Elimu nchini ipo mahututi

Elimu nchini ipo mahututi

Unachosema Mkuu Mr Rocky ni kweli kabisa, lakini pamoja na kuwa watoto wao ambao ni asilimia ndogo sana ya Watoto wa Tanzania hawasomi katika shule hizo lakini hakuna sababu yoyote ya kuiacha Elimu nchini ianguke kiasi hiki. Wanabwabwaja kwa dakika chache mjengoni kisha hakuna lolote la maana linalofanyika na huku elimu ikiendelea kuporomoka.

Mkuu BAK nani anayewaza hayo kwamba kuna mtoto wa mlala hoi kule chunya au kasulu ambaye anakalia jiwe au hana kitabu cha kiada au hana mwalimu wa kumfundisha au shule yake haina maabara
Wewe ndio unaona uchungu na elimu yetu ila waliokalia viti vya kunesa na kupigwa na kiyoyozi watoto wao wako shule za St nanihii na International School au wako Malaysia au South Africa au Uk wanasoma au wakiwa hapa bongo wako Feza au Tusiime na sio shule ya kijijini kwako ambako mwalimu akifuata mshahara shule inafungwa mpaka arudi
Bungeni mimi naitaga comedy maana hakuna wanachojadili wanapiga makofi na kugonga meza hata kwa upuuzi au kwa porojo za mchakato sijui tuko kwenye mpango ambako hizo comedy tumezisikia toka tunajua kuwa kuna bunge
And then viongozi wako kwenye ziara wanafuatilia utekelezaji wa ahadi na ilani za chama na kuangalia namna wanafunzi wanavyokaa chini kwenye vumbi wakati makampuni yao yanashindana kusafirisha mbao na magogo nje ya nchi kupata fedha za kigeni
Halafu BAK unajua ni aibu mbao zinatoka mikoani huko ila huko ndio kunaongoza kwa watoto kukaa kwenye mawe na sakafuni
 
Last edited by a moderator:
  • Thanks
Reactions: BAK

“Nina mtihani wa majaribio wa darasa la saba ambao haufanyiki. Niliwahi kumpa profesa mmoja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) ambaye alitumia saa mbili na nusu bila kupata jibu lolote la kuandika. Mtihani wenyewe haufanyiki,” alisema Mbatia na kutoa ofa ya Sh10 milioni kwa profesa mwingine yeyote bungeni ambaye ataweza kufanya mtihani huo na kupata alama 100.

Mbatia aache utani.......
hata aliye sekondari hawezi fanya mtihani wa darasa la saba na akapata 100% sembuse prof!
Ni kweli elimu imechakachuliwa sana na tunahitaji nguvu ya ziada kuitoa huko iliko, inasikitisha lakini ndo ukweli huo.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Bunge letu ni Bunge lililojaa usanii wa hali ya juu. Kinachoendelea pale mjengoni kinasikitisha sana.

Mkuu BAK nani anayewaza hayo kwamba kuna mtoto wa mlala hoi kule chunya au kasulu ambaye anakalia jiwe au hana kitabu cha kiada au hana mwalimu wa kumfundisha au shule yake haina maabara
Wewe ndio unaona uchungu na elimu yetu ila waliokalia viti vya kunesa na kupigwa na kiyoyozi watoto wao wako shule za St nanihii na International School au wako Malaysia au South Africa au Uk wanasoma au wakiwa hapa bongo wako Feza au Tusiime na sio shule ya kijijini kwako ambako mwalimu akifuata mshahara shule inafungwa mpaka arudi
Bungeni mimi naitaga comedy maana hakuna wanachojadili wanapiga makofi na kugonga meza hata kwa upuuzi au kwa porojo za mchakato sijui tuko kwenye mpango ambako hizo comedy tumezisikia toka tunajua kuwa kuna bunge
And then viongozi wako kwenye ziara wanafuatilia utekelezaji wa ahadi na ilani za chama na kuangalia namna wanafunzi wanavyokaa chini kwenye vumbi wakati makampuni yao yanashindana kusafirisha mbao na magogo nje ya nchi kupata fedha za kigeni
Halafu BAK unajua ni aibu mbao zinatoka mikoani huko ila huko ndio kunaongoza kwa watoto kukaa kwenye mawe na sakafuni
 
muheshimiwa supika jimbo langu lina matatizo kede kede ya elimu watoto hawana madawati vitabu havitoshi kwingine hakuna kabisa walimu nao ni tatizo kwan kuna shule nying jimbon kwangu zina upungufu mkubwa wa walimu. Lakini mh waziri naomba nikuhakikishie kuwa naunga mkono bajeti asilimia mia moja(100% ) makofi pwa! Pwa! Pwa! Pwa!

haaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa ccm ni hatari, yani nimekasirika mpaka nimejikuta nacheka.
 
Bunge letu ni Bunge lililojaa usanii wa hali ya juu. Kinachoendelea pale mjengoni kinasikitisha sana.
huwa natamani sana kusikiliza Bunge la budget, lakini kila ninapokuwa kwenye hiyo channel nashitukia tu nimeshabadilisha na kuingia kwenye FOOD!
Bora kujifunza kupika kuliko kusikiliza mapato na matumizi ya nchi yangu...... shame!
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kikwete is the root of all this. He is a reflection of the status of our education.

Simply put, he does not care. He rather spend his time with bongo flava artists than host lecturers at the state house.

He has a history of ditching presidential debates.

He is not interested, if he were, we wouldn't be where we are.

Kila mwaka wanafunzi wanafeli. Rais hajafanya lolote kubadilisha matokeo. Angalia watu wanaomzunguka Rais, kina Nape and company.

Huyo waziri mnamuonea, we don't have a serious president.
 
Yanini kupoteza muda wako kuwasikiliza wapuuzi. Wanaona elimu nchini inavyoanguka kwa kasi ya kutisha, na malalamiko wanayoenda nayo Bungeni kuhusu kuanguka kwa elimu yapo chungu nzima, lakini pamoja na hayo bado wanaunga mkono bajeti hiyo!!! Mie sioni hata faida ya kuwa na Bunge nchini.

huwa natamani sana kusikiliza Bunge la budget, lakini kila ninapokuwa kwenye hiyo channel nashitukia tu nimeshabadilisha na kuingia kwenye FOOD!
Bora kujifunza kupika kuliko kusikiliza mapato na matumizi ya nchi yangu...... shame!
 
Mimi huwa siamini kama CCM, mawaziri wake na uongozi mzima wa serikali hawajui watendalo! Sidhani kama wabunge hawajui kwamba kuna walimu wanapokea chini ya 250k kwa mwezi, halafu wao wanapitisha 300k kwa siku. Sidhani kama wabunge (BMLK)wangekuwa na uchungu, wangetumia karibu miezi miwili kutengeneza kanuni huku zaidi ya milioni 200 zikitumika kila siku. Fedha hizi zingeweza kuweka vitabu vya kiada na ziada kwenye mamia ya shule!
 
Mwisho wa siku bajet ikapita bila mabadiliko siyo?

Hamna kitu hapo , watanzania tuandike tumelwa.
 
Mnachagua wakwere kuongoza nchi halafu mnategemea nini. Mpaka hapo mtakapokubali kutawaliwa na watu wenye akili ndiyo mtaendelea
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Chezea wakwere wewe!labda tuombe Mungu siku moja aweza patikana kiongozi atakayejali elimu na walimu lkn kwa Magamba nimenawa maji.
 
Hakukosea kabisa Mnyika alipomuita DHAIFU, uongozi wa nchi umemshinda kabisa anaendekeza uVDG huku kila kitu nchini kikiwa katika hali ya kusikitisha na deni la Taifa la ndani na nje ya nchi likizidi kuongezeka kwa kasi ya kutisha na wanachofanyia hizo pesa wanazozikopa hakionekani.

Mnachagua wakwere kuongoza nchi halafu mnategemea nini. Mpaka hapo mtakapokubali kutawaliwa na watu wenye akili ndiyo mtaendelea
 
Halafu wenyewe bila hata aibu na woga wanakuja na kauli zao za, "Tumethubutu, tumeweza na sasa tunasonga mbele." Wakati nchi iko mahututi sijui wanasonga mbele kuelekea wapi!!

Kila kitu kiko hoi. Sio elimu, afya, maji, na miundombinu (usafirishaji per ce). Mgonjwa wa kufa huyu, hata drip haiendi!
 
Sekta ya elimu inahitaji tiba nzito


By Mhariri

20th May 2014

Katuni%20(34).jpg

Katuni


Kama ilivyokuwa mwaka jana kipindi kama hiki, bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi ambayo safari hii iliwasilishwa bungeni Jumamosi iliyopita jioni na Waziri Dk. Shukuru Kawambwa, wabunge wameonyesha kutokuridhishwa na mustakabali mzima wa elimu nchini.

Wapo wanaohoji hatua zinazochukuliwa kunusuru hali ya elimu nchini, wapo wanaohoji kasi ya serikali katika kukabiliana na changamoto za elimu hasa kuzidi kuporomoka kwa ubora wa elimu na pia kuhoji kama tiba ya matatizo hayo ni kupunguza viwango vya ufaulu kwa kurejesha chini zaidi wakati mataifa mengine yalipandisha viwango hivyo.

Wabunge wengi kama ambavyo hata Waziri wa Elimu mwenyewe alikiri, wamehoji juu ya upungufu wa walimu hasa wa sayansi na hisabati, ukosefu wa maabara katika shule nyingi, walimu kutokulipwa stahili zao, kuendelea kuwa na shule ambazo hazina sifa za kuitwa hivyo kwa sababu ya uchakavu wa miundombinu, ukosefu wa vifaa kujifunzia vikiwamo vitabu vya kiada na ziada.

Wabunge wengi walihoji sababu za kuyumba mno kwa kitengo cha ukaguzi katika shule kiasi cha kueleza kuwa ndicho kiini cha kushindwa kubadili mwelekeo wa kuporomoka kwa elimu nchini.

Akiwasilisha bajeti hiyo kwa mwaka wa fedha wa 2014/15, Waziri wa Elimu alisema kuwa zipo hatua kadhaa za kisera ambazo serikali imechukua kukabiliana na hali hiyo, miongoni mwake alitaja kuwa ni kukamilisha rasimu ya awali ya Muswada wa Sheria ya kuanzisha Bodi ya Kitaalamu ya Walimu Tanzania na kuiwasilisha katika Sekretarieti ya Baraza la Mawaziri ambapo imeshajadiliwa na sasa rasimu ya pili imekamilika kwa ajili ya kuwasilishwa kwenye kamati ya kitaalamu ya Makatibu wakuu (IMTC).

Kawambwa pia alisema kuwa kazi nyingine ni kukamilisha rasimu ya Muswada wa Sheria ya kuanzisha Mamlaka ya Ithibati na Uthibiti wa Ubora wa Elimu Msingi na Sekondari ambako shughuli mbalimbali hususan za ubora wa elimu zitaratibiwa na kusimamiwa. Rasimu hiyo itajadiliwa na wadau na kuwasilishwa katika mamlaka husika kwa ajili ya kukamilishwa kuwa sheria.

Alisema pia wamekamilisha na kuwasilisha katika Ofisi ya Rais - Menejimenti ya Utumishi wa Umma Muundo wa Utumishi wa Walimu katika kada mbalimbali na pia muundo wa uongozi katika ngazi za elimu ya msingi, sekondari na ualimu ikiwamo ukaguzi.

Katika hotuba hiyo, Waziri alianisha mikakati mingi sana ya kisera na kiutawala katika kunusuru sekta ya elimu nchini. Ingawa kimtazamo sera na mikakati hiyo inaonekana kuwa na maana, baadhi ya wabunge walisema kuwa imekuwa ni mchezo huo huo mwaka baada ya mwaka, lakini inapokuja suala la utekelezaji hakuna kinachofanyika.

Kwa mfano, suala la ithibati Waziri analaumiwa kwamba mwaka jana Machi aliahidi kuwa kazi hiyo ingelikuwa imekamilika, lakini hadi sasa mwaka mmoja baadaye kazi hiyo haijakamilika, huku Bunge likipewa maelezo ambayo hayatekelezwi.

Kimsingi kila anayefuatilia kwa karibu sekta ya elimu nchini hawezi kukwepa kuwa na hitimisho kama waliliokuwa nalo baadhi ya wabunge jana, kwamba elimu ya nchi hii siyo jambo la kuwasumbua vuongozi wetu serikalini kwa kuwa haiwahusu sana wao na watoto wao.

Baadhi ya wabunge walisema viongozi wengi serikalini wakiwamo wabunge, watoto wao hawasomi Tanzania, hawaathiriwi na kuporomoka kwa ubora wa elimu, athari hizo ni kwa wananchi wa kawaida ambao wanasomesha watoto wao katika shule za msingi za serikali, shule za sekondari za kata; pia madhara haya hawahusu hata wale wanaopeleka watoto wao shule za binafsi za humu humu nchini kwani viwango na ubora wa shule hizo binafsi ni wa juu mno kulinganisha na za serikali.

Kwa kila aliyepata fursa ya kutembelea nchi yoyote makini duniani, iwe imepiga hatua kubwa zaidi za maendeleo au kidogo, almradi ni nchi makini, hakika huduma za elimu bora zinapatikana kwenye shule za umma.

Ni kwenye shule za umma kwa sababu ndiko serikali huwekeza fedha nyingi kwa maana ya kuwa na walimu wazuri na bora na kuwa na vifaa vya kufundishia vya uhakika zaidi. Ni uwekezaji katika huduma muhimu kwa umma.

Kwa Tanzania kila kitu kinaonekana kwenda kinyume cha uzoefu wa wengine waliopiga hatua hata kinyume cha ilivyokuwa miaka ya nyuma kati ya 60 hadi 80; kila mahali serikali kwa makusudi inajiondoa kwenye wajibu wake wa kutoa huduma muhimu za kijamii; kama elimu, afya, barabara, maji na mawasiliano kutaja kwa uchache tu.

Tunafikiri kelele za wabunge hawa zitoshe na kwa kweli serikali ama iache kiburi na ikubali kubadilika vinginevyo kuupuuzia elimu kwa kiwango hiki, taifa hili linazidi kuangamia.

SOURCE: NIPASHE
 
mbatia ana akili kidogo

Akili zako ziko TUMBONI. Watu tunaongelea suala nyeti la kitaifa, wewe unakuja kutuonyesha UZEZETA wako. Jaribu kuficha ujinga wako angalau kidogo tu.
 
Hiyo ndio tofauti ya Mbatia na Lema. Wote si mawaziri vivuli, ila Mbatia anajua nini anafanya ila Lema ni box tupu limepewa nafasi kwasababu ni kabila moja na Mbowe.

nenda kaokote makopo wewe kichaa. kwanini unalazimishia ban wewe mwehu?
 
Back
Top Bottom