Elimu inasaidia vipi ukuaji wa uchumi?

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,510
2,000
Hello JF,

Ningependa kujua jinsi elimu inavyosaidia ukuaji wa uchumi...

reason being,

watu huku mtandaoni wamekua wakilalamika Rais kununua Ndege na kuacha ku invest kwenye Elimu..

sasa kwa faida ya wengi,,pamoja na Rais..

Mtuambie kwa nini elimu iwe kipaumbele na inavyofanya kazi katika kukuza uchumi..

Msigoogle :D:D:D:rolleyes::rolleyes::rolleyes:
 

GoPPiii.

JF-Expert Member
Oct 6, 2014
1,480
2,000
Elimu ina mchango sana kwenye ukuaji wa uchumi kwa sababu...

1. Huleta ujenzi,utumiaji na usimamizi wa viwanda na miundo mbinu mfano Barabara,Anga na Maji.

2. Elimu hustaarabisha watu mfano Uzingatiaji wa afya hii hufanya uwepo wa nguvu kazi yenye afya,uzazi wa mpango,n.k

3. Elimu huzalisha kada mbali mbali,mfano madaktari,wanasiasa,polisi na wanasheria. Wanasiasa waliosoma wakaelimika au wanasheria wakasoma wakaellimika hufanya mambo mengine kusonga katika nchi. Kama vile wasemavyo Siasa ni kila kitu.

4. Elimu hufungua fursa za kiuchumi,ni rahisi kupata fursa ukiwa na Elimu.

Eti mleta uzi ingekuwa ni essay hapa nina marks ngap!?

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Rebeca 83

JF-Expert Member
Jun 4, 2016
12,510
2,000
Elimu ina mchango sana kwenye ukuaji wa uchumi kwa sababu...

1. Huleta ujenzi,utumiaji na usimamizi wa viwanda na miundo mbinu mfano Barabara,Anga na Maji.

2. Elimu hustaarabisha watu mfano Uzingatiaji wa afya hii hufanya uwepo wa nguvu kazi yenye afya,uzazi wa mpango,n.k

3. Elimu huzalisha kada mbali mbali,mfano madaktari,wanasiasa,polisi na wanasheria. Wanasiasa waliosoma wakaelimika au wanasheria wakasoma wakaellimika hufanya mambo mengine kusonga katika nchi. Kama vile wasemavyo Siasa ni kila kitu.

4. Elimu hufungua fursa za kiuchumi,ni rahisi kupata fursa ukiwa na Elimu.

Eti mleta uzi ingekuwa ni essay hapa nina marks ngap!?

Sent using Jamii Forums mobile app

tehee teheee marks zako ni 0.000000000000000000000000011 lol,Asante kwa mchango wako..
 

Ocran

JF-Expert Member
Jun 29, 2017
1,019
2,000
Elimu inatoa ujinga, inakupa uwezo wa kufanya jambo lolote kwa umakini na ufasaha zaidi, kuanzia kwenye kilimo,uvuvi na uzalishaji wowote ule, shuhuli za maendeleo na huduma kwa jamii, unaweza sema mtu msomi kufanya mabaya au mtu sio msomi kufanya vzr lakn hii inatokea kwa wachache sana

Sent using Jamii Forums mobile app
 

1000 digits

JF-Expert Member
Oct 16, 2012
4,995
2,000
Elimu bora sio bora elimu.
Na ni lazima tuwekeze kwa malengo.
Mfano Bila elimu Tusingekua na Wataalam waliopo pale Muhimbili ambao walipelekwa kusoma nje wakati wa JK kwa malengo ya kupunguza gharama za kupeleka wagonjwa nje.

Ilibidi sasa tuhamie kwenye wahandisi wa madaraja, majengo,Magari,viwanda ,n.k
Wakasome nje ya nchi ili waibe Teknolojia waje kujenga nchi.

Sio kuwekeza kwenye elimu bure ya kisema Tanzania ilipata Uhuru mwaka gani.
Tunapoteza miaka mingi kwa kuwekeza kwenye elimu isiyo na tija ambapo ingewezekana kuwa ni vipindi tu vya kwenye Radio na TV kutoa elimu hiyo na sio kukaa Darasani kwa gharama kubwa bila maana yoyote.

Hata kwa historia tu ile mikoa iliyotangulia kupata elimu ndiyo yenye maendeleo makubwa.
Elimu inawafanya watu wanashindana kufikiri na kutatua changamoto zinazowazunguka kwa urahisi na kisayansi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

fazili

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
7,363
2,000
Mikataba ya hovyo tuliyoingia na kusababisha upotevu wa matrilioni ya shilingi inatokana na ukosefu wa elimu nzuri ya uchumi, mikataba na madini.
 

Mother Confessor

JF-Expert Member
Jan 7, 2016
17,386
2,000
Kwanza kama tunataka Elimu iwe kipaumbele kama Taifa,.lazima serikali ijipange na itambue kuwa watu/wananchi wake tunahitaji Elimu bora na sio bora Elimu...hapo ndipo tutaona faida ya Elimu kwenye kila nyanja ikiwemo uchumi,biashara,uwekezaji,kilimo n.k..
 

delta_state

Senior Member
Sep 24, 2015
172
225
Elimu ina mchango mkubwa sana katika maendeleo ya Taifa lolote
Sio tu kwa waliofaulu bali hata kwa wale wanaopita katika system ya elimu..walioishia la saba mtu alieishia la nne ilimradi anajua kusoma na kuandika..waliofeli form 2 ama form 4 ili mradi kapita katika mfumo wa elimu

1.kwa anaejua Kusoma na Kuandika tu..
---> huyu mchango wake katika uchumi ni kununua magazeti,vitabu na majarida mbali mbali..kifupi atakua market kwenye vitu hvyo kwahyo atasaidia kukuza uchumi
--->Ataweza kupata ajira ya ukarani mbali mbali..hasa maeneo ya kuegesha magari..atapata fedha na kukusaidia katika mzunguko wa fedha
--->Anaweza kua mbunge,diwani,mwenyrkiti wa kijiji...hivyo anawezatumia wadhifa wake kuhamasisha maendeleo..lakini pia anawezatumia fedha zake na kua act kama market ni kulipa kodi na hatimae kuleta maendeleo
--->Anaweza pia kua soko katika vitu mbali mbali
●matunda,mboga mboga,biscuits,chocolate
Kwa mtu aliepitia shule kidogo anakua na uelewa kutumia mboga mboga matunda kuliko mtu asieenda shule kabisa
--->ataweza kutumia saa kwahyo anakua soko..hivyo atasaidia kukuza uchumi
Mtu asiejua kusoma si dhani kama anaweza kununua saa

Hayo ni baadhi tu kwa mtu aliepata elimu ya kujua Kusoma na Kuandika..vipi kwa wale waliopata elimu zaidi


Sent using Jamii Forums mobile app
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom