzi aliyemaliza Kidato cha Nne?

Advance kuna raha yake sana. Aliyepitia Advance akaenda Diploma kisha chuo, huwa tofauti sana na aliyetokea Advance moja kwa moja kwakuwa anakuwa ameongeza ujuzi fulani na uelewa wa mambo but connection pia ndugu, wengi wa wanaopitia Advance huenda chuo na hupata kazi nzuri mapema kwakuwa hawazunguki na hivyo tayari unakuwa na connection kupitia wana.

Chukulia mfano huu:-
Wewe ni Mwajiri na wamekuja vijana 2 ambao wamesoma course moja chuo na wamepata GPA sawa like 3.5 ila mmoja alipitia Diploma na mwingine direct from Advance.... Yupi utamwajiri ukizingatia katika Interview wote wameperform the Same?

Probably ni yule aliyepitia Diploma kwani nitamtumia pia katika mambo ambayo huyu asiyepitia Diploma hayajui.
Ningekuwa mkuu wa nchi ningepitisha utaratibu kuwa kila mwanachuo lazima apitie Diploma ndio asome Bachelor kwani huwajenga zaidi kiakili na uelewa wa mambo.
 
hizo kazi zinatoka wapi mkuu Sasa Kama hatutaki kuwekeza kwenye uvumbuzi na sio kwamba ukipita kungine ndio hakuna uvumbuzi ila f6 inaraisisha kazi kukuwezesha wewe uwanja mpana wakukusanya na kuchanganua maarifa toka sehemu mbalimbali mfano halisi ni India na u.k pia wao wana A level Sasa angali u.k imeingiza vyuo vitatu kwenye top ten ya vyuo vikuu duniani wakati nchi nyingine za ulaya zenye mifumo mnayo ing'ang'ania hazijaweka record. Angalia wahindi sio tu hapa tz dar ila ni international mfano halisi makampuni makubwa Kama Google,microsoft,Coca-Cola yameanza kuwaamini wahindi pia angalia wahindi katika sekta ya afya sio wahindi tu pia hata madaktari wakibongo wamekuwa wakipewa sifa kuwa wana uwezo just kutokana F6
Kimsingi unaangalia mfumo wa elimu unaoupita unakusaidiaje kufungua maisha n kufanikiwa.....soko la ajira likoje/malengo yako Ni kufika wapi/una msukumo gani kwenye elimu yako nk lkn tukiacha utani nani bongo hii hasomi Ili kulenga hela???
 
ni kweli lakini inabidi tubadilike itafika kipindi hata hizo kozi unazozisema Zina soko. Nazo sitakua zimejaa. Viwanda wanakuja kufunguwa wahindi, wachina, huku wabongo wenye nchi wanapokea pesa za kijungujiko
 
Wakuu habari,

Naomba mnieleweshe kidogo nataka ni kusomea Course ya Computer Science

Je nikimaliza form4 niende Advance Level au chuo kabisa kipi bora?
 
Mtoto kamaliza form 4 kwa sasa anakuomba ushauri aende wapi?

1) Form six (A -level)
2) Certificate ( chuo)

Wewe utamshauri nin kulingana na soko la sasa na kwanin?
 
Nazani kujiunga A level ni muhimu ili akili ikomae hasa ukizingatia wanamaliza shule wakiwa wadogo mno. Angalia baada ya A level ndio uwaze pa kumpeleka kutegemea matokeo yake.
 
Nazani kujiunga A level ni muhimu ili akili ikomae hasa ukizingatia wanamaliza shule wakiwa wadogo mno. Angalia baada ya A level ndio uwaze pa kumpeleka kutegemea matokeo yake.
Je is it guaranteed kwamba akitoka diploma au cheti atapata Ajira?? Na ishu nyingine ni kwenye ada ,wazazi wataweza kulipa ada ya chuo ??
 
Je is it guaranteed kwamba akitoka diploma au cheti atapata Ajira?? Na ishu nyingine ni kwenye ada ,wazazi wataweza kulipa ada ya chuo ??

Ndugu, usiweke kipaumbele cha ajira, watu wamelalia vyeti vya kila aina uvijuavyo na bado wanasota ajira. Ada ya chuo ni kulingana na uwezo wako! hapo jiangalie binafsi, pia angalia uwezekano wa kupata mkopo.
 
Kuwa na ujuzi Ni sahihi kabisa.wigo wa jira nakukatalia maana wengi wana kuona kama sio msomi
Mimi naona form6 ni shortcut unless umefail(div1. 3-6), wanangu tuliomaliza form 4 wote wakaend clinical medicine direct sasahivi nimeshawa-bypass,nampango, nasikilizia majibu ya appl za vyuo zinatoka 25th mwezi huu...😊
 
Kusema ukweli tusifichane, kama huna kipato kizuri, ukiingia advance PCB, na unandoto za kuwa doctor of medicine, inabidi upambane kivyovyote vile upate div1 point 3-7 unless otherwise ushazingua.
 
Kusema ukweli tusifichane, kama huna kipato kizuri, ukiingia advance PCB, na unandoto za kuwa doctor of medicine, inabidi upambane kivyovyote vile upate div1 point 3-7 unless otherwise ushazingua.
😂😂😂 tukwambie au tukuache?
Hiyo MD ni ndoto yako kweli au umeaminishwa kuwa Ndoto yako ni MD?
 
Back
Top Bottom