SoC02 Elimu taka isiyopewa umuhimu

Stories of Change - 2022 Competition

cilla

JF-Expert Member
Jul 15, 2011
369
296
ELIMU TAKA ISIYOPEWA UMUHIMU

1659376420249.png

(picha kutoka google photo)​

UTANGULIZI​

Taka taka kwa mujibu wa wikipedia huru ni Taka au taka taka (kwa Kiingereza: waste, trash, garbage, rubbish, junk) ni mabaki ya vitu, ni yale yanayobaki baada ya kuzalisha vitu, pamoja na yale yaliyotumiwa tayari na ambayo hayana matumizi tena. Mfano wa taka ni, mabaki ya chakula, plastiki vyuma nk.Katika jamii zetu mijini na vijijini taka tofauti zinazalishwa kutoka mahospitalini, sokoni, viwandani, shuleni na majumbani n.k

TAKWIMU ZINASEMA NINI?​

Kwa mujibu wa ofisi ya taifa ya takwimu, Dar es salaam pekee inatarijiwa kuzalisha taka mara dufu hadi tani zaidi ya elfu 12 ikifika mwaka 2025. Taka za majumbani ni 75% ya taka zote zinazozalishwa jijini Dar es salaam na sehemu kubwa ya taka hizo hutupwa kiholela kutokana na kuwa na utaratibu mbovu wa ukusanyaji na uteketezaji wa taka.Asilimia 70 za taka za majumbani ni taka za vyakula.

Jiji la Dar es Salaam linakadiriwa kuzalisha zaidi ya tani 4,600 za taka kwa siku. Kati ya hizo ni asilimia 45 hadi 50 tu zinazopokelewa katika dampo sawa na tani 1,200 – 2,000 ya taka zinazokisiwa kuzalishwa kwa siku ambapo taka zinazobaki huishia kwenye maeneo ya wazi, mitaro ya maji, barabara na makazi.

Taka ni changamoto karibu kila mahali kwa sababu tunaendelea kuzalisha taka nyingi sana. Na kama tunavyoona kwenye maeneo yanayotuzunguka, taka kutokana na plastiki, glasi na chuma haziozi.

AINA ZA TAKA​

Kuna aina nyingi za taka lakini kwa uchache kuna
  • Taka ngumu kama taka za chuma, bati, makopo na plastiki.​
  • Taka maji hii hufahamika kama maji machafu ambayo yanakuwa katika hali ya kimiminika mfano wa maji yanayotoka vyooni.​
  • Taka hewa ambayo wakati mwingine hujulikana kama hewa chafu taka hizi zinakuwa mfano wa moshi, kama moshi wa magari, moshi kutoka viwandani na moshi kutoka majumbani.​
  • Taka sumu ambazo mara nyingi hutokana na kemikali za sumu ambazo huathiri afya ya mwanadamu.​
(Lakini hapa tutazungumzia zaidi zile taka zinazo zalishwa majumbani.)

JITIHADA ZA SERIKALI KATIKA KUTOKOMEZA TAKA MBALIMBALI
Serikali inafanya jitihada mbalimbali kama kutunga sheria mbalimbali ili kutokomeza taka katika maeneo yetu. Pia Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais imepewa Mamlaka ya kusimamia na kuratibu masuala yote yanayohusu mazingira nchini kwa mujibu wa sera na sheria ya Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (Environmental Management Act) Na. 20 ya 2004 pamoja na kanuni zake. Pia sheria ya Afya ya Jamii (Public Health Act) na 1 ya 2009. Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na kanuni zake inazitaka halmashauri za manispaa, wilaya, miji na majiji kuweka mfumo bora wa kukusanya, kuhifadhi na kusafirisha taka.​

ELIMU TAKA ISIYOPEWA UMUHIMU NI IPI?
Tukiangazia taka zinazozalishwa majumbani ambazo ndio nyingi ,Pamoja na mipango mizuri ya serikali katika kudhibiti kuzagaa kwa taka katika miji na vijiji bado kuna changamoto mbalimbali zinazosababisha miji mingi kubaki katika hali ya uchafu na taka taka kuzagaa kwenye mito, mitaro, barabarani na katika vichochoro.

Moja ya jambo ambalo halionekani kupewa msisitizo na mkazo katika ngazi ya chini kabisa ya mzalishaji taka hasa majumbani ni kukosekana kwa elimu ya kutenganisha taka. Serikali na taasisi zake bado haitoi msukumo na na elimu yakutosha katika kuwaelimisha wananchi juu ya kuzitenga taka kulingana na asili ya taka zenyewe.

Elimu ya utenganishaji taka ni ujuzi wa namna ya kuzigawa/ kuzitenga taka katika vyombo vya taka mfano makombo yavyakula yanakuwa na chombo chake, makaratasi na maboksi yanakuwa na chombo chake, pia plastiki inakuwa na chombo chake tofauti. Kwa kufanya hivyo taka badala yakuwa taka zisizoweza kutumika sinaweza kuwa malighafi tena inayoweza kuuzwa tena au kuchukuliwa nakurudishwa kiwandani.

Kukosekana kwa elimu ya kutenganisha taka hasa majumbani kwa wazalisha taka kunasababisha ukusanyaji wa taka kuwa mgumu lakini pia kunatatiza urejelezaji wa taka(recycling). Taka kama Chuma, shaba, risasi, karatasi, plastiki, aluminiam, mpira na kioo na nguo huweza kurejelezwa na kutumiwa tena kama malighafi kwa mara nyingine. Taka ya elektroniki na mafuta pia huweza kurejelezwa kwa urahisi. Kurejelezwa kwa taka husaidia katika kulinda rasilimali.

Kutokutenganishwa kwa taka kunasababisha serikali kutumia mtindo wa kupokea taka na kushindilia (controlled dumping) na si dampo la kitaalam (Sanitary landfill) hali ambayo imesababisha milima ya taka kiasi cha ujazo wa mita 2-3 katika eneo la karibu hekta 45. Hali hiyo imekuwa ikisababisha ugumu wa kupanga taka, kuzisukuma hasa kipindi cha mvua na kusababisha kukwama kwa magari, mitambo kufanya kazi kwa shida hivyo kuhitaji matengenezo ya mara kwa mara pamoja na matumizi makubwa ya nishati ya mafuta.

Katika mataifa mengi yaliyoendelea na yanayoendelea, urejelezaji taka umekuwa ni njia mojawapo ya kudhibiti wingi wa taka zinazopelekwa dampo na umeweza kuongeza thamani ya taka. Njia hiyo imeweza kuhamasisha utenganishaji wa taka katika jamii kwani taka huwa mali ambayo watu binafsi na mwananchi mmoja moja hujiongezea kipato na kusaidia kusafisha mazingira kwa gharama nafuu. Maeneo ya viwanda na karakana za urejelezaji taka huweza pia kutengwa ndani ya maeneo ya dampo ili hupunguza shughuli za urejelezaji taka unaofanyika katika maeneo ya makazi.
1659377996279.jpg

(picha kutoka google photo)
FAIDA ZAKUTENGANISHA TAKA
Taka ni fursa. Mfano wa taka ni, mabaki ya chakula, plastiki navyuma.Viwanda vinaweza kupata vyanzo vya malighafi kutoka kwenye taka,mfano taka za chuma zitapelekwa kwenye viwanda vya chuma, taka zenye mabaki ya chakula zitapelekwa kwenye madampo na huko wanaweza wakatengeneza mbolea pamoja na gesi kwa matumizi ya nyumbani. Lakini sio hivyo tu, kwa taka zinazotokana na maboksi na karatasi kuna viwanda vyenye kuzihitaji pia, badala ya kuagiza malighafi kutoka nje ya nchi. Hii itasaidia kiuchumi na pia katika utunzaji wa mazingira kwani kutakuwa na uzalishaji mdogo wa taka nchini.

Taka hizo zinazozalishwa ingawa zinaonekana ni vitu ambavyo havifai kwa matumizi tena,lakini ni malighafi ambazo zina weza kutumika kwa maendeleo ya viwanda hapa nchini.​

NAMNA YA KUFANYA
  • Ni muhimu serikali Kutoa elimu ya kutenganisha taka zinazoweza kurejelezwa kwa kuziwekwa katika sehemu tofauti na taka ambazo haziwezi kurejelezwa. Hatua hii ni muhimu sana katika mchakato wa kurejeleza na ni jambo muhimu sana kwa taka zinazoweza kurejelezwa kuwekwa katika pipa maalum.
  • Wizara ya elimu inapoandaa Mitaala yetu ya shule ilichukulie jambo hili kama ni sehemu ya maarifa na ujuzi wa maisha wa lazima kwa kila mtu na kuliweka kama mada moja wapo katika masomo yetu mashuleni.​

Mwisho
 
Back
Top Bottom