Theorist Mosses
JF-Expert Member
- Jul 16, 2022
- 345
- 253
Utangulizi
Sayari yetu ya dunia ni sayari ya tatu kati ya nane kwenye mfumo wetu wa nyota inayoitwa jua. ambayo ni sayari pekee inayo sapoti maisha iliyo bahatika kuwa na matabaka mazito ambayo ni anga hewa. lakini katika matabaka hayo siyo sehemu zote binadamu anaweza kuhimili hewa kuna kaeneo kadogo sana kanaitwa biosphere kwa kiswahili ni ile sehemu yenye hewa ambayo mtu anaweza kupumua kupata uhai "greenhouse" hapa ndipo tunasema pana sapoti maisha.
Ufafanuzi
Anga, ni uwazi ambao ndiyo umechukua nafasi kubwa ulimwenguni. Anga ndiyo imebeba kila kitu ikiwemo mfumo wote wa jua "solar system" na nyota zote ikiwemo sayari yetu ya dunia ambapo ndani yake ndiyo kuna gesi ambazo tunaita hewa kwahiyo anga siyo hewa.
Hewa, ni muunganiko wa gesi nyingi nyingi ambazo zipo kwenye anga. Kama vile hydrogen, oxygen, CO2, SO2, H2S, CH4, NH3 gesi hizi zimeundwa kwa atomi ambazo ni vipunje punje vidogo vigumu Kwahiyo hewa ni gesi siyo anga.
Atomi, ni vipunje vidogo vidogo sana kuzidi kipunje cha mchanga ambavyo ndiyo gesi yenyewe sasa. atomi imeunda vitu vingi sana kama vile gesi, moto, sumu, umeme, gari, ndege, radi na vitu vyengine vingi naomba tuzungumzie kuhusu umeme wa radi.
Radi
Ni umeme mkubwa sana ambao unapatikana kwenye matabaka mazito ya anga hewa wenye kuzalisha nguvu za umeme hadi kufikia voltage milioni 200 ampere 30000 kwa kila shoti moja ya radi, ambao ni mkubwa sana kuliko umeme wa tanesco wenye voltage 200 ampere 10.
Tuangalie sasa namna ambavyo umeme wa radi uzalishwa na matabaka ya anga hewa na nitakupa ushauri wa kisayansi namna unavyo weza kujikinga na kuwakinga wengine kuhusu umeme wa radi.
Jinsi matabaka yanavyo zalisha radi
Nyota yetu jua ndiyo chanzo kikuu cha maisha na nishati ya joto na mwanga kwenye mfumo wetu wa jua "solar system" ambapo ndani yake ndipo sayari yetu inayoitwa dunia inapatikana. Tunapata nishati ya joto kutoka kwenye nyota jua kwasababu ndiyo nyota iliyo karibu zaidi na dunia ukilinganisha na mabilioni ya nyota yaliyopo mbali ambayo tuna ya shuhudia mwanga wake hafifu wakati wa majira ya usiku.
Nyota yetu inapo zalisha joto lake usafiri kwa njia ya mawimbi moja kwa moja mpaka kwenye matabaka yaliyopo duniani Kumbuka kazi moja wapo ya matabaka ya anga hewa ni kichuja mionzi mikali itolewayo kutoka kwenye jua. katika mchakato wa kuchuja mionzi ya jua kuna baadhi ya mionzi hafifu itolewayo na jua ufanikiwa kupenya kwenye tabaka zito la hewa hadi kutufikia ardhini.
Mionzi iliyo fanikiwa kufika ardhini upelekea joto ambapo kukiwa na joto maji huvukizwa na kuwa mvuke hatimae kupanda tena kurudi kwenye anga hewa, ambapo hukutana na mawingu yaliyo katika hali ya unyevu nyevu basi nayo upoa na kuwa mawingu. kwahiyo kule juu kunakuwa na mpangilio wa mawingu ya aina mbili mawingu ambayo tayari yapo juu na mawingu yanayo panda.
Uwepo wa mawingu ya aina mbili kwenye anga hewa itafanya mawingu ambayo tayari yapo juu kuwa mawingu mazito na mawingu yanayo panda kuelekea juu kuwa mawingu mepesi. Mawingu mazito yanakuwa na matone tone ya maji itafanya kuwa na chaji chanya au hasi "postive, negative" na mawingu mepesi yenye mvuke mvuke pia kuwa na chaji chanya au hasi kwahiyo kunakuwa na mawingu mawili yenye chaji tofauti tofauti.
Mawingu, ni hewa au gesi iliyo katika hali ya unyevu nyevu ambao huo unyevu ndiyo maji au "mvua" ambapo maji ni muunganiko wa gesi mbili oxygen, hydrogen.
Katika ufafanuzi mwanzo nilisema hewa ni gesi iliyo undwa na vipunje punje "atomi" sasa vipunje punje hivi navyo vimegawanyika ndani yake siyo kitu kimoja. Ndani yake kuna neutron, electron, protons ambavyo vimeunda atomi. Vipunje hivi vina kamilisha atomi kuwa na chaji hasi na chanya kwamba vipunje hivi ndiyo chanzo cha umeme hata kwenye simu yako vipo vipunje vya atomi vinavyo sababisha simu yako kuwaka.
Turudi kwenye mawingu tumesema kuna mawingu ya aina mbili na yote yana vipunje vya atomi ambavyo vina chaji. kwamba kuna mawingu mazito yaliyopo juu tayari yenye chaji chanya na hasi, mawingu mepesi yanayo panda yenye chaji chanya na hasi.
Endapo mawingu haya mawili yatakapo tofautiana mikondo ya chaji itasababisha shoti ambayo ndiyo umeme wa radi. Hebu tuchukulie mfano kwamba tuna gusanisha nyaya mbili zenye umeme chanya na hasi lazima itatokea shoti hapo, ambapo hiyo shoti ndiyo mfano wa umeme wa radi unavyo tengenezwa na matabaka ya anga hewa.
Madhara
• Radi linaweza kupiga kwenye makazi ya watu. Hili ni tatizo ambalo linaweza kuleta maafa kwa watu ikiwemo kwenye makazi, biashara au hata kupelekea uharibifu wa mashamba, mifugo na mazao.
• Radi linaweza kusababisha magonjwa ya mshtuko wa moyo. Hili ni tatizo ambapo linaweza kupelekea mtu kuwa na magonjwa ya moyo kutokana na ngurumo kali ziambatanazo na radi.
• Radi linaweza kumharibu mtu kisaikolojia. Hili pia ni tatizo ambapo linaweza kupelekea mtu kuwa na wasiwasi kushindwa kujiamini kutokana na hofu hivyo linaweza kupelekea tatizo la kisaikolojia.
• Radi linaweza kuyumbisha uchumi. Hili ni tatizo kwamba radi linaweza kupiga kwenye sehemu muhimu za uwekezaji na kusababisha uharibufu ambao unaweza kuchochea kuyumbisha uchumi.
(Pichani ni Habari mtandaoni kuhusu madhara ya radi)
Ushauri
• usimruhusu mtoto wako kucheza au kumtuma dukani wakati wa mvua na radi. Unashauriwa kutokuwa unamtuma mtoto wakati wa mvua na radi ili kuepusha maafa yatokanayo na umeme wa radi.
• Usiwe unapanda minazi au kuwa karibu na nguzo za umeme wakati wa mvua na radi. Unashauriwa kuwa mbali na miti mirefu ambayo kwa asilimia kubwa radi upiga maeneo hayo itasaidia kujiweka salama zaidi.
• Zima simu yako au chombo chochote kinacho tumia umeme wakati wa mvua na radi. Unashauriwa kuwa unazima simu wakati wa mvua na radi kwasababu radi ni jamii moja ya umeme unao patikana kwenye vyombo vya umeme wa majumbani.
• Usikae sehemu zilizo binuka sana wakati mvua na radi. Unashauriwa kushaka kwenye maeneo yaliyo binuka zaidi kama vile milimani itasaidia sana kujiweka salama na madhara yatokanayo na radi.
Hitimisho
Elimu ya radi niliyo elezea kwa namna moja au nyengine itachangia kwa kiasi chake katika kupunguza majanga ya umeme wa radi na kuleta mabadiliko chanya kwenye nyanja mbalimbali katika jamii.
Ushauri
• usimruhusu mtoto wako kucheza au kumtuma dukani wakati wa mvua na radi. Unashauriwa kutokuwa unamtuma mtoto wakati wa mvua na radi ili kuepusha maafa yatokanayo na umeme wa radi.
• Usiwe unapanda minazi au kuwa karibu na nguzo za umeme wakati wa mvua na radi. Unashauriwa kuwa mbali na miti mirefu ambayo kwa asilimia kubwa radi upiga maeneo hayo itasaidia kujiweka salama zaidi.
• Zima simu yako au chombo chochote kinacho tumia umeme wakati wa mvua na radi. Unashauriwa kuwa unazima simu wakati wa mvua na radi kwasababu radi ni jamii moja ya umeme unao patikana kwenye vyombo vya umeme wa majumbani.
• Usikae sehemu zilizo binuka sana wakati mvua na radi. Unashauriwa kushaka kwenye maeneo yaliyo binuka zaidi kama vile milimani itasaidia sana kujiweka salama na madhara yatokanayo na radi.
Hitimisho
Elimu ya radi niliyo elezea kwa namna moja au nyengine itachangia kwa kiasi chake katika kupunguza majanga ya umeme wa radi na kuleta mabadiliko chanya kwenye nyanja mbalimbali katika jamii.